MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Idris Sultan amekuwa kwenye tetesi nyingi ambazo zimekuwa zikiendelea kila kona juu ya maisha yake, ikiwemo mamilioni aliyoyavuna kwenye Jumba la Big Brother ‘Hotshots’ kwamba yamepukutishwa na wanawake wa Kibongo na kwa sasa hana kitu pamoja na mambo mengine mengi.
Ili kukidhi kiu ya mashabiki kufahamu nini kinaendelea kwenye maisha yake binafsi na ya sanaa ikiwemo kuhusishwa kuwago-nganisha warembo wawili matata Bongo, Wema Sepetu pamoja na Sanchoka.Ijumaa lilimtafuta mchekeshaji huyo ambaye pia ni mtangazaji wa redio na kupitia makala haya anafunguka kila kitu;
Ijumaa: Vipi kuhusu kazi zako kwa sasa za vichekesho, unaweza kuelezea namna unavyozifanya, matamasha unayofanya na mipango yako mingine kwa sasa?
Idris na Wema Sepetu.
Idris: Sijafanya Stand-Up Comedy kwa muda sasa lakini malengo yangu kwa sasa ni kufanya kitu cha tofauti kwenye shoo yangu ya Sio Habari.
Ijumaa: Uliitwa Marekani kwa ajili ya kucheza muvi, nini kinaendelea katika projekti hiyo?
Idris: Nimefanya audition tano hadi nikafanikiwa kuchaguliwa kwenye muvi hiyo iitwayo Ballin ya Hollywood. Sasa tupo kwenye hatua za mwanzo za uzalishaji lakini rasmi tutaanza mwanzoni mwa mwaka 2018 na bajeti yake ni dola kama Mil. 5 (zaidi ya shilingi bilioni 11 za Kibongo).
Ijumaa: Unawezaje kufanya kazi ukiwa mtangazaji, mchekeshaji na muigizaji, unaugawaje muda wako?
Idris: Kazi zote zinategemeana na sina tatizo na muda wangu. Asubuhi nakuwa Choice FM katika kipindi changu, mchana nadili na projekti yangu ya Foreman ambayo ni brand ya viatu na usiku nakomaa na skripti za muvi na tamthiliya.
Ijumaa: Umewahi kuwa mshiriki wa Big Brother, kuna lolote ambalo mashabiki wako hawalifahamu kwa sasa, kama kualikwa, kuwa na projekti nalo au lingine lolote?
Idris: Ninachojua ni kwamba Big Brother kwa sasa imefungua matawi mengi ikiwemo Msumbiji, Angola, Nigeria na sehemu nyingine, kuhusu hayo mengine hakuna ambalo limetokea hata moja na wala hakuna kinacho-endelea.
Sanch.
Ijumaa: Baada ya kutoka tu Big Brother ndani ya kipindi kifupi kuna tetesi zilienea kwamba umefulia na waliokumaliza ni warembo wa Kibongo, hili unalizun-gumziaje?
Idris: Si kweli, hoji warembo hata 100 ambao unafahamu nipo karibu nao au nimewahi kuwa karibu nao kama yupo ambaye atakwambia amekula pesa zangu niambie nikamdai.
Ijumaa: Ukiwa miongoni mwa wasanii Bongo wanaozun-gumziwa kwenye mitandao ya kijamii unazungumziaje mapokeo ya Wimbo wa Seduce Me wa Ali Kiba?
Idris: Wimbo wake ni mzuri na kusingekuwa na ushindani wa timu nina uhakika wimbo usingepasua kama ulivyopasua.
Ijumaa: Lakini pia umekuwa ukihusishwa kuwa kwenye uhusiano na Wema wakati huohuo na Sanchoka ‘Sachi’ na kwamba wamekuwa wakipishana nyumbani kwako, vipi hili ni kweli?
Idris: Siku zote Wabongo huwa ni watu wa kujiongeza wanaposikia kitu.
Lakini pia juu ya kuwachanganya Wema na Sanchi ni kwamba hawajawahi kupishana nyumbani kwangu, sina taarifa zozote kuhusu wao kuwachanganya labda wajichanganye wenyewe au useme nimewachanganya kama marafiki tu.
Ijumaa: Kama Mtanzania unazungumziaje kupigwa risasi kwa Tundu Lissu?
Idris: Kama ni hii ishu imekaa kisiasa naona ni tendo linaloonyesha uoga na ulimbukeni mkubwa sana. Risasi zaidi ya 30 siyo tendo la kujeruhi ni kuua kabisa. Serikali ina haja ya kulifuatilia na iwape mrejesho Watanzania nini kilitokea na wahusika wakamatwe na wajulikane.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment