Mbunge
wa Iringa mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa ameibuka
na kumvaa Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai kwa kumwambia hana sifa ya kuwa
kiongozi wa kusimamia nidhamu ndani ya bunge bali alipaswa kuwa gerezani
muda huu.
Peter
Msigwa ameleza hayo mchana wa leo alipokuwa mjini Nairobi nchini Kenya
kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa
kwa kupigwa na risasi na watu wasiofahamika katika siku za hivi karibuni
na kupelekea kuamsha hisia za watu wengi juu ya jambo hilo ambalo
halikuwahi kutegemewa kutokea Tanzania nchi yenye amani na usalama wa
kutosha.
"Ninaomba
mumuogope Mungu kwa sababu tunaleta mchezo na maisha ya Watanzania,
mnataka kutunyamazisha ili tusiseme. Tutasema mpaka mwisho wetu kwa
sababu uhai wetu na usalama wa taifa letu umetishiwiwa kwa kiwango cha
juu sana lakini Mhe. Ndugai wewe kama spika unasifa gani ya kutuambia
sisi tuwe na adabu ndani ya bunge wakati wewe mwenyewe kipindi cha
kampeni ulionekanaa ukipiga watu hadharani na fimbo, ulitakiwa uwe
gerezani na siyo kutusimamia nidhamu ndani ya bunge", amesema Msingwa.
Pamoja
na hayo, Msigwa ameendelea kwa kusema "Nakuchukulia Mhe. Job Ndugai
kama wewe ni adui, yaani wewe ni adui wa usalama wa taifa la Tanzania
kwa sababu unasababisha muhimili wa bunge uwe dhaifu kutokana na
serikali ya Tanzania imekuteka na kukupa maagizo na kulifanya bunge liwe
butu, lishindwe kusimamia maamuzi na kulisimamia serikali. Nasema haya
kwa ujasiri mkubwa sina kitu cha kuogopa tena kama ndugu yetu
ameshapigwa risasi na tumeshaambiwa tunaofutwa ni sisi hivyo hatuna cha
kuogopa kusema jambo lolote", amesisitiza Msigwa.
Kwa
upande mwingine, Mchungaji Msigwa amedai muda mwingine wanashindwa hata
kuwaambia watoto wao kuwa Mhe. Job Ndugai ni kiongozi wao wa bunge kwa
kuwa wanatishwa, wanafukuzwa pamoja na kupigwa pingu huku akisisitiza
kuwa yupo tayari kufukuzwa bungeni lakini hatoweza kukaa kimya.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment