Taarifa kutoka Ghana zinaleza kuwa, wapinzani wa Yanga katika kundi A Medeama SC iko mbioni kujitoa kwenyemichuano ya Shirikisho Afrika kutokana na kukumbwa na ukata mkubwa. Hii ni kwa mujibu wa Meneja Tawala wa klabu hiyo Bejamin Kessie.
Klabu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Tarkwah wanataraji kucheza na TP Mazembe-Congo katika mchezo wao wa awali hatua ya makundi utakaopigwa June 17 jijini Lubumbashi.
Hata hivyo, Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) bado halijatoa fedha za kujikimu kwa klabu zote zinazoshiriki michuano hiyo, hivyo Medeama kukosa fedha zitakazowezesha safari nzima ya kwenda nchni Congo.
“Kwa sasa klabu haina fedha na inahitaji msaada mkubwa. Kwa maana hiyo tunafikiria kujitoa kwenye michuano hii endapo hatutapa msaada wowote,” ilieleza taarifa kutoka ndani ya klabu.
Kifungu cha 13 cha kanuni za CAF kinaeleza kuwa: “Endapo klabu itajitoa kabla ama wakati wa 8 bora, itapata adhabu ya kupigwa faini ya dola 1500 vile vile kukosa fedha za kijikimu zinazotolewa na CAF (engagement fees).”
“Mbali na adhabu hiyo, vile vile itakumbwa na adhabu ya kuzuiliwa ama kufungiwa kushiriki michuano yoyote ya CAF kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na kujitoa huko.”
Mwaka 2012, klabu nyingine ya Ghana Nania FC, ambayo inamilikiwa na legend wa taifa hilo Abedi Pele, ilijitoa kutokana sababu hizo hizo.
Nania, ambayo maskani yake ni Legon pia walipata fursa ya kushiriki michuano hiyo baada ya kushinda kombe la FA nchini humo, kama ambavyo Medeama ilivyopata nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment