Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Vipaza Sauti Vya Bunge Vyaharibika, Bunge Lasimama kwa Dakika 30.Fahamu zaidi hapa.

Shughuli
za Bunge la Muungano leo zilisimama kwa dakika 36 kabla ya kuendelea
tena, baada ya vipasa sauti vya ukumbini kushindwa kufanya kazi.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai amelazimika kuahirisha shughuli mara baada ya
kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu ambacho hata hivyo
wabunge walichukua muda mrefu kuuliza maswali kutokana na kuhama hama
wakitafuta mahali pa kusikika.
Awali, wabunge waliokuwa na nafasi
ya kuuliza maswali walilazimka kuhama maeneo yao na kuzua minong’ono
ndani ya ukumbi, huku Mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega na Mbunge
wa Manonga (CCM), Seif Gulamali wakilazimika kuuliza maswali yao wakiwa
uso kwa uso na Waziri Mkuu mbele ya ukumbi.
Hata hivyo, kuna
hali ya sintofahamu, kwani vipaza sauti vimeharibika ikiwa ukumbi huo
umefanya kazi kwa siku sita tu tangu ulipokabidhiwa baada ya ukarabati
mkubwa.
April 18, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson
alikabidhiwa ukumbi huo ikielezwa kuwa ulikuwa umefanyiwa matengenezo
makubwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuuboresha.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>Maalim Seif Arejea Zanzibar Akitokea India Kwenye Matibabu,Mamia ya Wafuasi wake Wampokea, Asema Polisi Imegeuka tawi la CCM.Fahamu zaidi hapa.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana aliwasili Zanzibar
kutoka ughaibuni na kulilaumu Jeshi la Polisi nchini akisema, “hapana
shaka yoyote sasa limegeuka tawi la CCM.”
Maalim Seif alisema
hayo jana … Read More
#BREAKING NEWS>>>KIJANA APONA KIFO BAADA KUKIMBILIA KITUO CHA POLISI MAENEO YA MABIBO MWISHO DAR-ES-SALAAM.FAHAMU ZAIDI HAPA..
Hili kundi ambalo lilikuwa linamkimbiza kwa mawe.
Kijana ambae bado jina lake sijalipata kwa amepona kwa kuitiwa mwizi,kwa muji wa watu ambao nimewauliza na kusema huyo kijana ambae walikuwa wanamkimbiza hakuwa mwizi bali… Read More
#YALIYOJIRI>>>SIKU chache baada ya kusambaa kwa picha yake inayomuonesha akiwa amepungua mwili na kuzua mjadala mitandaoni huku wengi wakimuonea huruma, mkongwe wa Muziki wa Takeu, Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ ameibuka na kufungukia afya yake.Fahamu zaidi hapa.
Picha inayomuonesha Nice akiwa amepungua mwili ilizagaa mapema wiki
hii kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliochangia mjadala wa
picha hiyo, walisema staa huyo aliyetikisa kwa utajiri enzi hizo, kwa
sasa atakuwa a… Read More
#YALIYOJIRI>>>Msanii mkongwe Joseph Haule ambae ni mbunge wa Mikumi ametoa msaada wa mabati katika shule ya msingi Mamoyo.Fahamu zaidi hapa.
Msanii mkongwe wa miondoko ya hip hop Joseph Haule ambae ni mbunge wa Mikumi ametoa msaada wa mabati katika shule ya msingi Mamoyo iliyopo katika kata ya Mabwerebwere.
… Read More
#YALIYOJIRI>>>Madiwani wa UKAWA Wavamia Ofisi ya Halmashauri ya Jiji La Dar Wakitaka Kuelezwa ni Lini Uchaguzi wa Meya Utafanyika.Fahamu zaidi hapa.
Zaidi ya madiwani 20 wanaotokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), jana walivamia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es
Salaam kumshinikiza Kaimu Mkurugenzi wake, Sarah Yohana kuitisha Baraza
la… Read More
0 comments:
Post a Comment