ALIYEKUWA kocha mkuu wa timu ya Azam FC, Mcameroon Joseph Omog
ameanza mazungumzo na uongozi wa klabu ya Simba kwa ajili ya kuja nchini
kuifundisha timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Simba
imeanza mazungumzo na kocha huyo baada ya kocha chaguo la kwanza Sellas
Tetteh, raia wa Ghana kuwapa masharti magumu, kabla ya kuzungumzia dau
la mshahara analotaka kulipwa kila mwezi.
Mmoja wa viongozi wa juu
wa Simba (jina tunalihifadhi) alisema kuwa klabu hiyo imechemsha
kuendelea na mazungumzo na Tetteh kwa sababu alikuwa anauliza vitu
ambavyo timu hiyo haina. Chanzo chetu kiliendelea kusema kuwa kutokana
na mahitaji muhimu yaliyoulizwa na kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa
ya Rwanda (Amavubi) kukosekana, Simba iliamua kusitisha mazungumzo na
mkongwe huyo.
“Kuhusiana na usajili, tumejipanga, tunafanya usajili kwa kushirikisha jopo na si mtu mmoja mmoja, wapo wachezaji na makocha wa zamani ambao wana mapenzi ya kweli na Simba,” kiongozi huyo alisema.
Wekundu hao wa Msimbazi pia walikuwa katika mazungumzo na Kalisto Pasua, lakini Mzimbabwe huyo ameikacha ofa ya Simba na kuendelea kuiongoza timu yake ya Taifa ambayo imefuzu kushiriki fainali za Kombe la Afrika mwakani. Simba ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita nyumba na mabingwa Yanga na Azam.
0 comments:
Post a Comment