DK.
Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria, amesema kuwa Tanzania
ni bora iendelee kutaabika na watanzania wafe wakiwa masikini kuliko
kuendelea kunyanyaswa na mataifa ya ulaya.
Mwakyembe
ambaye hata hivyo hakuyataja mataifa hayo lakini moja kwa moja
ilionekana kuyagusa baadhi ya mataifa ya Ulaya pamoja na Serikali ya
Marekani iliyovunja uhusiano na Serikali ya Tanzania katika mambo yote
yanayohusu miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na mfuko wa changamoto za
millenia (MCC).
Mwakyembe
ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wizara ya katiba
na sheria jijini hapa, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi kwa
mkoa wa Mwanza.
Mwakyembe
ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, amesema kuwa
anashangazwa na baadhi ya watu wanaotaka kuliingiza taifa katika mambo
mabaya yasiofaa na yalioko kinyume na maadili ya watanzania.
Amesema
mataifa hayo yamekuwa yakionekana kuilazimisha Tanzania kuingia katika
mambo yasiyokubalika na watanzania wenyewe ikiwemo suala la `ushoga`
kitendo ambacho alidai ni cha hovyo.
“Ni
bora tufe masikini kuliko kuendeshwa kwa hofu, wao wanataka watuendeshe
tu, sisi vitu kama vya ushoga vinapaswa kupingwa vibaya na haiwezekani
kabisa.
“Vitu kama vya ushoga ni vya hovyo na kama watanzania hatukubaliani navyo, hata maadili yetu yenyewe hayataki mambo kama hayo,” amesema Mwakyembe.
Machi
29 mwaka huu, Serikali ya marekani kupitia kwa bodi ya wakurugenzi wa
MCC ilitangaza uamuzi wa kuinyima Serikali Dora za kimarekani Milioni
472.8 ( zaidi ya Sh. Trioni 1 na bilioni 20) kutokana na marudio ya
uchaguzi wa serikali ya Zanzibar na sheria ya makosa ya mtandao.
Hata hivyo, Marekani kupitia kwa balozi wao hapa nchini Mark
Childress, jana ilionyesha kulegeza msimamo wao ambapo walisema
wataendelea kuisaidia Tanzania hasa katika sekta ya Afya na Elimu
licha ya changamoto za kisiasa zilizopo
Mahakimu mizigo kukiona
Katika
hatua nyingine Waziri Mwakyembe, amesema kuwa ofisi yake tayari
imekwishaunda kamati za madili za Mahakama, ili kudhibiti baadhi ya
mahakimu wanaofanya kazi kwa mazoea na kutokufata maadili.
Amesema
kuwa kuundwa kwa kamati hiyo, kutasaidia watu kufanya kazi kwa
kuzingatia weledi wa fani hiyo muhimu nchini kwani kuna baadhi ya
mahakimu walevi wasiofuata maadili ya kisheria.
“Tuna
taarifa wapo baadhi ya mahakimu ambao ni walevi na wengine wanafikia
hatua ya kupewa msaada baada ya kuzidiwa na pombe lakini sasa kesho
unashangaa huyo hakimu anakuja na yeye kutoa uamzi,” amesema Mwakyembe.
Amesema
kuwa lengo jingene la kuunda kamati hiyo ni kutaka kurekebisha baadhi
ya tabia za mahakimu wakiwemo wa Mahakama za mwanzo kutenda haki kwa
Wananchi wote bila kumpendelea mtu.
0 comments:
Post a Comment