Kiongozi wa CUF Mheshimiwa Ali Juma Suleiman ambaye alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa (CUF) Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa (CUF) Wilaya ya Magharibi A. Zanzibar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
Baadhi ya viongozi wa (CUF) na wanachama pamoja na wananchi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatilia mwili wa Marehemu Ali Juma Suleyman.
Naibu Katibu Mkuu (CUF) Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa Mheshimiwa Ali Juma alikuwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatia kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa kisha baadaye kutupwa katika maeneo ya Masingini na makundi ya watu yanayoendesha vurugu Zanzibar.
"Nasikitika kutangaza kifo cha Mheshimiwa Ali Juma Suleiman, Kaimu Mwenyekiti wa CUF Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Wilaya ya Magharibi A. Amefariki dunia majira ya saa 4 usiku hapa jana hapa Mnazi Mmoja Hospital baada ya kupigwa vibaya na Mazombi juzi usiku" alisema Naibu Katibu Mkuu CUF Nassor Mazrui
Viongozi wa CUF wamesema kuwa mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi tayari na sasa wamekabidhiwa kwa ajili ya kufanya mazishi ambayo yatafanyika leo katika makaburi ya Mwanakwereke, nje kidogo ya mji wa Unguja.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment