Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>AZAM YATUPWA NJE MICHUANO YA AFRIKAFAHAMU ZAIDI HAPA.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani
Afrika Azan FC wametupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa
magoli 3-0 na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa
kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia.
Azam walikomaa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa
hawajaruhusu goli hata moja licha ya mashambulizi makali ya mara kwa
mara kufanywa kwenye goli lao lakini golikipa Aishi Manula alikuwa imara
kuondosha hatari zote na kuiweka Azam salama.
Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza
lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la pili
na Ben Yousef akaihakikishia timu yake kusonga mbele baada ya kufunga
bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika.
Benchi la ufundi la Azam chini ya Stewart Hall lilifanya mabadiliko
kujaribu kubadili matokeo kwa kuwapumzisha Farid Musa, Salum Abubakar
‘Sure Boy’na Wazir Salum huku nafasi zao zikichukuliwa na Hamisi Mcha,
Himid Mao na Didier Kavumbagu lakini bado mabadiliko hayo hayakumlipa
kocha huyo raia wa England.
Esperance imeitupa Azam nje ya mashindano kwa jumla ya magoli 4-2 baada
ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Azam ikiwa nyumbani ilishinda
kwa magoli 2-1 lakini leo imejikuta ikikubali kuchapwa magoli 3-0 ndani
ya dakika 32 na kuyaaga mashindano rasmi
Related Posts:
#BREAKING NEWS>>>>MANJI AJIUZURU YANGA…HAYA NDO MANENO YAKE.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Baada ya taarifa kwamba Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
amejiuzulu uenyekiti kuzagaa, SALEHJEMBE ilifanya kila juhudi kumpata
na mwenye akazungumza kwa ufupi.
Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia
ku… Read More
#MICHEZO>>>Usain Bolt ameandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo.Fahamu zaidi hapa.Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ameandikisha historia ya kuwa
mwanariadha wa kwanza kushinda nishani ya dhahabu kwa mara ya tatu
mfululizo, katika mbio za mita mia moja, kwenye michezo ya olimpiki ya
Rio 2016.
Bolt, … Read More
#MICHEZO>>>>Timu ya Simba Sasa Kuendeshwa Kwa Hisa..Mo Dewji Akabithiwa Timu.Fahamu zaidi hapa.
Kamati ya Utendaji ya Simba na mfanyabiashara, Mo Dewji leo wafikia makubaliano ya kuendesha Klabu ya Simba kwa mfumo wa hisa.
Hisa zitauzwa kwa wanachama wapya kwa taratibu mahususi, wanachama wa zamani watagawiwa hisa za… Read More
#MICHEZO>>>Mtangazaji Edo Kumwembe Aula Supersport..Apata Deal la Uchambuzi wa Soka.Fahamu zaidi hapa.
Mchambuzi Mahiri wa Michezo Edo Kumwembe apata deal nono ya kuwa
mchambuzi wa Kiswahili wa Supersport chini ya DSTV, Ameandika haya
katika ukurasa wake wa Facebook mara baada ya kusaini mkataba:
"DEAL DONE. Am happy k… Read More
#MICHEZO>>>>MEDEAMA YAITWANGA TP MAZEMBE, YANGA HAINA CHAKE KOMBE LA SHIRIKISHO.FAHAMU ZAIDI HAPA.
TP Mazembe imekubali kipigo cha mabao 3-2 ikiwa ugenini dhidi ya Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho, leo.
Ushindi
huo wa Medeama, maana yake imefikisha pointi 8 ambazo haziwezi kufikiwa
na Yanga huku Mazemb… Read More
0 comments:
Post a Comment