Ndugu
waandishi wa habari, kwa heshima kubwa ya kutambua nafasi yenu muhimu
kwenye jamii, nimewaita hapa ili tushirikiane kuujuza umma kwamba tupo
kwenye wakati mzuri wa haki kuonekana ikitendeka dhidi ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam ambae kwa vielelzo vyote anatambulika kama Daudi Albert
Bashite lakini wengi wanamfahamu kama Paul Makonda.
Ndugu waandishi wa habari, huu ni mwanzo, na kwa hakika ni mwanzo mwema wenye kuashiria kuwa mwisho wa Daudi Bashite umewadia.
Ndugu
waandishi wa habari, mtakumbuka kuwa 22 Machi 2017 mwaka huu,
niliwasilisha mashitaka yangu dhidi ya Daudi Bashite kwa Tume ya Maadili
ya Viongozi wa Umma, kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kukiuka
maadili ya utumishi wa umma na kukosa sifa yakuwa kiongozi si tu DSM
bali Tanzania kwa ujumla.
Mashtaka yangu tume yalikuwa ni yafuatayo;
1.
Kugushi vyeti vya kitaaluma kuliko fannywa na RC makonda huku akijua
fika kuwa vyeti anavyotumia vya taaluma si vyake wala si muhusika hivyo
kujiita PAUL CHRISTIAN MAKONDA huku akijua fika kuwa yeye ni DAUDI
ALBERT BASHITE, amekiuka sheria za nji nakutenda jinai.
2.
Kula kiapo cha utii na uaminifu mbele ya Mheshimiwa Rais kwa uhusika wa
kugushi ni kosa kubwa sana kisheria,huku akijua fika kuwa Rais alipaswa
amuapishe yeye kama DAUDI ALBERT BASHITE na siyo PAUL CHRISTIAN
MAKONDA.
3.Kujipatia
Mali kama magari na vinginevyo kinyume na maadili ya viongozi wa umma,
ambapo zawadi zote unazopokea unapaswa kutangaza hadharani, ikiwemo
kupata mali hizo kwa wahusika ambao amekuwa akiwatangaza hadharani na
kuwatuhumu kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.
4.Kukiuka
Misingi ya utawala bora haki za binadamu na utawala wa sheria kwa
kutuhumu watu ovyo hadharani kuwa walijihusisha na biashara ya madawa ya
kulevya kabla ya kukutwa na hatia na kisha wengine kuachiwa huru baada
ya kubainika hawakutenda makosa hayo; kinyume kabisa na sheria ambapo
mtu anatakiwa kutangazwa hadharani anapokutwa ametenda makosa.
5.
Shitaka la mwisho lilikuwa ni la Uvamizi wa kituo cha kirusha matangazo
ya redio na runinga cha Clouds media, ambapo akijua kuwa maadili ya
viongozi wa umma, hayaruhusu kiongozi kushurutisha au kulazimisha jambo
lolote kwakutumia madaraka yake kama kiongozi, ambapo mtuhumiwa alitenda
kosa la kutaka kutumia nguvu kurusha kipindi cha kumkashifu Kiongozi wa
dini wa Maknisa ya Ufufuo na Uzima almaarufu kamam Askofu Josephat
Gwajima.
Ndugu
waandishi wa habari, jana Aprili 12, nilipokea barua kutoka kwa
Kamishna wa Tume, Jaji Harold R Nsekela akinijulisha kuwa Tume ya
maadili ya viongozi wa Umma imekubali Mashtaka yangu dhidi ya mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam, na kunitaarifu kuwa wameanza kuyafanyia kazi
mashitaka yote.
Ndugu
waandishi wa habari, taarifa hiyo ya Kamishna wa Tume ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, imetoa mwanga mkubwa kwamba HAKI ambayo wengi wamekuwa
wakiiomba, sasa Mwanga umeanza kuonekana.
Hivyo
niwaombe wapenda haki wote popote walipo tushirikiane kwa hili ambalo
mkuu wa mkoa amekuwa ni kero jijini Dar es salaam, Tupeane ushirikiano
wa kuniongezea vielelezo vingine zaidi ya vile nilivyowasilisha Tume
yaani vyeti na nakala zingine za mali kama nimesahau jambo lolote.
Mimi
mlalamikaji na mashahidi wangu muhimu tupo tayari, mbali na matukio ya
utekwaji na upoteaji wa watu lakini tumeendelea kutaka kuona mwisho wa
kero hii jijini Dar es salaam, hivyo wakati wowote shauri litakapo anza
kusikilizwa kwenye baraza la maadili ya viongozi wa umma, tutakuwa
mstari wa mbele kutaka haki itendeke.
Wenu
Katika upiganiaji haki
BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment