Wakali hawa wa muziki wa Hip-Hop Tanzania wamejizolea mashabiki kila kona ya nchi na nnje ya mipaka ya Bongo kutokana na hits zao zilizonakshiwa kwa mashairi makali na styles za kila aina.Ukisikiliza nyimbo za Joh Makini way back from track ,Hawapendi,Zamu Yangu,Chochote Popote,Niaje ni Vipi,I see Me,Xo,Dont Bother na hits nyingine kibao,utadhibitisha kuwa JOH amefika hapo alipo kutokana na bidii,ubunifu uwezo aliouonesha kwenye kazi zake.
Speaking of Fareed Kubanda au Fid Q kama wengi wetu tunavyomfahamu,mbali ya kuwa miongoni mwa MCs wachache waliodumu kwenye game kwa muda mrefu tangu muziki wa kizazi kipya ulipoanza kupewa air time,hits zake kama,Mwaza-Mwanza,Agosti 13,Propaganda,Iam Proffesional,Siri ya Mchezo,Bongo HipHop,Walk it off na hits nyingine nyingi,utagundua kuwa Fid Q ni hazina ya mashairi kwenye muziki wa kizazi kipya nchini.
Kutokana na sifa za wanamuziki hawa kufanana kwa kiasi fulani,japo kila mmoja ana utofauti wake mashabiki wa muziki wamekua wakitamani rappers hawa wafanye kazi pamoja jambo ambalo bado mpaka leo halijafanyika.Kutokana na ushindani kisanaa baadhi ya mashabiki wamekua wakitafsiri baadhi ya lines kwenye nyimbo zao na kufanya upinzani kati ya wasanii hawa kwa mashabiki wao uzidi kuwa mkubwa.
Kwa mfano,kwenye wimbo wa Joh Makini f.t G-Nako unaofahamika kama “Bye Bye”,kuna line inayosema “Hizi kuandika hatucopy kwenye vitabu,shika lako ntakuaribu babu”,tafsiri ya mstari huu japo haimtaji moja kwa moja huyo mtu anaeandika kwa kunukuu vitabu,ila ni wazi kuwa hili ni dongo kwa wapinzani wake kisanaa.Speaking of Fid Q,kwenye hits yake inayofahamika kama “Propaganda” kuna mstari unaosema,”Chaajabu wanampa promo lakini kwenye show nammeza”,tafsiri ya line hii japo haimtaji moja kwa moja huyo anaepewa promo na kumezwa kwenye show,lakini mstari huu ni dongo kwa wapinzani wake kisanaa.
DIAMOND X ALLY KIBA.
Wakali hawa wa muziki wa bongofleva pengine upinzani wao ndio wenye nguvu zaidi zaidi nchini ukichagizwa na timu za mashabiki wao ambao wamekua wakitupiana maneno kwenye social media.wasanii hawa ambao wamewahi kuwa maswahiba na badae urafiki wao kugubikwa na sitofahamu nyingi,kila mmoja amekua akikanusha kuwa na ugomvi na mwenzake japo kisanaa wasanii hawa wanaonekana kuwa maji na mafuta.
SHILOLE X SNURA.
Wasanii hawa ambao wameingia kwenye mainstream ya Bongofleva wakitokea Bongo Movie,mara kadhaa wamkanusha kuwa na ugomvi japo wapambe wao wamekua wakitupiana maneno ya kashfa kwenye social media.Kinachonogesha ushindani wa wasanii hawa ni kutokana mahadhi ya kazi zao kufanana.Kama umepata bahati ya kuhudhuria show za wasanii hawa utaona ni kwa kiasi gani wao na dancers wao wanawapagawisha mashabiki kwa mitindo hatari ya unenguaji as we know wamebarikiwa maumbo ya kuvutia.
NICK WA PILI X NICK MBISHI.
The saga between Nick wa Pili na Nick mbishi started like northing was serious,ila baada ya Nick Mbishi kuachia ngoma inayofahamika kama “Harakati za MaPunch kwenye line”ambapo ndani yake kulikua na mstari kama “Kivipi nick wa pili…wa kwanza hajulikani”,huo ukawa mwanzo wa mashabiki kuanza kutengeneza ushindani kati ya rappers hao.Baadhi ya mashabiki waliohojiwa juu ya uwiano wa rappers hawa ambao wamejizolea mashabiki kutokana na uandishi na misimamo yao,wengi wao wanadhani kutoelewana kwa wasanii hawa chanzo chake kinaweza kuwa majina yao ya mwanzoni kufanana hasa ikizingatiwa kuwa Nick Mbishi ndie alietangulia kuingia kwenye mainstream kabla ya Nick wa Pili.
Speaking of Nick wa Pili,rapper huyu ambae ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye elimu ya juu na ushawishi kwa vijana,mara kadhaa amekanusha kuwa na ugomvi na msanii yeyote,ila alipohojiwa kwenye kipindi cha E-News cha Clouds Tv kama yupo tayari kufanya kazi na Nick Mbishi alijibu kuwa ni jambo linalowezekana ila inategemea kama wao wawili wataelewana.
YOUNG DEE X DOGO JANJA.
Upinzani kati ya rappres hawa wa new generation ya muziki wa kizazi kipya nchini,umeanza kushika kasi tangu Janjaro alipoachia hits yake inayofahamika kama “My Life” ambayo ndani yake kuna mstari unaosema “Kitambo mi nachana,zaidi ya wanyamwezi,mtaongea sana nyie ma young hamniwezi,mtazidi kupenga kisa stress mpaka totoro,nawanyima chakula mwaka huu mle magodoro”,japo Janjaro hamtaji huyo “anaepenga”(kutumia madawa ya kulevya),ila mstari huu umegeuka mwimba kwa mashabiki wa Paka rapper Young Dee,wakidai kuwa Dogo Janja anatafuta bifu na rapper huyo.
HITIMISHO.
Tunatambua kuwa kufanya kazi pamoja kwa wasanii hawa kunategemea maamuzi yao binafsi na management zao na sio ushawishi wa mashabiki wao,japo colabo hizi zinaweza kuwa na manufaa makubwa kibiashara hasa ukizingatia upinzani uliopo kati yao.Uchambuzi huu haugemei upande wowote ila umeakisi mitazamo na maoni ya mashabiki wa wasanii hawa.
Credit : Clouds FM & Clouds Tv.
0 comments:
Post a Comment