MKALI wa Muziki wa Hip Hop, Bongo Kheri Sameer ‘Mr Blue’
ameendelea kumporomoshea lawama Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Hip
Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuwa usumbufu aliokuwa anampa ili kuiachia
ngoma yake ya Freedom ulimsababishia ‘rabsha’ ndani ya ndoa yake.
Shutuma hizo anazozitoa Blue ni mwendelezo wa ‘drama’ inayoendelea
kati yake na Sugu ambayo kwa sasa ndiyo habari ya mjini kufuatia madai
ya Blue kuwa mheshimiwa huyo alimzunguka kwa kuuchukua wimbo wake huo
ambao mwanzo yeye alimshirikisha, akaurekodi upya huku akifuta mashairi
yake lakini kama haitoshi ‘akashuti’ video, jambo ambalo Blue analiona
kuwa ni uonevu.
“Kwanza Sugu alinisababishia
matatizo ndani ya ndoa yangu mpaka nikawa sipokei simu zake. Alikuwa
ananipigia simu kila muda na kila siku akiuliza ‘project’ inatoka lini
hadi mke wangu akawa anauliza kuna nini kati yetu.
Mwanzoni nilimweleza hali halisi lakini kwa namna Sugu
alivyokuwa ananisumbua ilifika hatua mke wangu akadhani kuna jambo
lingine tofauti, kukawepo na rabsha za hapa na pale lakini sasa nimeweka
mambo sawa,” alisema Blue.
Alipotafutwa Sugu kuhusu suala hilo, hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu lolote.
0 comments:
Post a Comment