Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale
*******TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, imebaini kuwepo kwa watumishi hewa zaidi ya watano ambao uongozi wa mkoa huo haukuyawasilisha majina yao kwa Rais Dk. John Magufuli huku yakionekana kukopa fedha benki.
Pia
Takukuru imesema kuwa majina ya watumishi hewa hao baada ya kufanya
uchunguzi wamebaini hukopeshwa fedha kwa kisingizio kwamba wao ni
watumishi wa Serikali kitendo ambacho ni cha uongo.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale wakati
akitoa taarifa ya robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu,
ambako alisema majina yaliowasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa huo, John
Mongella sio kamilifu.
Amesema
watumishi hao hewa wamekuwa wakikopa fedha kutoka benki mbalimbali kwa
kutumia nyaraka za kughushi jambo ambalo alidai kwamba kuna baadhi ya
watumishi wasio waaminifu wanaohusika kufanya udanganyifu huo.
Amesema
pia katika uchunguzi wao unaonesha kuwa majina ya watumishi
yaliowasilishwa na baadhi ya halmashauri za mkoa huo sio kamilifu kwani
kuna watumishi wengine ambao hawajaorodheshwa.
Makale
amesema kuwa kutokana na kuonekana kwa hali hiyo Takukuru inaendelea
kufanya uchunguzi wa kina kuwabaini watumishi hewa wengine na watumishi
wengine wanaoshirikiana nao.
“Kuna
dalili za wazi ambazo zinaonesha kuna watumishi wasiokuwa waaminifu wa
halmashauli ambao wanahusika kufanya vitendo hivi vya udanganyifu,
atakaebainika atafikishwa mahakamani,” amesema Makale.
Watumishi wadakwa kwa utapeli
Makale
pia amesema kuwa Takukuru Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha miezi hiyo
tayari imewakamata aliyekuwa Meya wa Ilemela, Henry Matata, Justine
Lukaza (Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela) na Mfanyabiashara, Hemed Hamad
kwa kosa la kutoa zabuni feki ya kutoza ushuru kwenye stendi ya mabasi
ya Buzuruga jijini hapa.
Watumishi
wengine waliokamatwa kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao ni
pamoja na aliyekuwa Mganga wa Wilaya ya Magu, Patrick Mwindunga, Afisa
Ugavi wa Wilaya ya Misungwi, Zabron Marwa, anaetuhumiwa kuingia manunuzi
feki.
Wengine
ni wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Masalu Kangalukwi na
Amon Shija wanaotuhumiwa kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa.
TAMISEMI yaongoza kwa Rushwa
Katika
taarifa hiyo, Mhandisi Makale amebainisha kuwa Takukuru imepokea jumla
ya malalamiko 45 yanayohusiana na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi
ambapo katika malalamiko hayo, 27 yameelekezwa kwa watumishi wa idara
za Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 60. Kati
ya malalamiko hayo 27, malalamiko 13 yameelekezwa katika idara ya ardhi.Amesema idara zinazofuata kwa kulalamikiwa ni Mahakama yenye malalamiko tisa, polisi malalamiko sita na idara ya afya malalamiko matatu.
Mhandisi Makale amesema kesi 33 zinaendelea Mahakamani kutokana na vitendo vya rushwa Mkoani Mwanza huku kesi sita zikiwa ni mpya katika kipindi cha miezi mitatu na nyingine zikiwa katika upelelezi.
0 comments:
Post a Comment