Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kwamba
serikali itawalinda wastaafu nchini wakiongozwa na viongozi wakuu wa
umma ili wawe na heshma yao ndani ya jamii.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya
kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa tume ya
taifa ya uchaguzi.
''Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete wewe pumzika kwa raha zako , upo salama
watachonga wee lakini mimi kama Rais wa awamu ya tano nipo tayari
kuwalinda watumishi wote wastaafu kwa kuthamini mchango wao ndani ya
taifa hili''
Aidha
Rais Magufuli amesisitiza kwamba uchaguzi nchini umemalizika hivyo
vyama vyote vya siasa viongeze nguvu baada ya miaka mitano ili apimwe na
wananchi waliomchagua kama ametekeleza ahadi zake.
''Niwaombe
wanasiasa wenzangu uchaguzi umekwisha, kama ni wabunge jielekezeni
bungeni, kama ni madiwani jielekezeni kwenye maeneo yenu, sitakubali mtu
yeyote anikwamishe katika kutimiza ahadi zangu kwa wananchi'' Amesema Rais Magufuli.
Kuhusu
tume ya uchaguzi kukabiliwa na changamoto lukuki Rais Dkt. Magufuli
amesema fedha za tume hiyo ilizobakiza kiasi cha shilingi bilioni 12 na
kuzirudisha serikalini, serikali imeruhusu fedha hizo zitumike kujenga
jengo la tume hiyo ili kuondokana na gharama za kupangisha jengo
wanalotumia kwa sasa.
Aidha
akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva amesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
ulikuwa huru na wa haki na hata waangalizi wa nje wengi wamepongeza
uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment