Kama kuna watu walifikiri Rais John Magufuli hajui fasihi, basi wamejidanganya kwani jana alionekana kujibu kiaina wimbo wa kundi la wanamuziki wa rap la Wagosi wa Kaya unaoitwa ‘Dereva’.
Rais Magufuli alijifananisha na dereva wa lori ambaye “hawezi kusikiliza nyimbo za abiria” unaoitwa “Dereva”.
Alitoa kauli hiyo wakati akizindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli ya
kisasa kati ya Dar es Salaam na Morogoro, itakayotumiwa na treni ya
umeme katika hafla iliyofanyika Pugu jijini Dar es Salaam.
Wakati Wagosi wa Kaya wanamfananisha kiongozi wa sasa na dereva wa basi
asiyesikiliza abiria wake, Rais Magufuli alijifananisha na dereva wa
lori aliyechukua abiria wa aina tofauti.
Katika wimbo huo, Wagosi wa Kaya wameelezea viongozi wa Serikali katika
awamu zote nne ambao wamekuwa wakisikiliza abiria wao wanapokuwa na
shida, lakini wanasema wa awamu ya tano hasikilizi abiria hata
wanapotaka kushuka kujisaidia.
“Unapopakia abiria kwenye lori, huhitaji kuwauliza watasimama sehemu
gani wakati lori linaondoka. Wapo watakaotazama nyuma, wapo
watakaotazama ubavuni, wapo watakaotazama ubavu mwingine, wapo
watakaotazama kule lori unakolipeleka ili lifike salama. Lakini wapo
wengine, kama utakuwa umepania wasukuma, watakuwa wanaimba,” alisema
Magufuli.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment