Home »
Habari Moto
» #BREAKING NEWS>>>MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na
wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo,Japhery
Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa
barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya
ujenzi, Mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za
kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya
kiwango.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa
hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja
maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na
Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi
unaoendelea.
Kuyeko alisema kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada
ya manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa
ujenzi wa barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo.
Alisema baada ya kuingia madarakani kwa miezi mitatu walijaribu kutafuta
kero ndani ya manispaa ya Ilala ambapo walibaini idara ya ujenzi ina
malalamiko mengi kutoka kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa sababu ya
kusimamia ujenzi wa barabara chini ya kiwango na hakuna hatua stahiki
zilizochukuliwa na maofisa hao.
Alisema madiwani hao walimlalamikia Mhandisi Bwigane kuwa amekuwa
akikaidi wito wao wa kujadili ujenzi wa barabara mbovu pindi
zinapobainika jambo ambalo limesababisha manispaa hiyo kuwa na barabara
nyingi mbovu.
Jitihada za gazeti hili za kumtafuta Mhandisi Bwigane ili kuzungumzia
kusimamishwa kwake kazi hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake na
wakati wote kuwa imefungwa
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>Askari tisa JWTZ kizimbani kwa mauaji.Fahamu zaidi hapa.
ASKARI
tisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamefikishwa mahakamani
wakituhumiwa kwa mauaji ya mkazi mmoja wa Kata ya Chemchem Manispaa ya
Tabora.
Mwendesha
Mashtaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi… Read More
#YALIYOJIRI>>>>TCRA Yadai Haipendi Kufungia vyombo vya Habari ila Sheria Inawalazimu.Fahamu zaidi hapa.
Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania, TCRA, imesema haifurahii kuvifungia
vyombo vya habari bali inavitaka vifuate kanuni na sheria zilizopo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda, ameyasema hayo a… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Tundu Lissu Aponea Chupuchupu Dhamana Yake Kufutwa.Fahamu zaidi hapa.
Hofu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumfutia dhamana Tundu Lissu
ambaye ni mtuhumiwa wa kesi ya uchochezi, imetoweka baada ya mahakama
hiyo kukubaliana na utetezi wa wadhamini wake kuwa, Lissu yupo
Ujerumani k… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Majina ya waliofariki katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem na Hiace jijini Mwanza.Fahamu zaidi hapa.
WATU
13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem lenye
namba za usajili T 874 CWE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza na
Hiace yenye namba T 368 CWQ iliyokuwa ikitoka Jijini Mwanza kuelekea
… Read More
#YALIYOJIRI>>>Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPFi na kuvunja Bodi yote.Fahamu zaidi hapa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
21 Septemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya
Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof. Hasa Mlawa kuanzia leo.
Pamoja na… Read More
0 comments:
Post a Comment