Kikosi
cha Kilimanjaro Queens kimetinga katika fainali ya Kombe la kwanza la
Chalenji kwa wanawake baada ya kuwatwanga wenyeji wa michuano ya hiyo
Uganda kwa mabao 4-1.
Uganda
ambayo kikosi chao cha wanaume wakiwemo wachezaji kama Emmanuel Okwi
kimefuzu kucheza Afcon, dada zao walionekana kuushindwa kabisa mziki wa Kilimanjaro Queens.
Ushindi
huo sasa unaikutanisha Kilimanjaro Queens katika mechi ya fainali dhidi
ya Kenya ambao wamefanikiwa kutinga baada ya kuwang’oa Ethiopia kwa
kuwachapa mabao 3-2.
Katika
mechi hiyo ya Kilimanjaro Queens mjini Jinja, wenyeji walionekana
wamezidiwa kwa kiasi kikubwa na Queens walipata bao la mapema katika
dakika ya 6 kupitia Donosia Daniel.
Kama
vile wenyeji wangeweza kuamsha matumaini lakini walitandikwa bao la
pili mfungaji akiwa Mwanahmisi Omari katika dakika ya 17 na Stumai
Abdallah akapigilia msumari wa tatu dakika ya 31.
Kilimanjaro
Queens walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao 3-0 na Asha
Rashid ‘Mwalala’ alipigilia msumari wa mwisho huku wenyeji wakipata bao
moja la ‘kuchafua gazeti’.
0 comments:
Post a Comment