Sunday, 29 January 2017

Mbinu Mpya za Wanawake wa Siku Hizi Wanaosaka Ndoa Kwa Nguvu..Ni Noma Sana.Fahamu zaidi hapa.

Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi anaondoka...
Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka...

Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Hny nitunzie nimesahau hereni zangu mezani

Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadha,na ole wako uvihamishe alipoacha,kesi zinaanza...

Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza...Anahamia taratibu.. Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na 'Foundation'...

My Brother,huna haja ya kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO....
Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my days',Zamani nilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku hizi kuna Missed days,ukiambiwa hivi tu jua imekula kwako, inawindwa ndoa hapo...

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MESSI ALIVYOMNUNULIA MAMA YAKE CHUPA YA MVINYO KWA MILIONI 1.3.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Lionel Messi ameonyesha fedha si chochote kwa mzazi, maana amenunua chupa mvili za mvinyo kila moja ikiwa na thamani ya pauni 430 (zaidi ya Sh milioni 1.3).
Maana yake kwa chula mbili ni Sh milioni 2.6 ikiwa ni kukamilisha sherehe ya miaka 57 ya mama yake mzazi airway Celia.

Mvinyo huo ghali aina ya Vega-Sicilia's Unico, ulionekana kwenye picha za mtandao wa Instagram wakati Messi akisherekea pamoja na mama yake.

Baadaye alitupia picha wakati Celia akiwa anasherekea na wajukuu zake.


Messi ni raia wa Argentina ambaye alihamia Hispania akiongozana na baba yake, wakati huo Messi akiwa na umri wa miaka 13.


Messi alitua Argentina akiwa amekwenda kutibiwa ugonjwa wa kukua huku akitakiwa kujiunga na Barcelona ambayo aliiomba imsadie gharama za matibabu.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

#YALIYOJIRI>>>AJALI YA MGODINI: Wachimbaji watano kati ya 15 waliofukiwa kwenye kifusi mgodi wa RZ Geita wameokolewa asubuhu hii, juhudi za kuwaokoa waliobaki zinaendelea.Fahamu zaidi hapa.

Wakati  imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko Geita , wamebakiza mita tatu kuwafikia waliofukiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani akizungumza na ndugu wa watu waliofukiwa amesema kwamba wanafanya mpango wa kuwapelekea chakula wachimbaji hao.

Amesema kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kwamba wapo kumi na watano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula.

Alisema waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao waliandika majina  na  mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama.

Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji.

Watu wengi wapo katika eneo hilo wakiwemo ndugu wa waliofukiwa lakini kwa juhudi wanazoziona za uokoaji wametulia na kufuata maelekezo wanayopewa ikiwemo kukaa mita 500 toka eneo la tukio.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Diamond Awakomesha Ali Kiba na Wema Instgram...!!!.Fahamu zaidi hapa.

MREMBO asiyeishiwa matukio kila kukicha Bongo, Wema Isaac Sepetu na msanii wa Bongo Fleva anayewika kwa wimbo wake Aje, Ali Kiba, mwisho wa wiki hii wamenagukia pua katika mitandao ya kijamii na Diamond Platnumz ameendelea kuwaonyesha kuwa yeye ana nguvu kuwazidi wao mtandaoni.
Awali iliripotiwa kuwa Wema amefuta picha zake zote katika mtandao wake wa Instagram kwa shabaha ya kurudi kwa kishindo na kuwaonyesha watu kuwa yeye ndiye malkia wa mtandao huo hapa nchini. Jitihada zake ziligonga mwamba pale aliporejea na kutegemea mapokezi makubwa na haikuwa hivyo. Daimond aliweka video ya familia yake iliyowaonyesha laivu akiwa na mkewe na mwanaye Tiffa Dangote.
Video hiyo ilipata watazamaji 20,708 na wachangiaji zaidi ya 600 na kusababisha watu wengi kuacha kumzingatia Wema na kurudi kwa Diamond. 

Aidha Ali Kiba amekuwa akiendelea kushushiwa matusi na kupewa lawama na mashabiki zake baada ya kuonekana mahojioano kupitia vituo mbalimbali vya televisheni akisema kuwa yeye hapo alipofika ni juhudi zake.

Mashabiki zake hawakupendezwa na kauli hiyo na kuitafsiri kama majigambo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Picha: Dunia Yampinga Trump Baada ya Marufuku kwa Waislamu Kuingia Marekani Kuanza Jumamosi Hii..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Uamuzi wa Donald Trump kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu kutoka kwenye nchi zenye raia wengi wa dini hiyo, umesababisha hasira kuu duniani kote na wahamiaji wakikataliwa kupanda ndege kuingia Marekani.
Raia waliokuwa na hati za kusafiria kutoka Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walizuiliwa kwenye viwanja vya ndege, wakati wale waliokuwa wameshapanda ndege walishikiliwa baada ya kutua Marekani.
Katika tukio moja, abiria watano wa Iraq na mmoja wa Yemeni, waliokuwa na visa halali, walizuiliwa kupanda ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikitoka Cairo kwenda New York na hatimaye kuelekezwa kwenye ndege zinazorudi kwenye nchi zao.
Mwanamke mmoja aliyekiambia mauaji ya Isis nchini Iraq mwaka 2014, alizuiliwa kupanda ndege mjini Baghdad, baada ya kusubiria visa kwa miezi mingi ili akaungane na mumewe ambaye tayari yupo Marekani. Rais Trump amepiga marufuku kwa miezi mitatu wakimbizi toka nchi saba duniani, ili kuchuja magaidi wa kiislamu wasiingie nchini humo.
Wakimbizi kutoka Syria wamepigwa marufuku kimoja.
Hata hivyo, jaji mmoja alitoa ruhusa Jumamosi kwa raia kutoka nchi hizio saba waliokuwa wameshaingia nchini humo, wale waliokuwa njiani, wenye visa halali kukaa Marekani. Waandamaji kadhaa walikusanyika kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa Trump. Maandamano zaidi yatafanyika Jumapili hii.
 
Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Saturday, 28 January 2017

WAKATI AKIJIFUA NA KIKOSI BARCELONA, WASWIDI WAIOMBA TFF KIBALI CHA ULIMWENGU.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kila kitu sasa safi kwa mshambuliaji Thomas Ulimwengu katika kikosi cha AFC Eskilstuna kinachoshiriki Ligi Kuu ya Sweden, kwani licha ya kuanza mazoezi, timu hiyo imemuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) mchezaji huyo.

Tayari Ulimwengu na kikosi chake cha AFC wako nchini Hispania katika jiji la Barcelona ambako wameweka kambi.

Siku chache tu baada ya kuanza mazoezi na timu hiyo, timu hiyo imetuma barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiomba ITC ya Ulimwengu ili aweze kujiunga nao, hii inamaanisha klabu hiyo imekoshwa na uwezo wa straika huyo.

Ulimwengu ambaye alikuwa akiichezea TP Mazembe ya DR Congo, alijiunga na timu hiyo Jumatatu ya wiki hii na kuanza mazoezi juzi Jumatano kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred amesema AFC Eskilstuna imetuma maombi ya ITC ya Ulimwengu jana na leo hii wanatarajia kuituma ili akaanze kazi yake ya kucheza soka mara moja.

“Leo hii (jana) tumepokea maombi ya ITC ya Ulimwengu kutoka AFC Eskilstuna na hivi sasa tupo katika harakati za kuiandaa hivyo mpaka kufikia kesho (leo) itakuwa tayari tumeituma,” alisema Alfred.


Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wastara Aweka Wazi Sababu ya Kuacha Wanaume.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa filamu, Wastara Juma ameweka wazi sababu kubwa ambayo ilimpelekea kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Bondi Bin Salim na kwenda kuolewa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma kisha kuachana naye na kurudiana tena na mpenzi wake 
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live cha (EATV) Wastara anasema aliamua kuachana na Bond kutokana na tabia yake ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi na pombe pamoja na tabia zingine ambazo yeye alishindwa kuvumilia na kuamua kuachana naye.
"Ukweli ni kwamba kuna issue nzito ilitokea kati ya mimi na Bond mpka Bond mwenyewe aliamua kutoa ushuhuda na kutubu juu ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi, mpka aliamua kuondoka mwenyewe kwenda mbali na mazigira ambayo mimi nilikuwa naishi, alikuwa anatafuta njia ya kujisaidia ili aache vile vitu ambavyo binafsi nilikuwa sivipendi, kwanza kwenye mahusiano kulikua hakuna uaminifu kabisa, ilifikia hatua mpka kuna watoto wengi sana walikuwa wanaletwa wengine ni kweli wengine wa uongo vile vitu binafsi kama mwanamke vilikuwa vinaniumiza" alisema Wastara 
Mbali na hilo Wastara anasema baada ya hapo familia yake ilimshawishi aweze kuolewa na Mbunge huyo Sadifu ambaye alikuwa anahitaji kuwa naye na kusema aliwasikiliza sababu siku zote familia yake huwa inaiweka mbele na kuwasikiliza na kuamua kwenda kuolewa na Mbuge lakini anasema baada ya kuingia huko alikutana na matatizo mara kumi ya alipotoka hivyo ndoa hiyo ilimshinda ndani ya siku sabini na kitu  na kuamua kuachana naye.
Wastara alizidi kuelezea kuwa baada ya hapo Bond alirudi toka reharb akiwa ameachana na tabia zake zile na alijiridhisha kuwa sasa amebadilika hivyo akarudiana naye na wanaendelea kuishi pamoja mpka sasa kama wapenzi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wanajeshi Waua Kondakta Kwa Kipigo Tanga.Fahamu zaidi hapa.

Kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya kambi ya jeshi jijini Tanga.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado kinachunguzwa.

Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku, ambapo mashuhuda walidai kuona kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi na kuingizwa kambini na baadaye alitolewa akiwa hajitambui

Akizungumzia tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

“Tumekuwa tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,” alidai Khalid.

Diwani wa Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji la Tanga, Alhaji Mustapha Selebosi alisema sababu za kipigo hicho ni mwanafunzi wa shule moja jijini Tanga ambaye ni mtoto wa ofisa wa JWTZ kuzozana na kondakta.
 
==>Zaidi, Tazama  Video Hii


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wowowowo..Wema Sepetu Aibuka Upya Instagram ...!! ..Fahamu zaidi hapa.

MREMBO asiyeishiwa matukio kila kukicha Bongo, Wema Isaac Sepetu hatimaye ameibuka kwa mara nyingine Instagram baada ya kuitelekeza akaunti yake kwa muda ambapo alifuta picha zake zote za zamani na kubakiza maswali mengi kwa mashabiki wake ambao hawakuweza kupata majibu.
Kabla ya kufuta kila kitu kwenye akaunti yake hiyo, Wema alikuwa na zaidi ya followers milioni mbili na nusu, ambao wameendelea kumvumilia hadi jana jioni aliporejea na kuanza kuweka picha mpya kwenye profile yake kisha akaipost upya kwenye akaunti yake hiyo.
Hadi muda huu, Wema bado hajatoa sababu ya msingi iliyomfanya aamue kufuta posti zake hizo pamoja na kuwa na maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake wakimtaka awafafanulie kilichomfanya kuchukua uamuzi huo.
Wema ameandika yafuatayo kwenye akaunti yake:
Happy 2017… and am excited.. how Many Likes?? Share from
This one and am gonna Tell You something to Celebrate for the whole Year…. #WSSoCloseToYou #WSladieschoice #WSyourAddiction
#unataka kusikia jambo zuri kutoka kwangu kwa mwaka 2017? Gonga Likes za kutosha and nitarudi kukung’ata sikio… This be your First Image…. There is plenty of these Just for You…. I missed You too…. @ossegrecasinare You are Life….

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Ommy Dimpoz Afunguka Mapya Juu ya Wasanii wa Label ya WCB ya Diamond..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Kajiandae' akiwa na Alikiba amefunguka na kusema hata yeye anaweza kufanya collabo na msanii yoyote yule kutoka WCB. 
Ommy Dimpoz alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWz cha (EATV) na kusema kwenye muziki kuna wakati unaweza kupata wimbo ambao unahitaji collaboration na msanii fulani ili uweze kuwa bora zaidi hivyo inapotokea hivyo ni lazima ufanye mawasiliano na msanii huyo ili ufanye naye hata kama yupo WCB au sehemu nyingine.
"Siyo tu Nedy hata mimi naweza kufanya kazi na msanii kutoka WCB siyo tatizo, kwa sababu huu ni muziki pia ni biashara na lazima uangalie wimbo huu naotaka kufanya nikifanya na msanii fulani kutakuwa na hiyo combination nzuri? Kwa hiyo haijalishi kikubwa wote tunafanya muziki na kufanya biashara na kuangalia nikifanya na msanii huyu kazi yangu itakuwa na impact gani kwa hiyo hivyo vitu vyote vinawezekana" alisema Ommy Dimpoz
Mbali na hilo Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa kwa mwaka huu ataachia kazi nne, mbili zikiwa na kazi za kushirikiana na kazi mbili atakuwa amefanya yeye mwenyewe


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mume na mmiliki wa Famasi Watiwa mbaroni Kwa Kusababisha Kifo cha mjamzito.Fahamu zaidi hapa.

Watu  wawili, akiwemo mmiliki wa duka la dawa muhimu za binadamu katika kijiji cha Itagata wilayani Manyoni, wanashikiliwa na Polisi mkoani Singida kwa tuhuma za uzembe wa kusababisha kifo cha mjamzito, Heleni Maduhu (29).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni mume wa marehemu, Bahame Kamuda (32) na Joseph Hengwe (50) ambaye ni mmliki wa duka la dawa katika kitongoji cha Kilulumo, kijiji cha Itagata Tarafa ya Itigi wilayani Manyoni.

Alisema tukio lilitokea kitongoji cha Lulanga kijijini hapo Januari 25, mwaka huu saa 9.30 alasiri wakati mjamzito huyo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Misheni ya Itigi kwa matibabu zaidi kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kujifungulia kwenye duka la Dawa la Hengwe.

Alisema kuwa siku moja kabla, mume wa mjamzito huyo alimpeleka mkewe kwenye Zahanati ya kijiji Itagata ili kufanyiwa uchunguzi ambapo inadaiwa muuguzi wa Zahanati hiyo, Grace Simon iliwaambia njia ya uzazi ilikuwa haijafunguka; hivyo akawashauri warudi nyumbani.

Alisema kuwa aliporejea nyumbani hali ya mjamzito huyo ikawa mbaya hivyo kumlazimu mumewe kumpeleka Zahanati ya jirani ya Misheni katika Kijiji cha Mitundu kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, Kamanda Magiligimba alidai kuwa wakiwa njiani, mumewe aliona hali ya mkewe inazidi kuwa mbaya zaidi, aliamua kumpeleka kwenye duka la dawa muhimu linalomilikiwa na Hengwe lililopo jirani ambapo alijifungua mtoto wa kiume.

“Kutokana na mjamzito huyo kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua, mumewe aliamua kumkimbiza katika Hospitali ya Misheni ya Itigi kwa pikipiki lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kufika mbali kabla ya mama huyo kufariki dunia,” alisema Magiligimba.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Harmo Rapa Ang'ang'ania Jina la Harmonize ,Atoa Sababu Hizi Nzito za Kufanya Hivyo..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa bongo flava ambaye ndiyo anaanza kuchipukia, Harmo Rapa, amesema kuwa hana mpango na wala hawezi kubadili jina hilo lililompa umaarufu kwenye muziki kwa hofu ya kupoteza mashabiki wake. 
Msanii huyo anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la 'USIGAWE PASI'. ametoa msimamo huo kupitia eNewz ya EATV iliyomtafuta kuzungumza naye kuhusu mpango wa kubadili jina lake na kutotumia jina la 'Harmo Rapa'.
“Mimi sina mpango wa kubadili jina langu kwa sababu naogopa kupoteza mashabiki zangu na ukiangalia kwa sasa jina la Harmo Rapa limeshakuwa kubwa na tayari nimeshajitengenezea mashabiki kupitia jina hilo”
Pia amesema kuwa hana mpango wa kwenda WCB na wala hahitaji msaada wowote kutoka kwao huku akionesha jeuri kuwa angeweza kutoka hata bila kutumia jina hilo. "Hata bila kufananishwa na Harmonize mimi ningetoka tu"
Harmo Rapa ni moja kati ya wasanii ambao wamepata kiki ya kutosha kutokana tu na muonekano wake ambapo watu wengi wamekuwa wakimfananisha na Harmonize kutoka WCB.
Msanii huyo hivi karibuni katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alijifananisha na Fid Q na kuwaacha watu midomo wazi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kasi ya uokoaji watu 14 waliofukiwa mgodini yazidi kupamba moto.Fahamu zaidi hapa.

Bado kazi ya uokoaji wa watu 14 waliofukiwa na kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita inaendelea, na hadi jana waokoaji hawajafanikiwa kuokoa mtu yoyote.

Pamoja na juhudi hizo za uokoaji, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga amesema kuwa ana imani watu hao wataokolewa wakiwa hai.

Amesema kuwa jana imefanyika kazi kubwa ya kuchimba kifusi ili kutafuta njia ya kuwafikia waathirika huku mipira zaidi ya Oxygen ikiingizwa chini ya mgodi waliko watu hao ili kuwaongezea hewa.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Latson Mponjoli amesema juhudi za uokoaji zinaendelea kwa ushirikiano wa vikosi vya uokoaji vya Kampuni ya Geita Gold Mine (GCM), Jeshi la Zimamoto na Polisi pamoja na kikosi cha ukoaji cha Sekta ya Madini.

Amesema hali ni shwari katika eneo hilo na wana matumaini ya kuwafikia watu hao wakiwa hai.

Pia, Kampuni inayoendesha mgodi huo imesema kutokana na kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina mmoja waliofukiwa kifusini. Ilielezwa kuwa watu pia waliomshuhudia Mtanzania mmoja akingia mgodini humo bila kujiandikisha na hivyo kufanya waliofukiwa kufikia 14.

Watanzania 13 na raia mmoja wa China walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Idrisa Sultani Aaamua Kuanika Kila Kitu Jinsi Wema Sepetu Alivyomkausha Milioni 500 Zake za Ushindi wa Big Brother..!! ..Fahamu zaidi hapa.

Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa Idris Sultan ameamua kukiri wazi kuwa kipindi yupo kwenye mahusiano na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu alikumbwa na ukata.
Kupitia kipindi cha Clouds e cha Clouds Tv Idris Sultan amesema wakati yupo kwenye mahusiano yake yaliyopita na mrembo Wema Sepetu alikuwa kwenye Ukata hivyo nilijikuta sifanyi vitu vya maana kuliko
kipindi hiki ambapo yupo Single.
“ Wakati nipo kwenye mahusiano yangu yaliyopita niliyumba kidogo kiuchumi kwani sikuwa nafanya mambo mengi ya muhimu kuliko sasa hivi kwani hata watu wangu wa karibu watakueleza hivyo,nafurahi niko
single na naendelea kupambana“Alisema Idris.
Ikumbukwe idris alishinda tsh milioni 500 za kitanzania kwenye shindano la big brother Africa. Idris sasahivi ni mtangazaji wa choice FM

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Rais John Magufuli Aelekea Addis Ababa Kwenye Kilele cha Mkutano wa 28 wa Wakuu wa AU.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 25 January 2017

Simba Kutupwa Nje Kombe la Shirikisho..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Klabu ya Simba huenda ikatupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho kufuatia kumpanga beki wake Novalt Lufunga kwenye mchezo walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Polisi ya Dar es salaam huku akiwa na kadi nyekundu aliyoipata kwenye michuano iliyopita.
 Kwa mujibu wa rufaa ya klabu ya Polisi inadai kwamba Lufunga alilimwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa mwisho wa michuano hiyo msimu uliopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambapo Simba ilitupwa nje ya mashindano.
 Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' ambaye amelitolea ufafanuzi suala hilo huku akikanusha kuwa Lufunga hakucheza mchezo uliofuata baada ya ule wa Coastal, lakini pia akasema kuwa kanuni za mashindano hayo ni tofauti na kanuni za ligi.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

#Breaking News>>>Katibu Mkuu wa Simba Patrick Kahemele Aachia Ngazi ..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa  Kahemele zinaeleza aliandika barua na kamati ya utendaji ya Simba, imepitisha hilo.

Upande mwingine wa taarifa, umeeleza Kahemele anarejea na kujiunga na Azam TV ambako alikuwa akifanya kazi kabla.

“Kweli anaondoka, leo kamati ya utendaji ya Simba imekubaliana naye,” kilieleza chanzo.

Juhudi za kuwapata viongozi wa Simba walizungumzie hilo, zinaendelea.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Snura Afunguka Jinsi Anavyomtamani Leo Kesho Shilole..!!!..Fahamu zaidi hapa.

MWANADADA anayetamba na ngoma ya ‘Shindu’ Mwaga Maji Tucheze Kama Kambare, Snura Mushi (pichani) ameeleza kiu yake ya kutaka kufanya kazi na mwanadada mwenzake Zuwena Mohammed ‘Shilole’ endapo atakuwa tayari.
 
Snura amebainisha hayo usiku wa Jumanne, Januari 24, 2017 wakati akijibu swali kwenye interview ya kipindi cha Redio EFM. Snura amesema kuwa  kwa sasa hana bifu kabisa na Shilole, hayo yalikuwa mambo ya zamani na yalisha kwisha kitambo na endapo ikitokea nafasi ya wawili hao kukaa chemba na kufanya kazi pamoja yuko tayari kwa asilimia zote.
Shilole
“Kwa sasa sina bifu lolote na Shilole, tuko sawa, hayo yalikuwa mambo ya zamani sana tulishayamaliza, tupo sawa. Muziki wake na wangu uko tofauti hatuwezi kugombana”
Snura
“Kwanza natamani sana kufanya kazi pamoja na Shilole, ikiwezekana tufanye wimbo wa pamoja au movie (filamu) kwa kuwa yeye ni msanii mzuri wa kuigiza naamini tukifanya hiyo tutatengeneza pesa nzuri mimi na yeye”
“Kingine ni kwamba natamani pia kufanya naye shoo moja jukwaani hata kama ni hapa Dar es Salaam au popote, kwa maana sisi wasanii tupo kwa ajili ya kutafuta pesa, kwa hiyo ikitokea nafasi kama hiyo itakuwa poa sana.” Alisema Snura.
Shilole
Mbali na hayo Snura hakusita kueleza jitihada zake za kumtafuta Shilole licha ya yeye kuonekana kama hayuko tayari kufanya hivyo.
“Nimewahi kumtafuta kwa jitihada zangu ili tuweze kufanya angalau jambo moja kati ya hayo (shoo, wimbo au filamu) lakini inavyoonekana mwenzangu kama hayuko tayari.” Alimalizia Shilole.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mwana FA: Sina Mpango wa Kufanya Kazi Tena na Lady Jay Dee.Fahamu zaidi hapa.

Rapa mwana fa anaefanya vizuri na wimbo wake wa “Duke Suruali ” amefunguka na kuweka wazi hana tena mpango wa kufanya kazi na msanii lady jaydee.
 
Mwana FA alisema hayo kupitia kipindi cha planet bongo kunachorushwa na east Africa radio ” kwasasa sina mpango tena kufanya Kazi na lady jay dee na hili swali sijui kwanini linajirudia Mara kwa mara na wasanii wengine na sina tatizo nao


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Joh Makini unaoitwa "Waya".

Download wimbo wa Joh Makini-Waya.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa