Tuesday, 2 August 2016

#YALIYOJIRI>>>Mwanafunzi UDOM auawa kwa kupigwa na wenzake Wakati Wakitoka Baa.Fahamu zaidi hapa.

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Fredrick Joseph (25), ameuawa kwa kushambuliwa kwa kipigo na watu wanaosadikiwa kuwa ni wanafunzi wenzake wakati akitoka klabu ya pombe (Bar).

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akiwa anagalagala njiani.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, amesema mwanafunzi huyo ambaye ametokea Musoma mkoani Mara alishambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wasiofahamika.

Amebainisha mwanafunzi huyo alikutwa majira ya saa 10 alfajiri katika eneo hilo la chuo hicho huku akisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu huyo alikuwa na ugomvi na watu hao katika klabu ya pombe ya Canival Pub iliyopo chuoni hapo.

“Alipoondoka kurudi bwenini akiwa njiani alishambuliwa na watu hao wasiofahamika na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, kipigo kilichosababisha kifo chake wakati alipokimbizwa kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma,” alisema Mambosasa

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo kwa uchunguzi zaidi na hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Alipoulizwa kuwa taarifa za mwanafunzi huyo kushambuliwa na wenzake, Mambosasa alisema kwasababu inadaiwa haifahamiki upelelezi bado unaendelea.

“Kwa sababu mwenye bar si yupo, kama kuna ugomvi ambao ulikuwa unaendelea tutajua tu, nimemuelekeza OCD kufuatilia ni nani waliokuwa wanakunywa kwenye hiyo bar chuoni, ni lazima tu watakuwa wanachuo ili tuwabaini,”

Kamanda huyo amesema ameelekeza uchunguzi wa kina ufanyike kama kulikuwa na ugomvi ndio hao hao walienda kumtegea njiani.

Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutaja jina lake kwa madai kuwa  siyo msemaji wa polisi kimesema kuwa marehemu Joseph alikuwa anakunywa pombe pamoja na marafiki zake lakini baada ya kulewa walianza ugomvi ambao hata hivyo waliamuliwa.

“Baada ya kuamuliwa ule ugomvi wa awali ndipo wenzake walipokwenda kumsubiria kwa mbele kwenye kichaka ambapo walimvamia na kumshambulia na kumwacha karibu ya kufa,” kilisema chanzo hicho.

Kiliongeza kuwa, baada ya kumwacha hapo na kutoweka ndipo walinzi wa chuo hicho waliokuwa doria walimuokota na kumfikisha kwenye kituo kidogo cha polisi kilichopo Chimwaga ambapo alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipofariki wakati akipatiwa matibabu.

Chanzo hicho kimesema hakuna mtuhumiwa hata mmoja anayeshikiliwa na polisi kwa kuwa wote waliomshambulia walitoroka na hawajulikani walipo.

#MICHEZO>>>>KAZI IPO, MANJI AWAITA WANACHAMA WA YANGA JUMAMOSI, WANAKUTANA DIAMOND JUBILEE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Wanachama wa Yanga, watakutana Jumamosi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Ukumbi huo, Juzi Jumapili wanachama wa Simba walipitisha uamuzi wa klabu yao kuacha mchakato wa kuwa kampuni.

Wanachama hao wa Yanga, watakutana na kupata nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti wao Yusuf Manji.

Baada ya mkutano huo, wanachama hao wa Yanga watapata nafasi ya kuhudhuria mechi ya kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar.

#MICHEZO>>>EXCLUSIVE: MO DEWJI AANZA KAZI, AMWAGA SH MILIONI MIA ZA USAJILI SIMBA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mkurugenzi Mtendaji na rais wa makapumni ya Mohammed Enterprises Ltd (MeTL Group) Mohammed Dewji ‘MO’ ametoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa klabu ya Simba kwa ajili ya kusaidia zoezi la usajili kama alivyoahidi siku chache zilizopita.

Bilionea huyo ambaye anania ya kuwekeza bilioni 20 alisema, yuko tayari kusaidia zoezi la usajili endepo klabu hiyo ingeridhia kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wanachama wa kadi hadi kuwa kampuni ambayo itaendesha kwa mfumo wa kibiashara.

Julai 31 klabu ya Simba iliridhia kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji japo haikujulikana mara moja kwamba wameamua kuingia katika mfumo upi.

MO amesema ametimiza ahadi aliyoitoa baada ya wanachama wa klabu ya Simba kukubali kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji: “Niliahidi kusaidia kwenye zoezi la usajili kwa ajili ya klabu yetu ya Simba SC, ninafuraka kubwa sana kumkaribisha rais wa klabu (Simba). Mimi kama mwanachama ningependa kuchangia kwenye hilo zoezi.”

Rais wa Simba Evans Aveva ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Patrick Kahemle, amemshukuru MO kwa kuamua kusaidia zoezi la usajili ambalo bado klabu hiyo inakabiliwa na upungufu wa mkwanja kwa ajili ya usajili licha ya Mbunge huyo wa zamani wa Singida kutoa shilingi milioni 100 kupiga tafu usajili.

“Kama alivyoahidi kwenye mkutano na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya mkutano wetu mkuu, aliwaambia wana Simba kupitia waandishi wa habari kwamba endapo mkutano wa August 31 utaridhia mabadiliko ya uendeshaji wa klabu yetu, basi yeye kama mwanachama wa Simba atachangia zoezi la usajili.”

“Usajili wetu wa Simba unaendelea haujafika mwisho tumebakiza takribani siku tano ili kufunga zoezi hilo, ni zoezi ambalo lina gharama kubwa. Tuliwasiliana na mwanachama wetu tukamwambia kiasi kilichobaki ambacho ni shilingi milioni 420 ili kumalizia zoezi hili la usajili. Kwahiyo alichotoa mwanachama wetu kitatusaidia kwa kiasi kibwa kutoka hapa tulipo.”

“Kuna mchezaji mmoja kutoka Ivory Coasta ambaye dau lake la usajili ni zaidi ya milioni 100, kwahiyo kwa kupata pesa hizi naamini tutaweza kumsajili mchezji huyo.”

“Wanachama wengine waige mfano wa Mohammed Dewji na kuchangia katika zoezi hili wasijewakasema MO ametoa kiasi cha pesa kwahiyo ndiyo tumemaliza zoezi la usajili.”

​Picha za utupu za kisagaji za mke wa Donald Trump zasambaa.Fahamu zaidi hapa.

Gazeti la New Daily News limechapisha picha za utupu za mke wa mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump, Melania.

Limeandika kuwa miaka mitatu kabla ya kukutana na mume wake, Donald Trump, Melania alipiga picha za utupu na mrembo mwingine kwaajili ya jarida la Ufaransa.

Picha hizo za kisagaji zilipigwa huko Manhattan mwaka 1995, kipindi hicho akiitwa Melania Knauss, mwenye umri wa miaka 25 na alikuwa akitumia jina la “Melania K.”


Baadhi ya picha hizo ziliwekwa kwenye jarida la Max la Ufaransa, zaidi ya miaka 20 iliyopita. Baadhi yake hazijawahi kuchapishwa hadi sasa.

Picha kali zaidi inamuonesha Melania akiwa amelala kitandani na mlimbwende aitwaye Emma Eriksson, akiwa mtupu pia nyumba yake.

Alipoulizwa kuhusu picha hizo, Donald Trump alisema: Melania was one of the most successful models, and she did many photo shoots, including for covers and major magazines. This was a picture taken for a European magazine prior to my knowing Melania. In Europe, pictures like this are very fashionable and common.”

Mrembo huyo raia wa Slovenia, mwenye miaka 46 sasa, alikutana na Trump kwenye hafla ya Fashion Week mwaka 1998. walioana January 2005 na wana mtoto mmoja, Baron, 10.

Miss World Kenya Apokonywa taji lake Kama Miss Sitti Mtemvu.Fahamu zaidi hapa.

Aliyekuwa mshindi wa tuzo la Miss World Kenya 2016 , Roshanara Ebrahim, amepokonywa taji lake baada ya kukumbwa na sakata .
Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya,Roshanara mwenye umri wa miaka 23, alishinda taji la mwaka uliopita na alikuwa anatarajiwa kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya Miss World, mwishoni mwa mwaka huu.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, wasimamizi wa Miss World Kenya, kampuni ya bidhaa za urembo, Ashleys imeandika,

'Kuanzia sasa, Roshanara hatoiwakilisha Kenya nchini na hata kimataifa kama Miss World. Tumefahamishwa kuhusu sakata kubwa inayomkumba Roshanara Ebrahim, ambayo inakiuka sheria na masharti ya Miss World Kenya. Tunatekeleza sheria zetu na tunatarajia wanamitindo wetu kusimamia maisha yao ya kibinafsi.

Kulingana na gazeti hilo , Roshanara ameandika kukubaliana na uamuzi huo na kuwasihi warembo wenye umri mdogo kuhakikisha maisha yao ya kibinafsi, hayaathiri jukumu lao la Miss World.

''Nakaribisha uamuzi wa ofisi ya Miss World Kenya kunipokonya taji la Miss World Kenya kwa masikitiko makubwa, namtakia atakayechukua nafasi yangu kila la heri.

Kabla ya uamuzi wa ofisi ya Miss World Kenya, Roshanara alilazimika kujitetea dhidi ya madai yaliomhusisha kuwa na uhusiano na mwanasiasa mashuhuri.

Tayari ofisi ya Miss World Kenya, imeahidi kumtangaza mwanamitindo atakayejaza pengo lililoachwa na Roshanara Ebrahim siku chache zijaazo.

Roshanara anayesomea uwakili, anatarajiwa kuendelea na shughuli zake za kuwasaidia watoto walio na mpasuko wa mdomo, yaani 'cleft.

#MICHEZO>>>>JOHN OBI MIKEL ABADILI JINA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

John Obi Mikel ameamua kubalisha jina lake. Jina lake halisi alikuwa anaitwa Michael John Obi, lakini Shirikisho la Soka nchini Nigeria kwa bahati mbaya walikosea herufi wakati wakimwandikisha jina lake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 cha nchi hiyo mwaka 2003.

Waliandika Mikel badala ya Michael, hivyo Obi alimua kutumia jina hilo mpaka alijiunga na Chelsea mwaka 2006.

Taarifa zilizoenea leo zinaeleza kwamba, sasa Mikel ambaye hapo awali alikuwa akiitwa John Michael Nchekwube Obinna, amebadili jina rasmi na atakuwa akiitwa ‘Michael John Obi’.

#YALIYOJIRI>>>>Ugonjwa wa Sumukuvu Wahatarisha Maisha Nchini..Umeua Watu 14 Mpaka sasa Huku 54 Wakiwa Wanaugua Ugonjwa Huo.Fahamu zaidi hapa.

Watu 14 wamefariki dunia katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara kutokana na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama ‘Aflatoxicosis’ unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka iliyoharibika.

Hayo yamesema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa ya milipuko na magonjwa mengine leo jijini Dar es Salaam.

“Ugonjwa uliosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) uliripotiwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni, 2016 katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na baadaye mkoani Manyara katika wilaya ya Kiteteo” alisema Waziri Ummy na kuongeza kuwa:

“Wagonjwa walikuwa na dalili za kuumwa tumbo, kuharisha, kutapika, tumbo kuvimba na kuwa manjano sehemu mbalimbali za mwili ambayo inaashiria kuathirika kwa ini”

Alisema mbali na vifo hivyo, hadi kufikia Julai 31 mwaka huu wagonjwa 54 waliripotiwa kuugua ugonjwa hu huku wagonjwa wanne wakilazwa kutokana na kuugua.

“Hadi kufikia tarehe 31, July 2016 kulikuwa na wagonjwa 54 na watu 14 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.Aidha katika wiki iliyopita aliripotiwa mgonjwa mmoja mpya kutoka wilaya ya Kondoa” alisema Waziri Ummy na kufafanua kuwa:

“Jumla ya wagonjwa waliolazwa wodini ni wanne kati yao mmoja yupo Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na watatu wapo katika Hospitali ya Kondoa”

Waziri Ummy alitaja wilaya zilizoripoti wagonjwa hao na idadi ya wagonjwa kuwa ni wilaya ya Chemba wagonjwa 38, Kondoa wagonjwa tisa , Kiteto wagonjwa watatu, Chamwino wagonjwa wawili na Dodoma Manispaa  mgonjwa mmoja.

“Vijiji vilivyoathirika zaidi na ugonjwa huo ni kutoka wilaya ya Chemba ambavyo ni Kinkima, Itolwa, Mwailanje na katika wilaya ya Kondoa ni kijijini cha Ubembeni” alisema Waziri Ummy.

Hivyo, aliitoa hofu familia iliyopoteza watu wanne katika kijiji cha Mwaikuzabe na kusema vifo hivyo havihusiani na uchawi au kuwekewa sumu bali ni chakula cha siku ile kilithibitika kwamba kilikuwa na sumukuvu.

Kufuatia athari hizo Serikali itafanya uchunguzi wa kina katika wilaya kumi  za Chemba, Kondoa, Chamwino na Kiteto na wilaya nyingine za mikoa ya Sindida, Dodoma na Manyara zinazopakana na wilaya hizo.

Alisema uchunguzi huo unalenga kubaini hali ya usalama wa vyakula vinavyotumiwa na jamii ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na kuwaathiri wananchi wengi zaidi wanaoishi katika wilaya hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taifa wa Afya wa Wizara hiyo Dkt. Fausta Mosha alisema wizara imeandaa  vipepereshi vyenye maelekezo yanayotoa elimu juu ya kijikinga kwa kuandaa chakula kuanzia hatua ya uvunaji shambani hadi wakati wa kula.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowelle alisema njia bora ya kupambana na ugonjwa huo ni kuukinga kwa kuhakikisha sumu kuvu haizalishwi kutoka kwenye nafaka.

Akifafanua kuhusu udhibiti, Waziri Ummy alisema wanashirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kutoa elimu kwa wananchi juu ya njia sahihi ya uhifadhi na uandaaji wa chakula utakaosaidia kupunguza kiasi cha sumukuvu kwa nafaka ambazo hazijaharibika sana.

“Njia hizi ni pamoja na kuhifadhi nafaka zilizokauka vizuri na kuchambua nafaka zilizoharibika (zilizooza, kuvunjika, zilizobadilika rangi), kukoboa mahindi kabla ya kusaga au kuacha kutumia nafaka zitakazoonekana kuharibika rangi” alisema.

Waziri Ummy alisisitiza Serikali kuendelea kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kupunguza uchafuzi wa sumukuvu katika vyakula, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa kupima sumukuvu katika damu na choo kidogo miongoni mwa taasisi za ndani ya nchi.

Inaelezwa kuwa ugojwa wa‘Aflatoxicosis’unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka uliwahi kutokea nchini Kenya mwaka 2004 na kusababisha vifo vya zaida ya watu 100 huku wengine 200 waliathirika.

#Breaking News>>>Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale akamatwa na Polisi leo asubuhi.Fahamu zaidi hapa.

Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.


Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.



Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Monday, 1 August 2016

Nay wa Mitego Aanza Kuuza Mkaa Baada ya Kufungiwa Muziki...Tazama Video Hapa.

Mchekeshaji Stan Bakora ameendelea na utani wake ambapo Ijumaa hii ameachia video ya kumdhihaki rafiki yake Nay wa Mitego baada ya kufungiwa na BASATA.
TAZAMA VIDEO:

#BURUDANI>>>Huyu Ndio Mwanamke Anayemuumiza Kichwa Zari Hassan wa Diamond Kwa Sasa...Check Video.

Hamisa Mobeto Kwa sasa amekuwa Kirusi Kwenye Penzi la Mwanamuziki Diamond na Zari Hassan Hasa tetesi zinazosema Kuwa anatoka kimapenzi kwa siri na Diamond....
Leo Ametupostia hii Video kwenye page yake ya Instagram
Angalia Video Hapa chini:

#BURUDANI>>>Baraka Da Price na Najma Watupia Video Wakifanya Yao Kitandani..Video Hii Hapa.

Penzi kati ya Baraka da Prince linazidi kuwa Gumzo mitandaoni Baada ya Jana Baraka Kuposti Video Akifanya yake Kwa Najma Huku Naj Akiwa katika Usingizi mzito
Nimekuwekea Video Hapa Chini:

#MICHEZO>>>KAULI YA WAZIRI NAPE KUHUSIANA NA MABADILIKO YA SIMBA HII HAPA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameweka wazi anachoamini ni bora katika mabadiliko yaliyofanywa na wanachama wa kalabu ya Simba.

Wanachama wa klabu ya Simba wamepitisha kwa pamoja kuwa klabu yao kuingia kwenye mfumo wa kampuni na hisa kuanza kuuzwa hasa ikiwa ni siku chaache baada ya mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji ‘Mo’ kutangaza hadharani nia yake ya kutaka kununua hisa asilimia 51 kwa Sh bilioni 20.

Nape ameandika kupitia mtandao wa Twitter akieleza uamuzi huo wa wanachama wa Simba kama utasimamiwa kwa uhakika utakuwa na tija.

Huku akisisitiza mfumo mpya kama utasimiwa utakuwa na tija kwa mashabiki wa Simba kununua hisa, ikiwa ni maana maendeleo ya Simba yanaweza kuchagishwa na Wanasimba wenyewe.

Kauli hiyo ya Nape, inaonyesha wazi inaunga mkono uamuzi wa wanachama hao wa Simba walioupitisha katika mkutano wa mwaka wa wanachama Jumapili iliyopita.


Lakini anaweka msisitizo katika usimamizi bora kwenye katika mfumo huo ili kuufanya kuwa na tisa.

#YALIYOJIRI>>>Mrema akutana na Madereva Bodaboda wa Kinondoni.Awataka wampe majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa.Faham zaidi hapa.

Mwenyekiti wa Parole Augustino Mrema amewataka madereva bodaboda kote nchini kujiepusha na tabia za kushiriki maandamano ya kisiasa yanayoandiwa na baadhi ya wanasiasa kwa lengo la kuvunja sheria za nchi.

Pia amewaagiza waendesha bodoboda Kinondoni wampe majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa ili ayakabidhi kwa rais Magufuli.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
Baadhi ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani) alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo.

#MICHEZO>>>>Bale Akodi kisiwa cha karibu billioni 2 kumchumbia demu wake.Fahamu zaidi hapa.

Gareth Bale alikodi kisiwa cha Tagomago, kilichopo karibu na Ibiza ili kufanya shughuli ya kumposa mchumba wake Emma Rhys-Jones.
Kwa mujibu wa ripoti mchezaji huyo wa Real Madrid alikikodi kisiwa hicho Tagomago, ambapo alisherehekea miaka yake 27 ya kuzaliwa na alitumikia nafasi hiyo pia kumuomba amuoe mchumba wake Emma Rhys-Jones na mpenzi wake alimkubalia.
Gharama za kukodi kisiwa hicho ilikuwa 450,000 kwa wiki – ambazo ni zaidi ya Billioni 1.9 za kitanzania, Bale alilipa kiasi hicho na kufanyia shughuli hiyo. Kwa Bale hiyo ilikuwa fedha ndogo na hata hakutumia kutoka kwenye mshahara wake wa £15m kwa mwaka – zaidi ya billioni 45 za kibongo.
Muda mfupi kabla ya shughuli hiyo, Bale alitoka kulipwa kiasi cha €600,000 kutoka kwenye bonasi ya kufika nusu fainali ya Euro 2016.

#YALIYOJIRI>>>>Rais Magufuli Amaliza mgogoro wa makazi Magomeni Kota.Fahamu hapa.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemaliza mgogoro wa makazi wa Magomeni Kota uliodumu kwa kipindi kirefu.Hayo yamesbainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati akiongea na Kamati ya Mgogoro wa Makazi ya Magomeni Kota mbele ya waandishi wa habari.

“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefuta hati na mikataba yote inayohusiana na ardhi ya yaliyokuwa makazi ya Magomeni Kota, Dar es Salaam”,alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi Rais ameondoa umiliki wa eneo hilo toka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kumilikisha Serikali Kuu ambayo ndiyo itakayosimamia ujenzi wa nyumba 644 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.

“Tutajenga nyumba 644 na kuwauzia kwa bei ya jengo na siyo ya ardhi ili kuwapeni unafuu katika kununua,”alisema Lukuvi huku akishangiliwa na baadhi ya wakazi wa Magomeni.

Aidha, Lukuvi amesema kuwa anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ameagiza timu ya wataalamu wa Wizara kupima na kuchora michoro kwa ajili ya ujenzi.

Lukuvi amesema katika eneo hilo zitajengwa nyumba za heshima ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu ili kukidhi mahitaji ya kifamilia kwani watu hawa wamekaa kwa miaka takribani 50 hadi wameshapata wajukuu. Ameongeza kuwa kila mmiliki wa nyumba hiyo atapewa hati yake hata kama nyumba hiyo itakuwa kwenye ghorofa.

Lukuvi amesema kuwa Rais ameagiza maeneo kama ya Magomeni Kota katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara nayo yatakuwa katika mfumo huo wa Magomeni. Kwa mujibu wa Lukuvi wazee ambao wanakaa kwenye nyumba kama hizo sehemu nyingine wasiondolewe kwani hao walikuwa watumishi wa umma hivyo Rais amesema wasibughudhiwe.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mgogoro wa Makazi Magomeni Kota, George Abel ameshukur Mhe Rais Magufuli na Wazir Lukuvi kwa kutatua mgogoro huo ambao anadai umewasumbua sana.

Ameahidi kutoa ushirikiana kwa Serikali pindi suala la ujenzi litakapokuwa linaendelea ili kuhakikishaujenzi unaenda haraka.Naye Wakili ambaye alikuwa akiendesha kesi hiyo kabla ya Mhe. Rais kuingilia kati, Mhe. Twaha Tasilima ameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

“Rais Dkt Magufuli na Mhe. Waziri Lukuvi ni watu wa vitendo na si maneno na kweli wanawajali wanyonge, nawashukuru sana,”alisema Tasilima.

Uamuzi wa kurudisha eneo hilo kwenye Serikali Kuu umetolewa na Rais Magufuli tarehe 10/7/ 2016.

SHAMSA FORD AACHIA PICHA HIZI JANA KWENYE BIRTHDAY YAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.


Download wimbo wa Ben-Pol & Stereo unaoitwa "SHILINGI".Hapa hapa.

DOWNLOAD HAPA CHINI.

STAA ZARI AKILA BATA HUKO SAUZI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Diamond Platnumz’s Babymama, Zarina Hassan ‘Zari’ shared her pic showing off her sweet beauty while  hanging out i South Africa where now she is, See another pic as she shared on her Instagram account;

PICHA MPYA ZA STAA WEMA SEPETU ALIZO ACHIA MTANDAONI.


#MICHEZO>>>SIMBA YAENDELEZA DOZI MOROGORO, YAICHAPA BURKINA FASO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Simba imeendeleza dozi katika mechi zake za kirafiki baada yakuichapa Burkina Faso ya Morogoro kwa mabao 5-0.

Katika mechi hiyo ya kirafiki, Ibrahim Ajib ameendelea kung’ara baada ya kufunga mabao mawili huku Moussa Ndusha raia wa DR Congo, Shiza Kichuya na Said Ndemla kila mmoja akitupia moja.

Hii ni mechi ya tatu ya Simba ya kirafiki na zote imeshinda ikianza na ile dhidi ya Polisi Moro iliyoshinda 6-0 kabla ya kuitwanga Moro Kids 2-0.

#YALIYOJIRI>>>>Wafanyabiashara Wawili Wauawa Gesti Dar es Salaam.Fahamu zaidi hapa.

Watu wawili wamekutwa wamefariki katika nyumba ya wageni ya Kings Rest House iliyopo Mtaa wa Bumila, Gongo la Mboto jijini Dar  huku miili yao ikiwa imeungua moto. 

Mmiliki wa gesti hiyo, Damian Mng’ong’o alisema alifuatwa kanisani jana saa 1.30 asubuhi na kuambiwa kuna chumba kimoja katika gesti yake kinafuka moshi na aliondoka kanisani kuelekea ilipo nyumba hiyo. 

Alisema alipofika aliona moshi bado unafuka huku nje kukiwa na umati mkubwa wa watu wakishangaa.

“Tulifanya uamuzi wa kufungua mlango lakini hatukuona mtu yeyote chumbani, ndipo mmoja wa wafanyakazi alipofungua mlango wa choo ndani ya chumba tukakuta maiti mbili zikiwa zimechomwa. "

Alisema mhudumu wa gesti alitueleza kuwa jana (juzi) saa tano asubuhi alikuja mwanamume mmoja akachukua chumba na baadaye jioni alikuja kijana mwingine wakawa wameingia wote katika chumba hicho. 

“Baada ya muda nilipiga simu polisi kuripoti tukio hilo nao waliwasili ndani ya muda mfupi wakafanya uchunguzi wao na kuhoji baadhi ya watu, baadaye wakawaleta madaktari kupima, kisha wakaondoka na maiti hizo mbili kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya hatua nyingine.” 

Mfanyakazi wa jikoni katika gesti hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema watu hao waliofariki ni wafanyabiashara wanaouza ng’ombe katika mnada wa Pugu na mara nyingi wakija Dar es Salaam hufikia hapo. 

“Wengi wanaofanya biashara ya ng’ombe wakija hufikia hapa, mpaka sasa sijajua kilichotokea kwa hawa waliokufa, lakini tukio hili limewashtua wenzao kwani baadhi walipoona tukio hili wameingiwa na hofu na kuondoka,” alisema. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema wanaendelea kuchunguza na taarifa za awali hazijathibitisha kama waliuawa hapo gesti au sehemu nyingine na kupelekwa hapo. 

“Kuna viashiria kuwa huenda waliuawa wakaletwa pale kwani wana alama ya kamba katika shingo kama vile kuna mtu aliwanyonga na katika matumbo yao kuna majeraha kama wamechomwa kitu chenye ncha kali,” alisema na kuongeza: 

“Mpaka sasa uchunguzi unaendelea na Jeshi la Polisi linafanya kazi yake na tunasubiri taarifa kutoka kwa wataalamu wa masuala ya uchunguzi na alama za vidole ambayo itaeleza kwa nini wao waungue lakini nguo zao zisiungue. Pia kitanda na vitu vingine visiungue na kwa nini watu waende kuzima moto, wakati watu wameshafariki,” alisema Hamduni. 

Hamduni alisema mmoja wa waliofariki alijiandikisha kama Lameck Ludovick, mfanyabiashara na mkazi wa Dar es Salaam.

#MICHEZO>>>HATIMAYE, UONGOZI SIMBA WAOMBA MCHANGO WA USAJILI KWA MO DEWJI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

BARUA KUTOKA UONGOZI WA SIMBA KWENDA KWA MO DEWJI.
Sasa inaonekana mambo yanaanza kwenda vizuri na muunganiko wa umoja kati ya uongozi wa klabu ya Simba na Bilionea, Mohammed Dewji ambaye ni shabiki na mwanachama wa Simba, unaanza kukolea.

Hii ni baada ya leo, uongozi wa Simba kumkaribisha kwenye kikao cha kamati ya utendaji lakini baadaye umeandika barua pia kuomba fedha kwa ajili ya usajili.


Ombi hilo ni sehemu ya kumkumbusha Mo kutokana na ahadi yake kuwa yuko tayari kuchangia usajili.

Tayari Mo ametangaza nia yake ya kununua hisa asilimia 50 za klabu ya Simba kwa kutoa Sh bilioni 20.

#MICHEZO>>>MBEYA CITY YATOA KICHAPO KWA RUVU SHOOTING HII LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Dakika 90 Za mchezo wa kirafiki Kati ya Ruvu shooting na City zimemalizika Kwa wenyeji kushinda 1-0, bao Hilo limefungwa Kwa njia ya penalti kwenye dakika ya 49.

#YALIYOJIRI>>>>MTI WENYE SURA YA DONALD TRUMP WAONEKANA UINGEREZA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

DUNIA ina maajabu mengi, wakati joto la uchaguzi nchini Marekani likiwa limepamba moto, mti wenye sura inayofanana na mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump umeonekana huko Glewstone, Hereford nchini Uingereza.

Mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia.Fahamu zaidi hapa.

GHENT, Ubeligiji
WATUMIAJI wa pombe sasa wataweza kupata auheni ya bei ya vinywaji hivyo, baada ya wanasayansi kugundua kifaa maalumu kitakachotumika kubadilisha mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia.

Kugunduliwa kwa kifaa hicho ni mkombozi kwa wamiliki wa viwanda vya pombe ambapo wataweza kupata malighafi ya kutengenezea bia kwa urais.

Kinatarajiwa kufungwa kwenye vyoo vya baa mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa mikojo hiyo ya walevi.

Kifaa hicho ambacho kitakuwa kikitumia umeme wa jua pia kitakuwa na uwezo wa kubadili mikojo hiyo kutumika kama maji ya kunywa.

Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubeligiji, walisema kifaa hicho kitaanza kutumika hususan maeneo ya mijini kwenye nchi zinazoendelea.

Licha ya kuwepo kwa mashine maalum yenye uwezo wa kutibu maji machafu ikiwemo mkojo kisha kutumika kwa matumizi mengine muhimu ya binaadamu, wataalamu hao wamesema kifaa hicho walichokigundua kinauwezo zaidi wa kuyatibu maji hayo bila kutumia nguvu ya umeme.

Dk. Sebastiaan Derese, alisema kifaa hicho kitakuwa kikitunza mikojo kwenye tangi maalum ambalo litatumika kutibu kisha kutumika kama malighafi ya kutengenezea bia.

Kwa mara ya kwanza kifaa hicho kilianza kutumika kwenye tamasha la muziki ililofanyika mjini humo ambapo jumla ya lita 1000 za mikojo, zilikusanywa kisha kutengenezewa bia.

Alibainisha kuwa, bia zilizotengenezwa kupitia mikojo hiyo imewavutia wanywaji wengi hususan kwenye matamasha mbalimbali.

#YALIYOJIRI>>>Wakili Kibatala: Mkurugenzi wa Bagamoyo Aliyetumbuliwa na Rais Magufuli ameponzwa na Kesi za Uchaguzi zilizoipa ushindi Chadema.Fahamu zaidi hapa.

Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema, Peter Kibatala amempa pole aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi kwa kuenguliwa kwenye nafasi hiyo, ikiwa ni siku moja baada ya kesi za uchaguzi alizotolea ushahidi wilayani Kilombero kuhukumiwa. 

Akiandika katika ukurasa wake wa Facebook jana, Kibatala alisema: “Tunasikitika nawe, na kukupa pole nyingi sana.” 

Katika ujumbe huo aliothibitisha baadaye kuuandika, Kibatala aliongeza: “Tunakushukuru sana kwa kutoa ushahidi wa ukweli na wa haki katika kesi za uchaguzi majimbo ya Kilombero na Mlimba yaliyotolewa hukumu jana (Julai 29).” 

Wakili hiyo aliongeza: “Wakati wa Uchaguzi Mkuu ulikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero na Msimamizi wa Uchaguzi katika Majimbo waliyoshinda Chadema.” 

Juzi, taarifa ya Ofisi ya Rais–Tamisemi iliyotolewa  na Katibu Mkuu, Mussa Iyombe bila kufafanua sababu za kuenguliwa kwake, ilieleza kwamba Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mbilinyi kwa sababu hakuridhishwa na utendaji wake wa kazi. 

Mbilinyi alikuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero kabla ya kuhamishiwa Dodoma na baadaye Bagamoyo. 

Alipotafutwa kuthibitisha maneno yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa facebook, Kibatala alisema: “Ni kweli niliandika kwenye ukurasa wangu wa facebook na ninaomba maneno hayo yabaki kama yalivyo, naona watu wengine wameanza kutafsiri vinginevyo.”

Katika hukumu hizo, Majaji Projest Rugazia na Penterine Kente waliwapa ushindi wabunge wawili wa Chadema, Susan Kiwanga na Peter Liajualikali baada ya kukosekana ushahidi wa kutengua matokeo hayo.

Juhudi za kumtafuta Mbilinyi kuzungumzia hatua iliyochukuliwa dhidi yake hazikuzaa matunda kutokana na simu zake zilizopigwa mara nyingi kutokuwa hewani.

#YALIYOJIRI>>>>Mbowe Ahojiwa na Kuachiwa Kwa Dhamana.Tundu Lissu Asisitiza Oparesheni UKUTA Iko Palepale.Fahamu zaidi hapa.

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema licha ya viongozi wa chama hicho kutishwa, kukamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi, bado msimamo wao kuhusu operesheni Ukuta itakayofanyika Septemba Mosi mwaka huu uko pale pale.

Chama hicho kinatarajiwa kufanya operesheni mpya iliyopewa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta).

Operesheni hiyo inatarajiwa kuwa itakwenda sambamba na uzinduzi wa mikutano ya hadhara nchi nzima, ambayo itafanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Hatua hiyo imefikiwa na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi kwa siku nne mfululizo wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na kutoa maazimio matatu ambayo yatatekelezwa na chama hicho.

Pamoja na mambo mengine, chama hicho kimesema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini, kiliyodai kuwa yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwanasheria  Lissu alisema msimamo wao uko palepale na hakuna kilichobadilika.

“Wamemuhoji kwa taarifa aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari juu ya msimamo wa chama wa kufanya mkutano nchi nzima. Tatizo jeshi letu wakisikia maandamano, mkutano au mtu anamsema Magufuli basi anatuhumiwa kwa uchochezi, wametumia muda mrefu kumuhoji lakini mwisho wamemwachia kwa dhamana na amewahi ‘Airport’ ili aende kuhudhuria mazishi ya kamanda wetu Senga (Joseph) na watamwita watakapomwihitaji tena,” alisema Lissu.

Alisema pamoja na hayo bado msimamo wa chama hicho kufanya mikutano waliyoiita Operesheni Ukuta ipo pale pale ifikapo Septemba Mosi, mwaka huu.

“Nafikiri ni muhimu sana huko tunapoenda kuzungumza na wenzetu hii kitu inaitwa uchochezi ni nini? Tunashitakiwa kwa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo waliingiza vifungu vya uchochezi mwaka 1978 lengo lao kuu ni kuwafunga watu midomo na ilitungwa wakati wa mfumo wa chama kimoja.

“Hata hivyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ndiye wa kwanza kushtakiwa kwa uchochezi  pamoja na mwandishi Robert Makenge na mwenzao Rashid Bagedae, kwa msingi huo sisi tunafuata nyayo zake,” alisema.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema kuitwa mchochezi, ni jambo la ufahari kupinga udikteta kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere.

“Nasema hivyo kwa sababu Mwalimu Nyerere ndiye wa kwanza kuitwa mchochezi, ni kitendo cha kufunga watu midomo ili washindwe kuwaita watu wajinga pale wanapofanya ujinga.

“Tume ya Jaji Nyalali mwaka 1992 wakati mfumo wa vyama vingi unatambulishwa na kuanza nchini ilipendekezwa sheria hii ifutwe kwa sababu haiendani na mfumo uliopo lakini hakuna kilichofanyika,” alisema.

Mwanasheria huyo ambaye naye amefunguliwa kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, aliwataka wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi Agosti 2, mwaka huu mahakamani hapo.

“Dawa yao si majaji bali umma… umma ufurike, tutawashinda hawa watu makesi yenyewe ni haya ambayo hayana kichwa  wala miguu,” alisema na kushangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Mbowe alifika kituoni hapo akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwamo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ambaye hata hivyo alizuiwa kuingia katika chumba cha mahojiano.

Askari waliokuwa kwa wingi katika eneo hilo, walisikika wakisema kuwa anayepaswa kuingia ndani ni Mbowe, Mwanasheria Tundu Lissu na Wakili wa Chadema, John Mallya.

Lowassa, wafuasi wa Chadema na waandishi wa habari walilazimika kubaki nje huku askari wakiimarisha ulinzi wakiwa wamebeba bunduki zao huku magari yenye maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa pembeni.

Wakati chama hicho kikijiandaa kutekeleza Operesheni Ukuta Septemba Mosi, tayari Rais Magufuli amezuia operesheni hiyo na kuwaonya wale wote watakaokaidi agizo lake na kuamua kuandamana.