Friday 15 September 2017

Ripoti ya Shambulio la Tundu Lissu Yaota Mbawa Kamati ya Bunge Yashindwa Kuwasilisha.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge imeshindwa kuwasilisha ripoti juu ya shambulio la risasi la Mbunge wa Sindida Mashariki Tundu Lissu, ambayo ilitakiwa kuwasilishwa leo kabla ya Bunge halijaghailishwa.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Adadi Mohamed Rajabu ambaye ni Mbunge wa Muheza kwa kudai muda waliopewa kukamilisha ripoti hiyo ni mdogo hivyo hawakuwahi kukamilisha.

Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama ya Bunge inatarajiwa kukutana kuanzia kesho ili kujadili na kuiwasilisha ripoti hiyo katika bunge  lijalo litakaloanza mwezi Novemba 2017.
Ikumbukwe kwamba baada ya kutokea tukio la kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu, Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe aliwasilisha hoja ya kulitaka bunge liunde kamati maalum ya kuchunguza tukio hilo ili iweze kubainika aliyefanya tukio hilo, na Spika Mhe. Job Ndugai alikubali na kupitisha hoja hiyo.

TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment