Baada
ya malalamiko ya muda mrefu ya serikali ya China juu ya mtandao wa
ujumbe mfupi wenye kubeba mafaili ya Sauti, Picha na Video “WhatsApp”
hatimaye imeuondoa rasmi nchini humo.
Imeripotiwa
kuwa mtandao wa WhatsApp haupatikani nchini China kwa siku ya tatu sasa
ambapo inadaiwa kuwa Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo 'Observatory of
Network Interference' (OONI) imefuta matumizi ya mtandao huo.
WhatsApp
ambayo inamilikiwa na kampuni ya Facebook yenye makao yake makuu nchini
Marekani imekuwa kwenye mgogoro na China ikilalamikia Serikali na
mamlaka za usalama nchini humo kuingilia mawasiliano ya wateja wao kwa
madai ya kufanya uchunguzi wa usalama wa taifa.
Hata
hivyo kwa wageni wanaoingia nchini China huduma hiyo bado inapatikana
kupitia SIM Card za mataifa yao hivyo inaonekana huduma hiyo imesitishwa
kwa raia wa China pekee.
Mkurugenzi
mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg bado hajatoa taarifa yoyote
kuhusiana na hatua hiyo ambayo imechukuliwa na serikali ya China ambayo
awali ilipinga matumizi ya mtandao wa Facebook nchini humo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment