Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mbunge wa Bukoba Mjini
(Chadema), Mh.Wilfred Lwakatare na mwenzake, Ludovick Rwezaura
waliokuwa wakistakiwa kwa kosa la kula njama za kutoa sumu kwa nia ya
kumdhuru aliyekuwa Mhariri wa Gazeti.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amewaachia huru washtakiwa hao leo
Alhamisi mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa
kuomba kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwenendo wa
Makosa ya Jinai kisha Mahakama kuridhia.
Kishenyi ameomba kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu hicho kwa sababu
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea kuwashtaki washtakiwa
hao na baada ya kutolewa kwa maelezo hayo hakimu aliwaachia huru
washtakiwa hao leo.
Pamoja na hayo Mh. Lwakatare amemshukuru Mungu kwa kuwa na siku njema na yenye furaha.
Hata hivyo wakati kesi hiyo inaondolewa mahakamani hapo alikuwapo Mbunge
Lwakatare pekee huku mshtakiwaRwezauraakiwa hajafika kwa kile
kinachodaiwa kuwa na matatizo ya kifamilia.
Awali Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ilimfutia kesi ya
makosa ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph, baaadaye
Jamhuri ilikata rufaa kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment