Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya
Tanzania Bara.
Taarifa
iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza
kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo
vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.
Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1.Arusha - Richard Kwitega
2.Geita - Selestine Muhochi Gesimba
3.Kagera - Armatus C. Msole
4.Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
5.Pwani - Zuberi Mhina Samataba
6.Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
7.Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
8.Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
9.Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
10.Tanga - Eng. Zena Said
Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;
1.Kigoma - Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
2.Morogoro - Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)
Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;
1.Dar es salaam - Theresia Louis Mbando
2.Dodoma - Rehema Hussein Madenge
3. Iringa - Wamoja Ayubu Dickolagwa
4.Katavi - CP Paul Chagonja
5.Lindi - Ramadhan Habibu Kaswa
6.Mara - Benedict Richard Ole Kuyan
7.Manyara - Eliakimu Chacha Maswi
8.Mbeya- Mariam Amri Mjunguja
9.Mtwara - Alfred Cosmas Luanda
10.Mwanza - CP. Clodwing Mathew Mtweve
11.Njombe - Jackson Lesika Saitabau
12.Rukwa - Symthies Emmanuel Pangisa
13.Ruvuma - Hassan Mpali Bendeyeko
Makatibu
Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa
siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini
Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Aprili, 2016
0 comments:
Post a Comment