Wednesday, 6 April 2016

#YALIYOJIRI>>>Mishahara ya vigogo wa Serikali Waliokuwa Wanalipwa Milioni 36 hadi milioni 40 kwa mwezi yaanza kufyekwa.Fahamu zaidi hapa.

Siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutoa agizo la kupunguza mishahara mikubwa ya watendaji wa mashirika ya umma, hatimaye Serikali kupitia Bodi ya Mishahara imeanza kazi ya kufanya marekebisho hayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli, kuagiza kushushwa kwa viwango vya mishahara ya viongozi wa mashirika ya umma ambapo wengine hulipwa Sh milioni 36 hadi milioni 40 kwa mwezi.

Jana  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema katika kipindi cha miezi 15 kuanzia sasa mishahara ya watumishi hao itapunguzwa na kuwa yenye uwiano.

“Katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa tunayo Bodi ya Mishahara ambayo ilianzishwa katika Serikali ya awamu ya nne na jukumu lake kubwa ni kufanya mapitio ya mishahara mbalimbali na kuhakikisha mishahara ya watumishi wa umma haipishani sana.

“Hatua ambazo tumeanza kuzitekeleza, tayari mamlaka zetu zimeanza kukutana kupitia Utumishi, Hazina na Msajili wa Hazina ili kuangalia namna ya kulitekeleza agizo hilo,” alisema Waziri Kairuki.

Alisema kutokana na hali hiyo mamlaka hizo hivi sasa zinaangalia mishahara ya taasisi mbalimbali na watumishi ili kuweza kubaini wale wanaolipwa zaidi ya Sh milioni 15 ni wangapi na itakatwa vipi.

Akizungumzia taasisi zinazozalisha kwa kiwango kikubwa na kuwa na uwezo wa kujiendesha, Waziri Kairuki, alisema Bodi ya Mishahara hivi sasa ina jukumu la kuangalia uwiano baina ya mtumishi wa umma na mashirika ya Serikali.

“Unakuta mtumishi wa taasisi X kiwango chake cha elimu, uzoefu, ujuzi, muda wa kuingia kazini pamoja na kazi anayoifanya ni sawa na ya mtumishi wa taasisi Y lakini unakuta mtumishi X analipwa mshahara mkubwa zaidi ya mara tano ya mtumishi Y jambo ambalo si haki katika utumishi,” alisema.

Kauli ya Rais Magufuli
Machi 30, mwaka huu akiwa wilayani Chato, Mkuu huyo wa nchi, alisema kuna watu wanalipwa kiwango kikubwa cha mishahara na wamekuwa wakiishi kuliko hata malaika na sasa ni lazima washushwe ili waishi kama shetani.

Hatua ya Rais Magufuli, kupitisha panga na kuweka uwiano wa mishahara kwa watendaji wa taasisi hizo unaelezwa kuwa utaisaidia uwajibikaji na usawa kwa watendaji.

Katika mkutano huo, Rais Magufuli, alishangazwa na baadhi ya bodi za wakurugenzi kushindwa kufanyakazi zao kwa mujibu wa sheria na badala yake wamekuwa na kazi ya kupandisha mishahara kwa watendaji.

Alisema anashangazwa na bodi hizo, kwani kila kukicha zimekuwa zikifanya kazi ya kupandisha mishahara pamoja na kufanya vikao nje ya nchi.

Alisema hivi sasa ameunda timu ya wataalamu ambayo imeanza kufanya kazi ya upunguzaji mishahara mikubwa kwa watendaji wakuu wa mashirika ya umma.

“Tena hawa wakurugenzi ndio wanaongoza kwa kulipwa fedha nyingi na hata kwenda kufanya vikao ulaya. Ninasema hapa kwamba suala hili litaanza kushughulikiwa katika bajeti hivi karibuni,” alisema Rais Magufuli.

Alisema tayari ameunda timu ya wataalamu ambayo inafanya kazi ya kupunguza mishahara hiyo na kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi ili asipatikane Mtanzania anayelipwa zaidi ya kiwango hicho.

“Kuna watu wanaishi kuliko hata malaika lazima tuwashushe waishi kama shetani,” alisema Rais Magufuli.

Tuesday, 5 April 2016

BREAKING NEWS>>>>MWENYEKITI WA CHADEMA IRINGA APATA AJALI NA KUFARIKI DUNIA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa Vijijini  Ndg.Sinkala Mwenda amepata ajali jana  jioni  eneo la Tanangozi na kukimbizwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu lakini bahati mbaya akafariki dunia muda mfupi wakati madaktari wakijitahidi kuokoa uhai wake. Pumzika kwa amani Kamanda Sinkara.!

#YALIYOJIRI>>>Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ateketea kwa Moto Akiwa Ndani ya Gari Lake.Fhamu zaidi hapa.

Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki baada ya kuteketea ndani ya gari lake jijini Dar es Salaam juzi.

Gari la Dk Mgaya liliteketea baada ya kugongana na lori katika eneo la Mbezi Africana, Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia juzi na kuwaka moto uliosababisha kifo chake.

Juzi picha mbalimbali zilisambaa zikionesha gari aina ya Toyota Prado lililopata ajali eneo hilo la Africana baada ya kugongana na lori, baadaye ilibainika kuwa aliyekuwa katika gari hilo ni Dk Mgaya.

Akizungumza  kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema gari la Dk Mgaya liliteketea na hata kushindwa kujulikana dereva wa gari hilo.

Alisema baadaye ndugu wa marehemu ndio walithibitisha kuwa gari hilo lililoteketea na dereva aliyekuwemo ni Dk Mgaya ambaye hata hivyo naye aliteketea ndani ya gari hilo.

“Lile gari liliungua na hakuna kitu kilichopatikana, hata wakati polisi wanafika eneo la tukio walikuta tayari dereva amekuwa majivu kutokana na kuteketea kwa moto… labda baada ya kupima vinasaba ndio itathibitika kama ilikuwa ni yeye,” alisema Kamanda Fuime.

Alisema hata gari hilo hawakuweza kulitambua mara moja na baada ya kufuatilia Mamlaka ya Mapato (TRA) ilibainika kuwa mmiliki wake ni Dk Mgaya.

Alisema “ndugu wa marehemu ndio wamesema kuwa ni ndugu yao.” 

Dk Mgaya alijiunga na idara hiyo miaka kadhaa iliyopita akitokea masomoni nchini Marekani na alikuwa ni mtaalamu wa artificial intelligence.

Monday, 4 April 2016

Habari Katika Magazeti ya siku ya Leo Jumanne ya April 5 yako hapa.


#YALIYOJIRI>>>Mafuriko yafunga Barabara kuu Itokayo Dodoma Kwenda Morogoro kwa saa 10.Fahamu zaidi hapa.

Zaidi ya magari 1,500 jana, yalikwama katika eneo la Chalinze Nyama wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa zaidi ya saa 10, baada ya mafuriko kuziba barabara kuu itokayo Dodoma kwenda Morogoro.

Mafuriko hayo yalitokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku mbili mfululizo.

Akizungumza katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema vyombo vya ulinzi na usalama vitakuwa katika eneo hilo ili kutoa ushauri kwa watumiaji wa barabara na kuwataka wananchi kufuata ushauri wa vyombo hivyo.

“Wakazi wanaoishi mabondeni wahame ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha,”alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi alisema zaidi ya kaya 100 zimekosa mahali pa kuishi baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao.

“Kaya mbili zilichelewa kutoka kwenye nyumba wanazoishi ikabidi tutafute Kikosi cha Zimamoto ambacho kilifika na kuwaokoa,”alisema.

Mgomi alisema mafuriko katika sehemu hiyo yanatokana na daraja dogo lililopo ambalo linashindwa kuhimili wingi wa maji.

Kufuatia tukio hilo, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, viongozi wa halmashauri, tarafa na kata walitarajiwa kukutana jioni kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kuwasaidia waliokumbwa na maafa.

“Tuone wadau wanatusaidiaje, tunapataje chakula lakini watu wa Msalaba Mwekundu wamefika na mablanketi na baadhi ya vifaa,” alisema.

#YALIYOJIRI>>>Walimu Walazwa UCHI na Kuchapwa Viboko.Fahamu zaidi hapa.

Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa Shule ya Msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.

Walimu hao wanakumbana na matukio ya ajabu ikiwamo kujikuta uchi, kupigwa fimbo na mtu asiyeonekana na kulazwa nje ya nyumba zao.

Mmoja wa walimu walioathirika na matukio hayo, Emmanuel Shaaban alisema yeye na familia yake hawana raha kutokana na matukio hayo kwa kuwa usiku huvuliwa nguo na kujikuta wamelazwa sehemu nyingine, huku wakiwa wamechanjwa kwa wembe mwili mzima.

“Tarehe 26 mwezi wa pili, siku ya Alhamisi sitaisahau kabisa. Ndiyo siku ambayo nilikatwa viwembe mwili mzima na hali yangu ilikuwa mbaya, niliishiwa nguvu na mwili ukawa na ganzi na nilipokwenda hospitali niliambiwa sina ugonjwa,” alisema Shaaban.

Alisema alipotoka hospitali alikwenda kijijini kwao mkoani Mwanza na huko aliendelea kuwa na hali mbaya kutokana na kuzimia mara kwa mara kwa sababu ya maumivu ya kichwa hadi alipotibiwa kienyeji.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Mbelwa alisema awali alikuwa akiona vituko usiku na mchana, lakini alivumilia huku akitunza siri bila kuwaeleza wenzake ili asiwakatishe tamaa.

Mbelwa alisema baadhi ya matukio aliyokutana nayo ni kuvuliwa nguo usiku, kulazwa eneo jingine, kuchapwa viboko, kumwagiwa damu kwenye korido ya nyumba, kuchanjwa kwa wembe, kuzungukwa na nyoka mwilini, kuona mtu na kisha anapotea na kutupwa kwenye mashimo.

Mzazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, Asha Kondo alikiri kuwapo kwa matukio ya watoto kuugua na kuanguka hadi uongozi wa kijiji ulipopeleka mganga wa kienyeji kutoa kinachodaiwa ni uchawi.

Mratibu wa Elimu wa Kata ya Marui, Damaru Charles alisema amekuwa akipokea malalamiko hayo na kuyawasilisha ngazi za juu.

Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa, Aurelia Rwenza alisema tatizo hilo linawapa shida walimu na kurudisha nyuma maendeleo ya elimu katika sehemu hiyo.

“Kwa kweli walimu wameathirika, hivi sasa tunatakiwa kuwajenga kisaikolojia,” alisema.

Saturday, 2 April 2016

#YALIYOJIRI>>>KHALI SI SHWARI KWA DAVID KAFULILA,MAHAKAMA YAMTAKA ALIPE FAINI KWA USUMBUFU.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayoendelea mjini Kigoma, imemtia hatiani David Kafulila na kumtaka kulipa gharama kutokana na kukiuka kanuni ya kuwasilisha hati za kiapo mahakamani, zikiwa zimethibitishwa kama Sheria ya Makosa ya Uchaguzi inavyoelekeza.

Hata hivyo, kiwango cha faini anachotakiwa kulipa hakikutajwa. Kosa hilo halikuzuia ushahidi wake kupokewa upya mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo aliyoifungua kupinga ushindi wa Hasna Mwilima (CCM) kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, Kafulila aliyegombea kwa tiketi ya NCCR Mageuzi analalamika kupokwa ushindi.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mwilima ambaye ni mshtakiwa namba moja wakati msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni washtakiwa namba mbili na tatu.

Jaji wa Mahakama Kuu, Ferdinand Wambali alisema Kafulila aliwekewa pingamizi na mawakili wa utetezi wakimlalamikia kuwasilisha hati ya kiapo iliyokiuka kanuni za uwasilishwaji kwa mujibu wa sheria.

Katika hoja yao mawakili hao waliiomba Mahakama hiyo kutozipokea hati hizo.

Jaji alisema Kafulila hakutekeleza matakwa ya kisheria ambayo yanaagiza anayewasilisha haki za viapo kuhakikisha kuwa zimethibitishwa kabla, kwa ajili ya shahidi kuanza kutoa ushahidi wake.

“Pingamizi la wajibu maombi linakubaliwa kwa upande mmoja, lakini pia linaachwa. Uamuzi wa Mahakama ni kwamba mleta maombi awasilishe upya hati za kiapo mbele ya Mahakama zikiwa zimethibitishwa,” alisema jaji.

“Lakini pia mleta maombi atalazimika kulipa gharama za usumbufu wa kesi kwa wajibu maombi kutokana na shauri kuahirishwa kwa siku mbili mahakamani.” Kufuatia mjadala huo kuwa mkali na mawakili wa kila upande kujenga hoja, jaji aliahirisha kesi hiyo

#YALIYOJIRI>>>CCM Yatoa Tamko Baada ya Wabunge Wake Kufikishwa Mahakamani Leo Kwa Tuhuma za Rushwa.Fahamu zaidi hapa.

Kwa kipindi cha hivi karibunin kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa.

Tuhuma hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya wabunge wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi  na kinaunga mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo.

Lazima ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi,dini, wala kabila na kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa.

CCM inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Chama cha mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Friday, 1 April 2016

#MICHEZO>>Ferguson – “Guardiola hawezi kufikia level ya Barcelona ndani ya EPL”.Fahamu zaidi hapa.

Msimu ujao kwenye EPL kutakua na moja ya kocha bora kwenye ligi za Ulaya naye ni Pep Guardiola akiiongoza club ya Manchester City.

Sir Alex Ferguson mwenye miaka 74 ameulizwa swali kuhusu ujio wa Pep ndani ya EPL. Majibu ya Pep yalikua kama hivi , Bila kujiuliza maswali mengi Pep ana ethics nzuri kwenye kazi yake, anafanya hivyo kwenye muda wa mazoezi hadi muda wa mechi. Yeyote anayedhani kwamba Pep atashindwa kwenye EPL basi inabidi abadirishe mawazo. Man City wamefanya kitu kizuri kumchukua kwenye timu yao. Lakini Pep hata kutana na vitu virahisi kwenye EPL, kila kocha anayetoka nje ya England lazima atakwambia ugumu wa EPL. Pep anaweza kufanikiwa ndani ya EPL lakini sidhani kama atafikia level ya mafanikio kama alivyokua na Barcelona, ile ilikua level nzuri sana na walikua vizuri

#MICHEZO>>>BARCELONA VS REAL MADRID: RONALDO NA MESSI WANAVYOLINGANA REKODI ZA EL CLASICO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mapumziko ya lili mbalimbali kupisha mechi za kimataifa yamemalizika, sasa wachezaji wanarejea kwenye vilabu vyao kuendelea na majukumu yao. Mwishoni mwa juma hili zitapigwa mechi kibao kutoka ligi za mataifa mbalimbali, lakini akili, macho na masikio ya dunia nzima ni juu ya mchezo wa Barcelona dhidi ya Real Madri ‘El Clasico’ mchezo wa ligi ya Hispani maarufu kama La Liga.

Barcelona wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa mbele ya Madrid kwa pinti 10 wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, mchezo huo utagubikwa na hisia juu ya kifo cha gwiji wa Barcelona Johan Cruyff aliyefariki juma lililopita na Barcelona wamepanga kutoa heshima zao kwa nyota huyo kwenye mchezo huo dhidi ya Madrid.

Siku hizi game ya El Clasico si vita kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona pekee bali na fursa kwa watu kuwalinganisha Cristinano Ronaldo na Lionel Messi ndani ya uwanja kutokana na upinzani wa ubora wa wachezaji hao nyota wa timu mbili tofauti.

Bila shaka hawa ndiyo wachezaji nyota kuwahikutokea katika vilabu hivi kuwa na upinzani mkubwa kwa wakati mmoja wakichezea vilabu vyao. Ni fursa nzuri ya kuwashuhudia Messi na Ronaldo wakicheza katika timu zenye upinzani mkubwa angalau mara mbili au zadi ndani ya msimu mmoja.

Ukweli ni kwamba, wawili hao wamepokezana tuzo ya Ballon d’Or katika kipindi cha miaka nane mfululizo.
Kuelekea mchezo wa El Clasico, ukilinganisha rekodi ya wachezaji hao kufunga magoli tangu Ronaldo alipojiunga na Madrid inafanana kwa kiasi kikubwa sana.

Ronaldo na Messi wanamagoli sawa wakiwa wacheza idadi sawa ya mechi, huku Messi akimzidi Ronaldo kwenye upande wa assists.
El Clasico tangu msimu wa 2009-10…
MESSI
24 idadi ya mechi alizocheza
15 idadi ya magoli aliyofunga
10 idadi ya assists alizotoa

CRISTIANO
24 idadi ya mechi alizocheza
15 idadi ya magoli aliyofunga
2 idadi ya assists alizotoa

Gazeti moja la Madrid linalofahamika kwa AS limelinganisha rekodi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi juu ya mchezo wa El Clasico, angalia ukurasa ma mbele wa gazeti hilo hapa chini.
AS linaripoti kwamba, hakuna mtu atakayebisha kwamba Ronaldo ni mchezaji wa mechi kubwa kwa mujibu wa takwimu walizozitoa.

Lakini kati ya michezo 24 ya El Clasico waliyokutana, Messi amefanikiwa kuisaidia Barcelona kushinda michezo 12, Ronaldo amefanya hivyo mara 6, huku michezo mingine 6 timu hizo zikitoka sare.

Ukichambua idadi ya magoli yao kwenye mchezo wa El Clasico, Ronaldo amefunga magoli 9 kwenye uwanja wa Nou Camp wakati Messi ametupia mara 10 akiwa Bernabeu. Hiyo inamaanisha wachezaji hao ni hatari kwenye mchezo huo bila kujali wapo kwenye uwanja gani.

#MICHEZO>>>Sababu 5 zinazoweza kumpeleka Messi Manchester City.Fahamu zaidi hapa.

Moja ya story ambayo inazungumziwa sana kipindi hiki ni tetesi za kwamba Messi anaweza kujiunga na kocha wake wa zamani kwenyue club ya Manchester City msimu ujao.
Hizi hapa ni sababu 5 ambazo zimechambuliwa kuonyesha uwezekano wa Messi kujiunga na Manchester City.

1)Guardiola connection
Pep anaweza kuwa kivutio kikubwa kwa Messi kwa sababu wamepata mafanikio makubwa wakiwa pamoja ndani ya Barcelona. Muda wote Pep amekua shabiki mkubwa wa Messi na anamuamini kiasi cha kumuacha afanye kile anachofikiria uwanjani bila maelekezo yake akiamini hawezi kumuangusha. Kila mchezaji angependa kuwa na kocha kama huyu.


2)Changamoto mpya
Messi ameshinda karibia kila taji ambalo anatakiwa kushinda akiwa na Barcelona. Kuanzia binafsi hadi ya ki-team, sasa kwa mtu ambaye anatafuta mafanikio mengine anaweza kuamua kwenda zake kutafuta changamoto mpya. Mfano kushinda taji la ligi ya England.


3)Muda muafaka Barca kumuuza Messi
Sasa hivi ana miaka 28 na ana thamani kubwa, baada ya miaka miachache ijayo lazima thamani yake itapungua na hawataweza kupata pesa nyingi kama wakimuuza sasa hivi. Wanatakiwa kumuuza na ku-focus kwa vipaji vyenye umri mdogo kama Neymar.


4)Kufata Pesa
Messi anaweza kuongeza mshahara wake kwa kiasi kikubwa sana kama akihamia Etihad. Wamiliki wa Man City watamuangalia Messi kama faida uwanjani na nje ya uwanja, hivyo basi mzigo watakaompa sio wa kitoto kama kawaida ya warabu kwenye pesa hawana noma.


5)Marafiki
Sergio Aguero na Messi ni marafiki wa karibu sana. Wamecheza pamoja wakiwa under 20 World Cup mwaka 2005 na pia wakashinda Gold Medal kwenye Olympic pamoja. Messi ni baba wa ubatizo wa mtoto wa Aguero kuonyesha kwamba hawa jamaa wapo karibu hadi kifamilia.


#YALIYOJIRI>>>MAKONDA ATANGAZA NEEMA KWA WAENDESHA BODABODA JIJINI DAR ES SALAAM.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza neema kwa waendesha bodaboda katika jiji la Dar es Salaam kwa kuwadhamini pikipiki kutoka kwa kampuni zinazofanya biashara hiyo.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana waendesha bodaboda kwa ajili ya kuboresha kazi hiyo katika kuwaletea maendeleo ya uchumi, amesema kuwa udhamini wa pikipiki kwa atakayekopeshwa kulipa sh.25,000 kila wiki na baadae kumiliki pikipiki hizo.

Makonda amesema umefika wakati wa vijana kumiliki pikipiki zao na sio kufanya biashara hiyo za watu ambao wanachukua fedha nyingi na wao kuendelea kuwa na maisha magumu.

Amesema tayari kampuni ameshapata ambayo itatoa pikipiki 5,000 kazi ya kuwadhamini haitakuwa ngumu kutokana kila atakayekopa lazima awe katika kituo kilichosajiliwa na kuwa na uongozi kamili.

Makonda amesema kuzuiwa kwa bodaboda mjini huku baadhi bodaboda zikifanya biashara hiyo inatokana na watumishi wachache kumiliki bodaboda hizo na kuwakingia kifua waendeshaji pindi wanapokamatwa.

Katika utatuzi wa changamoto  za waendesha bodaboda Makonda ameunda timu ya watu 13 itayofanya kazi miezi mitatu na kuweza kupata ufumbuzi na kazi hiyo ofisi yake itatoa sh.milioni moja kila mwezi katika kusaidia timu hiyo kushughulikia matatizo.

Katibu wa Kamati waendesha bodaboda, Daud Laurian amesema kuwa kuna chama cha kukopa na kulipa kilianzishwa lakini matokeo yake viongozi wamehujumu sh.milioni 50.

Amesema kuwa waendesha bodaboda wamekuwa wakilipishwa faini zisizo na kichwa ikiwa ni pamoja na kuibuka watu wengi kufanya kazi ya kuwakamata ikiwemo na matapeli.

Download nyimbo ya Yamoto band inayoitwa "nigande".Hapa hapa.


#YALIYOJIRI>>>Taarifa Rasmi Ya TAKUKURU Kuhusu Kumfikisha Mahakamani Mbunge wa Sumve, Richard Mganga Ndassa Kwa Tuhuma za Rushwa.Fahamu zaidi hapa.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imemfikisha Mahakamani Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji kwa kosa la kushawishi na kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a) na (2).

Akiwa kama mjumbe wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji tarehe 13/3/2016 Mhe. Ndassa alimwomba rushwa ya shilingi Milioni 30 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi J. Mramba ili amsaidie kuwashawishi wajumbe wengine wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji kupitisha bila kipingamizi taarifa ya TANESCO kwa mwaka 2015/2016.

Mbunge huyo amefunguliwa kesi namba 118/2016 na alisomewa mashtaka hayo na Wakili wa TAKUKURU Dennis Lekayo akishirikiana na Emmanuel Jacob katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kupata mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 10. Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na kesi hii itatajwa tena tarehe 18/4/2016.
 
IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
1 APRIL, 2016.

#YALIYOJIRI>>>Bosi wa Zamani wa TRA na Wafanyakazi wa StanBic Benki Wafikishwa Mahakamani.Fahamu zaidi hapa.

 Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (kati) sambamba na Waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari (kushoto) na Shose Sinare (kulia), wakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakisubiri kusomewa mashtaka yanayowakabili, leo Jijini Dar es salaam.
Habari zaidi endelea kufatilia hii blog:"hebronmalele.blogspot.com"

#YALIYOJIRI>>>China Yasema Uchaguzi wa Zanzibar Ulikuwa Huru na Wa Haki.....Yaahidi Kuendelea Kutoa Misaada na Kushirikiana na Tanzania.Fahamu zaidi hapa.

Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ofisini kwa Waziri huyo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Balozi wa China amesema kuwa Serikali ya China inaamini kwamba uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita ulikuwa huru na haki. 

Balozi Youqing amesema kuwa Makamu wa Rais wa China ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake na kwa watu wa Zanzibar kwa kuendesha uchaguzi huo katika misingi ya haki na uhuru. 

“Alikuwepo shuhuda wetu katika kushuhudia uchaguzi huo na alituambia kuwa ulikuwa wa haki na uhuru,” alisema Balozi huyo.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani huo ni wajibu wa mataifa makubwa kwa nchi zinazoendelea. 

Alimhakikishia Mheshimiwa Makamba kwamba China ina mipango mingi ya ushirikiano na Tanzania, ikiwemo kwenye sekta ya umeme na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania, ikiwemo kupitia makampuni ya China, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania kwenye sekta ya umeme yanatimia.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Makamba alimshukuru Balozi Youqing pamoja na Serikali ya China kwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

 “Ujumbe na salamu ulizotoa leo umetupa faraja Watanzania. Urafiki baina ya nchi zetu, na baina ya vyama vyetu vya CCM na CCP, ni wa muda mrefu, ni wa majira yote, na umejengwa kwenye misingi ya kuheshimiana na hauna budi kuendelezwa”, alisema Mheshimiwa Makamba.

Pia Waziri Makamba na Balozi Youqing walikubaliana kutembelea Pemba na Unguja kwa pamoja mwezi Aprili ili kukagua na kutengeneza miradi ya maendeleo kati ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile, walikubaliana kuhusu kutengeneza mradi mkubwa wa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na China kwenye teknolojia zitakazosaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuhifadhi mazingira.

Waziri Makamba pia amemueleza Balozi Youqing kuhusu hitaji na umuhimu wa ushirikiano katika kuiwezesha Tanzania kumiliki teknolojia ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia taka ngumu zinazozagaa katika miji ya Tanzania ambapo Balozi Youqing aliahidi kulifuatilia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

DIAMOND AKUTANA NA MKONGWE WA BOLINGO AWILO LONGOMBA NCHINI UFARANSA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mkongwe Awilo longomba alipo kutana na familiar nzima ya Diamond huko Paris ufaransa!!! Inasemekana kuna kitu kinafata...huenda ikawa collaboration

#YALIYOJIRI>>>Nchi 10 kati ya 14 za Ulaya zasitisha msaada wa kibajeti kwa Tanzania.Fahamu zaidi hapa.

Tanzania tutegemee kuingia kwenye shida ya kiuchumi. Wale washirika wetu wa maendeleo yaan zile nchi za ulaya. Kwa kauli ya pamoja wamesitisha misaada katika nchi yetu.
Tukumbuke misaada yao inaingia moja kwa moja kwenye bajet!! Wanaojua hatujitoshelezi. Kimaneno tunajitosheleza kwa 60% kivitendo hatuzid 40%.Ni zaid ya ile MCC. Maamuzi hayo yamekubaliwa na nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa ulaya.

Swali kwa watawala hata hizo milijua hamtapewa mlijiandaa kujitegemea?

Maana ya MCC nilimsikia msemaji wa wizara ya fedha anasema waljua haztakuja hawakuziweka kwenye bajeti.

Je na za washirika wa maendeleo hamkuziweka???

Wananchi mnatwambia tufunge mikanda suruali zetu zinavyotupwaya wakati nyie mnashindwa Hata kufunga vifungo vya makoti kwa vitambi.



Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.
Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani kuondoa msaada wa dola 472 wa kufadhili miradi ya maendeleo kutokana na jinsi uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar ulivyoendeshwa.

Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.

Chanzo: BBC Swahili

#YALIYOJIRI>>>Mkazi wa Mwananyamala Apandishwa Mahakamani Kwa Kutishia Kumuua Rais Magufuli Kwa Kujitoa Mhanga.Fahamu zaidi hapa.

Kondakta wa daladala, Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli kwa maneno.

Seif alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana mchana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kenneth Sekwao.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambaye atasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.

Licha ya dhamana yake hiyo kuwa wazi, mshtakiwa huyo alishindwa kukamilisha masharti hayo kwani baada ya kusomewa mashtaka alipoulizwa kama alikuwa na wadhamini alishindwa kuwapata.

Akimsomea shtaka linalomkabili, Wakili Sekwao alisema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, Makumbusho wilayani Kinondoni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (a) na kifungu cha 35 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.

Wakili Sekwao alisema akiwa katika baa hiyo, mshtakiwa alitishia kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga.

Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alisema Wakili Sekwao akimnukuu mshtakiwa huyo.

Hata hivyo, Wakili Sekwao alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

#YALIYOJIRI>>>EWURA Yashusha bei za Umeme kwa watumiaji wa Viwango tofauti Kuanzia Leo.....Service Charge Yafutwa Rasmi.Fahamu zaidi hapa.

Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.

Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa. 

Bei mpya  kwa watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni sh.292  toka  298  ya  zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka sh. 200  ya  hapo  awali.
Bei mpya  kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157 toka sh. 159. Wanaonunua kwa wingi (bulk) ni sh. 152  toka  sh. 156  ya  hapo awali

Tazama jedwali  hili  kuona mgawanyo  wa  bei  mpya.