Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>RONALDO AKIMBIA UWANJA MADRID IKIICHAPA VILLAREAL 3-0.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Real Madrid imeshinda mchezo wake wa Jumatano usiku dhidi ya
Villareal kwenye uwanja wake wa Bernabeu na kuweka hai matumaini yao
kwenye mbio za taji la La Liga.
Mashaiki wa Madrid walimshuhudia star wa timu yao Cristiano Ronaldo
akitoka nje ya uwanja kutokana na maumivu ya nyama za paja kabla ya
mechi kumalizika.
Chakushangaza ni kwamba, Ronaldo aliondoka uwanjani wakati mchezo
unaendelea bila kumwambia mtu yeyote, Ronaldo alipitiliza moja kwa moja
hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa zimesalia dakika chache
mchezo kumalizika.
Wapenzi wa Madrid bado wanamatumaini wakiamini nyota wao hana tatizo
kubwa, na ilikuwa ni presha katika kuwania tuzo ya Pichichi kwa nyota
huyo ambaye hakufunga goli kwenye mchezo huo huku mpinzani wake Suarez
akimsogelea kwa tofauti ya bao moja baada ya kutupia bao nne na
kufikisha magoli 30 goli moja nyuma ya Ronaldo.
Mashabiki wa Manchester City kwa upande mwingine watakuwa wakimwombea
mabaya Ronaldo ili timu yao itakapokutana na Madrid kwenye nusu fainali
ya Champions League wiki ijayo asiwepo uwanjani.
Ronaldo aliisaidia Madrid kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya
mabingwa Ulaya baada ya kupiga hat-trick kwenye mchezo wa marudiano
dhidi ya Wolfsburg, madaktari wa Madrid watakuwa wanafanya kila njia
kuhakikisha star wao anarejea uwanjani mapema iwezekanavyo.
Related Posts:
Simba Wamuacha Asante Kwasi.
KIKOSI cha Simba kimewasili salama jijini Mwanza asubuhi kwa ndege tayari kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao Mwadui FC huku wakimuacha beki wao kiraka Mghana, Asante Kwasi.
Simba inatarajiwa kuvaana na Mwadui kesho Alha… Read More
Ngoma, Yanga Mambo Safi Wamalizana.
SIKU chache baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kutamka hatua yao ya kufikiria kuvunja mkataba na mshambuliaji wake, Donald Ngoma, kufuatia majeraha sugu, suala hilo sasa halipo, imeelezwa.Ngoma, ambaye anaendelea kuuguza ma… Read More
Kibaka Amuingiza Mjini Pluijm Wamuibia Mkoba wa Fedha.
MUDA mchache baada ya kushuhudia timu yake ikipata bao la pekee katika
dakika za nyongeza dhidi ya Tanzania Prisons juzi, Kocha wa Singida
United, Hans van der Pluijm, alijikuta akiingizwa mjini na vibaka kwa
kuibiwa mko… Read More
Mwamuzi Jonesia Rukyaa Ameteuliwa Kuchezesha Michuano ya Algarve Nchini Ureno.
Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limesema kuwa mwamuzi wa kike nchini mwenye beji ya Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA), Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuchezesha mchezo wa michuano ya Algarve kwa mwaka huu nchini Ur… Read More
Simba, Yanga Kumaliza Vipolo Vyao Kabla ya Kusafiri kwa Mechi za Kimataifa.
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC iliyopo kileleni mwa msimamo na mabingwa watetezi Yanga SC iliyopo nafasi ya pili zinatarajiwa kucheza mechi zao za viporo za VPL kabla ya kusafiri kwa mechi za kimataifa.Yanga… Read More
0 comments:
Post a Comment