Yanaweza yakafika maswali 1,000. Mijini na vijijini watu wanajiuliza
maswali na kama kila swali litachukuliwa kwa uzito, Roma Mkatoliki
atakuwa na kazi ya kujibu zaidi ya maswali 1,000 ya Watanzania.
Baadhi ya maswali ambayo hayajapata majibu kuhusu utekaji wa Roma ni
pamoja na alichohojiwa na watekaji, kwa nini watekaji waliwafunga
vitambaa vyeusi, kwa nini ofisa mmoja wa Serikali alitabiri kuwa
watarudi kabla ya Jumapili na utata kuhusu mazingira ya kufika polisi
baada ya kutekwa.
Siku moja baada ya kuachiwa na watekaji, Roma hakueleza alichohojiwa na
watekaji. “Watekaji walikuwa wakituhoji na kutupiga,” alisema Roma
aliyekuwa amefuatana na wasanii aliotekwa nao, Moni, Bin Laden na Imma.
Mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii, Godlisten Malisa ameandika
katika mtandao wake wa facebook akihoji maswali kadhaa kuhusu utekaji wa
Roma.
Miongoni mwake anahoji, ni kwa nini msanii huyo alijikuta yupo Ununio,
lakini akaenda kuripoti Kituo cha Polisi Kati (kikuu) na baadaye
Oysterbay huku akiwa tayari amekwenda nyumbani kwake kubadilisha nguo
ambazo ni ushahidi badala ya kwenda polisi moja kwa moja.
Swali hilo ambalo majibu yake hayajapatikana linapewa nguvu na idadi ya
vituo vya polisi vilivyopo kati ya Ununio na Posta, ambayo Roma
alivipita bila kujisalimisha na kutoa taarifa kuwa alikuwa ametekwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment