Waziri
wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameweka wazi
anachoamini ni bora katika mabadiliko yaliyofanywa na wanachama wa
kalabu ya Simba.
Wanachama
wa klabu ya Simba wamepitisha kwa pamoja kuwa klabu yao kuingia kwenye
mfumo wa kampuni na hisa kuanza kuuzwa hasa ikiwa ni siku chaache baada
ya mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji ‘Mo’ kutangaza hadharani nia
yake ya kutaka kununua hisa asilimia 51 kwa Sh bilioni 20.
Nape
ameandika kupitia mtandao wa Twitter akieleza uamuzi huo wa wanachama wa
Simba kama utasimamiwa kwa uhakika utakuwa na tija.
Huku
akisisitiza mfumo mpya kama utasimiwa utakuwa na tija kwa mashabiki wa
Simba kununua hisa, ikiwa ni maana maendeleo ya Simba yanaweza
kuchagishwa na Wanasimba wenyewe.
Kauli
hiyo ya Nape, inaonyesha wazi inaunga mkono uamuzi wa wanachama hao wa
Simba walioupitisha katika mkutano wa mwaka wa wanachama Jumapili
iliyopita.
Lakini anaweka msisitizo katika usimamizi bora kwenye katika mfumo huo ili kuufanya kuwa na tisa.
0 comments:
Post a Comment