Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>YANGA YAREJEA KILELENI VPL.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Yanga imerejea kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada
ya kuifunga mtibwa Sugar kwa goli 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye
uwanja wa taifa. Yanga ilienguliwa kileleni mwa ligi na mahasimu wao
Simba takribani mwezi mmoja ulipita lakini wamerejea kwenye nafasi yao
kufuatia kushinda mechi zao za viporo.
Bao pekee la ushindi limefungwa na Simon Msuva dakika ya 48 kipindi
cha pili kwa kiki ya chinichini aliyoiachia akiwa nje ya eneo la hatari
na kumshinda mlinda mlango wa Mtibwa Sugar Said Mohamed.
Licha ya kupata ushindi huo, Yanga ilipoteza nafasi nyingi za kupata
magoli mengi zaidi kutokana na ubora wa golikipa Said Mohamed ambeye leo
alikuwa kwenye kiwango bora na kuokoa michomo kadhaa ya washambuliaji
wa Yanga.
Unachotakiwa kujua:
- Ushindi wa Yanga dhidi ya Mtibwa unaifanya timu hiyo kufikisha
pointi 59 na kukaa kileleni mwa ligi kwa pointi 2 zaidi ya Simba ambayo
inashuka hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 57 lakini timu hizo
zikiwa zimecheza mechi 24.
- Yanga imeishinda Mtibwa Sugar katika game zote mbili za ligi kwa
mara ya kwanza baada ya kufanya hivyo kwa mara ya mwisho msimu wa
2008/09.
- Yanga imeifunga Mtibwa jumla ya magoli matatu msimu huu na kuondoka na pointi zote sita baada ya michezo miwili.
- Simon Msuva ameifungia Yanga magoli mawili katika mechi mbili
mfululizo. Alifunga goli la kwanza kwenye mchezo wa Yanga vs Mwadui
Jumatano walipopata ushindi wa magoli 2-1 lakini mchezo dhidi ya Mtibwa
amefunga goli pekee.
Related Posts:
#MICHEZO>>>>Bale Akodi kisiwa cha karibu billioni 2 kumchumbia demu wake.Fahamu zaidi hapa.Gareth Bale alikodi kisiwa cha Tagomago, kilichopo karibu na Ibiza ili kufanya shughuli ya kumposa mchumba wake Emma Rhys-Jones.
Kwa
mujibu wa ripoti mchezaji huyo wa Real Madrid alikikodi kisiwa hicho
Tagomago, ambapo al… Read More
#MICHEZO>>>KAULI YA WAZIRI NAPE KUHUSIANA NA MABADILIKO YA SIMBA HII HAPA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameweka wazi
anachoamini ni bora katika mabadiliko yaliyofanywa na wanachama wa
kalabu ya Simba.
Wanachama
wa klabu ya Simba wamepitisha kwa pamoja kuwa… Read More
#MICHEZO>>>>KAZI IPO, MANJI AWAITA WANACHAMA WA YANGA JUMAMOSI, WANAKUTANA DIAMOND JUBILEE.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Wanachama wa Yanga, watakutana Jumamosi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Ukumbi huo, Juzi Jumapili wanachama wa Simba walipitisha uamuzi wa klabu yao kuacha mchakato wa kuwa kampuni.
Wanacham… Read More
#MICHEZO>>>>JOHN OBI MIKEL ABADILI JINA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
John Obi Mikel ameamua kubalisha jina lake. Jina lake halisi alikuwa
anaitwa Michael John Obi, lakini Shirikisho la Soka nchini Nigeria kwa
bahati mbaya walikosea herufi wakati wakimwandikisha jina lake katika
kikosi c… Read More
#MICHEZO>>>EXCLUSIVE: MO DEWJI AANZA KAZI, AMWAGA SH MILIONI MIA ZA USAJILI SIMBA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Mkurugenzi Mtendaji na rais wa makapumni ya Mohammed Enterprises Ltd
(MeTL Group) Mohammed Dewji ‘MO’ ametoa kiasi cha shilingi milioni 100
kwa klabu ya Simba kwa ajili ya kusaidia zoezi la usajili kama
alivyoahidi siku … Read More
0 comments:
Post a Comment