Simba imeendeleza dozi katika mechi zake za kirafiki baada yakuichapa Burkina Faso ya Morogoro kwa mabao 5-0.
Katika
mechi hiyo ya kirafiki, Ibrahim Ajib ameendelea kung’ara baada ya
kufunga mabao mawili huku Moussa Ndusha raia wa DR Congo, Shiza Kichuya
na Said Ndemla kila mmoja akitupia moja.
Hii
ni mechi ya tatu ya Simba ya kirafiki na zote imeshinda ikianza na ile
dhidi ya Polisi Moro iliyoshinda 6-0 kabla ya kuitwanga Moro Kids 2-0.
0 comments:
Post a Comment