Mwenyekiti
wa Parole Augustino Mrema amewataka madereva bodaboda kote nchini
kujiepusha na tabia za kushiriki maandamano ya kisiasa yanayoandiwa na
baadhi ya wanasiasa kwa lengo la kuvunja sheria za nchi.
Pia amewaagiza waendesha bodoboda Kinondoni wampe majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa ili ayakabidhi kwa rais Magufuli.
Mwenyekiti wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
Baadhi ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani) alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo.
0 comments:
Post a Comment