Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>SERENGETI BOYS YAWACHAPA WACONGO 3-2, MASHABIKI WAKIINGIA BUREE TAIFA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Timu
ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka Serengeti Boys imepata
ushindi wa mabai 3-2 dhidi ya Congo Brazzaville katika hatua ya tatu
kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana itakayofanyika mwakani.
Mchezo
huo ambao ulifanyika kwenye Uwanja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam ulishuhudiwa na maelfu ya mashabiki ambao waliingia bure uwanjani
hapo kutokana na agizo la Waziri Nape Nnauye, aliyetaka iwe hivyo ili
kuwoangezea nguvu Serengeti Boys.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha
kwanza zinakamilika Serengeti ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, yakiwa
yamewekwa wavuni na Yohana Mkomola katika dakika ya 39 na 42.
Baada ya kufunga bao la pili alishangilia kwa kuvua jezi yake jambo ambalo lilisababisha apewe kadi ya njano.
Dakika
ya 72, Congo walipata penalti baada ya mchezaji wao mmoja kufanyiwa
faulo ndani ya eneo la 18, wakapiga na kufunga, dakika ya 82, Serengeti
walipata bao la tatu kupitia kwa Issa Makamba na kuamsha shangwe.
wakati
Watanzania wakiamini timu yao imeshinda mabao 3-1, Wacongo hao walipata
bao la pili katika dakika ya 90 baada ya mabeki wa Serengeti kujisahau.
Timu
hizo zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2 ambapo mshindi wa hapo atasonga
mbele kwa kufuzu moja kwa moja katika michuano hiyo ya vijana.
Related Posts:
Mashabiki 400 wa Juventus Waanguka kwa Presha Turin Baada ya Timu Yao kuchakazwa Goli 4-1 na Madrid Jana.
Zaidi ya Mashabiki 400 wa Juventus wameripotiwa kuzirai baada ya timu
yao kupokea kipigo cha aibu cha mabao 4-1 kutoka kwa Real Madrid jana
Jumamosi.
Mashabiki mbalimbali walikusanyika maeneo mbalimbali kufuatilia mec… Read More
Samatta Apiga Bao, KRC Genk ikishinda 3 - 0.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana
amefunga bao la tatu timu yake, KRC Genk ikishinda 3-0 ugenini dhidi ya
Sint-Truiden Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Ubelgiji kwenye mchezo
wa … Read More
Yanga Wamemfanya nini Hamis Tambwe...Mwenye Afunguka Haya Kwa Uchungu Akiwa Kwao Burundi.
STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe, huenda msimu ujao asionekane katika
kikosi cha timu hiyo kutokana na kutojua hatima yake ndani ya klabu
hiyo mpaka sasa.
Tambwe ambaye ameongoza Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara m… Read More
Sakata la Manula Kusaini Simba..Azam Watoa Tamko Hili.
Afisa Habari wa klabu ya Azam, Jaffar Iddi amefunguka na kukanusha
taarifa zinazoendelea mitaani kuwa kipa namna moja wa Azam FC, Aishi
Manula amesaini mkataba na klabu ya Simba na kudai kuwa mchezaji huyo
bado atabaki … Read More
MSUVA AFUNGUKA HAYA JUU YA TIMU TATU ZA KIMATAIFA ZINAZOMUHITAJI.
Timu tatu kutoka katika nchi tatu, sasa zinataka kumsajili kiungo wa pembeni wa Yanga, Simon Msuva.
Timu hizo zinatokea katika nchi za Morocco, Misri na Afrika Kusini na Msuva amethibitisha hilo.
Akizungumza na M… Read More
0 comments:
Post a Comment