MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza neema kwa waendesha
bodaboda katika jiji la Dar es Salaam kwa kuwadhamini pikipiki kutoka
kwa kampuni zinazofanya biashara hiyo.
Hayo
ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana waendesha bodaboda
kwa ajili ya kuboresha kazi hiyo katika kuwaletea maendeleo ya uchumi,
amesema kuwa udhamini wa pikipiki kwa atakayekopeshwa kulipa sh.25,000
kila wiki na baadae kumiliki pikipiki hizo.
Makonda
amesema umefika wakati wa vijana kumiliki pikipiki zao na sio kufanya
biashara hiyo za watu ambao wanachukua fedha nyingi na wao kuendelea
kuwa na maisha magumu.
Amesema
tayari kampuni ameshapata ambayo itatoa pikipiki 5,000 kazi ya
kuwadhamini haitakuwa ngumu kutokana kila atakayekopa lazima awe katika
kituo kilichosajiliwa na kuwa na uongozi kamili.
Makonda
amesema kuzuiwa kwa bodaboda mjini huku baadhi bodaboda zikifanya
biashara hiyo inatokana na watumishi wachache kumiliki bodaboda hizo na
kuwakingia kifua waendeshaji pindi wanapokamatwa.
Katika
utatuzi wa changamoto za waendesha bodaboda Makonda ameunda timu ya
watu 13 itayofanya kazi miezi mitatu na kuweza kupata ufumbuzi na kazi
hiyo ofisi yake itatoa sh.milioni moja kila mwezi katika kusaidia timu
hiyo kushughulikia matatizo.
Katibu
wa Kamati waendesha bodaboda, Daud Laurian amesema kuwa kuna chama cha
kukopa na kulipa kilianzishwa lakini matokeo yake viongozi wamehujumu
sh.milioni 50.
Amesema
kuwa waendesha bodaboda wamekuwa wakilipishwa faini zisizo na kichwa
ikiwa ni pamoja na kuibuka watu wengi kufanya kazi ya kuwakamata ikiwemo
na matapeli.
0 comments:
Post a Comment