Mastaa
wengi wa Bongo wamekuwa wakiahidi vitu vingi kwa mashabiki wao lakini
vitu hivyo vinakuwa vinapotea hewani bila ya kutekelezeka.
‘Ahadi
ni deni’, watu wengi wanakuwa wanasahau maneno ambayo mwanzo waliyasema
wenyewe na bila hata ya kurudisha tena mrejesho kwa mashabiki wao juu
ya kauli zao za mwanzo walizozisema.
Baadhi
ya mastaa wameshaanza kupoteza uaminifu kwa mashabiki wao kutokana na
kuahidi kuja na vitu vingi lakini muda umezidi kwenda na mambo yanazidi
kubadilika huku kauli zao zikiwa hazitekelezwi.
Hawa ni baadhi ya mastaa walioshindwa kutekeleza ahadi zao kwa mashabiki wao.
Wema Sepetu
Ni mwaka mmoja takribani Madam atoe ahadi ya kuachia movie aliyofanya na staa wa movie kutoka Ghana, Van Vicker.
Ni
kweli kuna kipindi Sepetunga hakuwepo nchini kwa muda kidogo na alidai
kuwa anaenda kushoot movie yake na staa huyo wa Ghana. Aliwahi kusema
alifanya connection na Van Vicker kupitia Instagram. Movie hiyo hadi leo
haijatoka.
Naamini
hiyo movie siku ikitoka inaweza ikaweka rekodi ya kuwa movie ya kwanza
kuuza kwa soko la ndani kutokana na umaarufu waliokuwa nao Madam Wema na
Van Vicker, lakini pia itamfanya Wema kutanua soko lake nchi za Afrika
Magharibi.
Muda bado upo ngoja tuendelee kusubiri japo wengi wamechoka kuisubiria na tayari wameshakata tamaa juu ya ujio wa hiyo movie.
Alikiba
Unakumbuka
kauli ya kuwa kuna nyimbo ya Alikiba na Davido inakuja? Ni muda mrefu
tangu hilo limezungumzwa lakini bado mpaka leo halijatimia.
‘Lisemwalo
lipo na kama halipo basi laja’ lakini pia waswahili wanasema kuwa
‘ngoja ngoja yaumiza matumbo’, tutasubiri mpaka lini?
Alikiba
amezidi kuachia nyimbo nyingine kama ‘Nagharamia’ na ‘Lupela’ huku
mashabiki wakiwa na hamu ya kuisikiliza nyimbo aliyoimba na Davido
ambayo tunategemea utakuwa ni muziki mzuri ambao utazidi kuutangaza
muziki wa Bongo Fleva nje ya mipaka ya Tanzania.
Idris Sultan
Ukiwataja
wasanii wasomi kwenye Bongo Fleva, hutaacha kulitaja jina la Nick wa
Pili lakini pia ni miongoni kati ya wasanii wachache wanao hit na nyimbo
zao kadhaa bila kuwa na video kama ‘Safari’ na ‘Baba Swalehe’.
‘Baba
Swalehe’ ni wimbo wa Nick ambao bado unafanya vizuri tangu siku ya
kwanza ilipoachiwa kwenye redio. Ingawa ni miezi mingi imepita tangu
wimbo huo utoke Novemba mwaka jana, bado Nick hajaachia video yake.
Aliwahi
kudai kuwa angeachia video yake baada ya G-Nako kuachia wimbo wake mpya
na sasa ni miezi kadhaa tayari imeshapita tangu G-Nako aachie Original
lakini video ya Baba Swalehe haipo.
Barnaba ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo Fleva waliobarikiwa kuwa na vipaji vingi kwenye muziki.
Mwaka
jana mwishoni Barnaba aliachia wimbo aliomshirikisha staa kutoka nchini
Uganda, Chameleone. Baada ya kuachia wimbo huo ‘Nakutunza’ Barnaba
alitoa ahadi ya kuachia video ya wimbo huo baada ya miezi miwili lakini
mpaka sasa imepita miezi mitano na siku kadhaa tangu ameachia wimbo huo
na bado video yake haijaonekana.
‘Nakutunza’
ni wimbo ambao umewakutanisha mafundi wa muziki na hakika huwezi
kuchoka kuusikiliza. Mpaka sasa mashabiki wameshatengeneza script zao
vichwani kwaajili ya v
Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan anaingia kwenye orodha ya mastaa walioshindwa kutekeleza ahadi zao.
Ni
takribani miaka miwili tangu atangazwe kuwa mshindi wa BBA, baada ya
muda Idris aliahidi kuja na reality TV show ambayo alisema amepanga
itakuwa inaonyeshwa kwenye kituo cha BET.
Haijulikani
iwapo ndoto hizo za kuja na Reality Show zimepotea au bado mipango ipo
vile vile. Ni kitu kizuri ambacho alikifikiria Idris na kingeweza
kumuongezea umaarufu zaidi na kumpa deals kibao za kuingiza pesa kwa
kuwa kingeweza kuonekana dunia nzima.
Barnaba
chanzo na Bongo5
0 comments:
Post a Comment