Thursday, 21 April 2016

BREAKING NEWS>>>Okwi arudi Msimbazi, Kiiza out.Fahamu zaidi hapa.

Straika Mganda, Emmanuel Okwi yupo njiani kurejea Msimbazi kwa mara nyingine.

Straika huyo anayependwa na mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kutokana na mchango wake mkubwa, kwa sasa anacheza soka la kulipwa Denmark katika klabu ya Sonderjyske, akishindwa kutamba na mabosi wa Msimbazi wanajiandaa kumrejesha.

HII inaweza kuwa taarifa nzuri kwa mashabiki wa Simba, lakini ni mbaya kwa wale wa Jangwani, baada ya kufahamika kuwa straika Mganda, Emmanuel Okwi yupo njiani kurejea Msimbazi kwa mara nyingine.


Straika huyo anayependwa na mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kutokana na mchango wake mkubwa, kwa sasa anacheza soka la kulipwa Denmark katika klabu ya Sonderjyske, akishindwa kutamba na mabosi wa Msimbazi wanajiandaa kumrejesha.


Hata hivyo ujio wa Okwi utafungua milango kwa Hamis Kiiza ‘Diego’ kuondoka Msimbazi kulingana na mipango iliyoanza kusukwa na mabosi wa klabu hiyo.


Ipo hivi. Viongozi wa Simba sasa wanajipanga kwa mambo mawili, moja ni kupigana hadi hatua ya mwisho kwenye ubingwa wa Ligi Kuu Bara na pili ni kusuka kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao na tayari Okwi yupo kwenye mipango yao kwa asilimia 90.


Simba ilimuuza Okwi kwa dau la Dola 110,000 kwenda Sonderjyske ya Dermark ambako inaonyesha soka la nchini humo limemkataa na hivyo klabu yake imeitaka Simba imnunue Mganda huyo na mabosi hao wamekubali kwa roho moja.
Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa mmoja wa mabosi wa timu hiyo yupo tayari kutoa fedha hizo ili Okwi arejeshwe Msimbazi, lakini ikielezwa kuwa ni lazima Kiiza aondoke kwa kuwa Simba inataka kubaki na Mganda mmoja tu.


Kiiza ndiye mfungaji bora wa Simba msimu huu akiongoza pia orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu akiwa na mabao 19, lakini atalazimika kumpisha Okwi endapo dili hilo litakamilika huku nafasi ya Raphael Kiongera ambaye mkataba wake unamalizika ikizibwa na Laudit Mavugo raia wa Burundi.


Mavugo amethibitisha kujiandaa kutua Msimbazi kwa kutumia mkataba waliosaini awali mwaka jana, lakini dili likafa baada ya klabu yake ya Vital’O kuweka kauzibe ikitaka dau kubwa la uhamisho.


“Nakuja kama mchezaji huru, kuna mambo yatawekwa sawa, ila uhakika naja,” alisema Mavugo.


Mavugo alishindwa kujiunga na Simba baada ya viongozi wake kuongeza dau na kuitaka Simba itoe Dola 100,000 jambo ambalo lilikuwa gumu kwa kile kilichoelezwa kuwa kiwango cha straika huyo hakiendani na fedha hizo.


MSISITIZO
Habari kutoka ndani ya Simba, zinaeleza kuwa miongoni mwa mapendekezo ya awali ya kocha wao Jackson Mayanja ni kwamba Simba mpya isiwe na sura nyingi za wachezaji kutoka Uganda hivyo hata beki Juuko Murshid naye yupo kwenye mipango ya kuuzwa katika moja ya timu nchini Lebanon


0 comments:

Post a Comment