Sakata la utekaji limeendelea kung’ang’ania bungeni baada ya mbunge wa
Ukonga (Chadema), Mwita Waitara kutaja wabunge watano akidai kuwa wamo
kwenye orodha ya watu wanaotakiwa na Idara ya Usalama wa Taifa.
Amesema hayo siku moja baada ya mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein
Bashe kukiambia chombo hicho kuwa alitekwa na maofisa wa idara hiyo
wakati akitoa taarifa baada ya mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
kutakiwa atoe uthibitisho kuwa Usalama wa Taifa wanahusika na utekaji
watu unaoendela nchini.
Akizungumza wakati wa kuomba mwongozo bungeni jana, Waitara alisema kuna
timu mbili za watu watatu zimeundwa na Usalama wa Taifa kwa ajili ya
kuteka watu.
“Jana (juzi) nikiwa hapo nje nilipokea message (ujumbe) kuhusu wabunge
ambao ni target (walengwa). Mtoa taarifa anasema zimeundwa timu mbili za
watu watatu za Usalama wa Taifa,” alisema.
Alitaja wabunge ambao wanatafutwa kuwa ni Nape Nnauye (Mtama-CCM),
Hussein Bashe (Nzega Mjini-CCM), Godbless Lema (Arusha Mjini-Chadema),
Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini-Chadema) na yeye mwenyewe.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment