Mkazi
wa jijini Dar es Salaam, Leonard Kyaruzi amepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka mawili ikiwemo
kuchepusha na kusambaza taarifa za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli
kwa njia ya mtandao whattsapp.
Mshtakiwa
huyo amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Magreth
Bankika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Wakili
wa Serikali Simon Wankyo alidai kuwa June 2, mwaka huu katika jengo la
Tanzanite Tower lililopo barabara ya Sam Nujoma, mshtakiwa alichapisha
taarifa ya kumdhalilisha Rais Magufuli.
Wankyo
alinukuu taarifa hiyo kwamba”Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri?
Hashauriki? Au ni zuzu?Bwege sana huyu jamaa, He Doesn’t consider the
law in place before opening his mouth! Au nay eye anaumwa ugonjwa wa
Mnyika?” .
Katika
shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza,
mshtakiwa alisambaza taarifa ya kumdhalilisha Rais Magufuli, kupitia
mtandao wa Whattsapp kwamba “Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri?
Hashauriki? Au ni zuzu?Bwege sana huyu jamaa, He Doesn’t consider the
law in place before opening his mouth! Au nay eye anaumwa ugonjwa wa
Mnyika?”.
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.
Hakimu
Bankika amesema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na mdhamini
mmoja anayetambulika, atakayesaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni moja.
Mshtakiwa alitimiza masharti hayo. Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hakimu amesema kesi hiyo itatajwa Julai 18, mwaka huu na mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment