Wabunge
wawili wa Chadema wametumia mahojiano nje ya nchi kuzungumzia matatizo
ya Tanzania wakisema hayawezi kumalizwa na mtu mmoja bali kwa mifumo
imara ya mihimili ya Mahakama, Bunge na Serikali.
Wakizungumza
katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha KTN cha Nairobi, Kenya
jana Jumapili walisisitiza umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya ili kuipa
nguvu mihimili hiyo.
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema ufisadi ambao Rais John Magufuli
anaushughulikia sasa ulifanywa na watendaji waliokuwa chini ya Chama
cha Mapinduzi (CCM).
Alisema
chama hicho kimeongoza nchi tangu Tanzania ilipopata Uhuru, hivyo
ufisadi huo ulifanywa na viongozi waliokuwa chini ya chama hicho.
“Ili tuwe na mfumo wenye nguvu tunatakiwa kubadilisha Katiba ili tuwe na Mahakama na Bunge huru,” alisema.
Lema alisema kumtegemea mtu mmoja hakuwezi kuleta mafanikio kama ambayo yamefikiwa na Kenya.
Alisema
Katiba ikibadilishwa na kuwa na vipengele mbalimbali, vikiwemo vya kuwa
na Tume Huru ya Uchaguzi na kumshtaki Rais akitoka madarakani Tanzania
itakuwa imepiga hatua.
Alisema mabadiliko ya Katiba nchini Kenya si tu yataisaidia katika siasa bali katika kukuza uchumi wao.
“Uamuzi
wa Mahakama ya Juu ya Kenya kufuta matokeo ya Rais si tu yatawasaidia
kisiasa bali yatajenga imani hata kwa wawekezaji,” alisema.
Alisema wawekezaji wataongezeka nchini Kenya kwa sababu wanakuwa na imani na Mahakama.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alisema
Rais ana nguvu kuliko mihimili mingine na amekuwa akitoa maelekezo kwa
mihimili hiyo.
“Bunge
la Tanzania limetekwa na Serikali, wenzetu CCM wako wengi kuliko sisi
wapinzani, wakikaa kwenye Party Caucus (vikao vya chama) yao wanaamua
mambo yenye manufaa kwa chama chao,” alisema.
Alisema madhara ya wabunge wa CCM kufanya uamuzi wenye manufaa kwa chama hayawaathiri wapinzani tu, bali Watanzania kwa jumla.
Wabunge
hao wako jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa
risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma.
==>Wasikilize hapo chini
==>Wasikilize hapo chini
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment