Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Utafiti: Mbwa kuwa tiba ya Malaria.Fahamu zaidi hapa.
Kemikali zinazopatikana katika watu walioambukizwa ugonjwa wa Malaria zinaweza kutolewa na mbwa ,utafiti umebaini.
Wanasayansi
katika shule ya London kuhusu usafi na dawa kutoka eneo la tropiki
wamepewa takriban dola 100,00 na wakfu wa Bill and Melinda Gates ili
kufanya utafiti zaidi.
Watashirikisha usaidizi kutoka watoto 400
wa Gambia,ikiwemo baadhi ambao wanajulikana kuwa na ugonjwa wa Malaria
ambao watahitajika kuvaa soksi za nailoni kwa saa 24.
Mbwa hao watafunzwa kubaini kati ya violezo vya malaria na vile ambavyo sivyo.
Mmoja ya watafiti James Logan aliambia BBC Newsday kwamba hatua hiyo itasaidia kuzuia kusambaa kwa Malaria.
Chanzo
BBC SWAHILI.
0 comments:
Post a Comment