Mbunge
wa Ulanga, Gudluck Mlinga (CCM), amesema Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo
Pinda, alitaka kuchomokea dirishani baada ya kutoswa katika uteuzi wa
urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
jana.
Mlinga
ambaye pia ni mtoto wa marehemu, Selina Kombani, alitoa kauli hiyo juzi
jioni, wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alisema
baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia upinzani na
wenzake, Pinda naye alitaka kuwafuata, lakini akashtuka na kubaki CCM.
“Yule
mwingine alituzingua tukampiga chini akaenda upinzani, Pinda naye mwaka
jana alitetereka, tukamtosa akataka kuchomokea dirishani… akashtukia
akabaki, kwahiyo CCM hatufanyi mambo kwa kuambiwa kama wanavyofanya
upinzani,” alisema.
Kauli ya Mlinga ilionekana kumkera Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM) ambaye aliomba kutoa taarifa: “Mheshimiwa
mwenyekiti nampa taarifa mzungumzaji, amemvunjia heshima Pinda kwa
kusema alitokea dirishani, afute kauli yake mara moja au athibitishe ni
lini Pinda alitokea dirishani… mtoto huna adabu, huna nidhamu,” alisema Keissy huku akishangiliwa na wabunge wa upinzani.
Baada ya taarifa ya Keissy, mwenyekiti akamtaka Mlinda kuendelea kuchangia na kujikita kwenye hoja.
“Pamoja
na umbile langu ndogo, leo nipo hapa kuwapa semina wabunge wa upinzani.
Huyo mwenyekiti wenu namfahamu kwa sababu nimeoa huko, kwahiyo aibu
yake aibu yangu, na hata ile hotuba yake aliandikiwa hapo mlangoni… mimi
ningekuwepo asingetoa.
“Wabunge
wa upinzani waelewe nimewaambia natoa somo kwao na naomba nitoe mfano
mwingine. Haya mambo ya mnakaa hapa eti mwenyekiti kasema, kila kitu
mwenyekiti… mimi namfahamu huyo mwenyekiti wenu kwa sababu nimeoa huko,
tangu nampata binti yao yeye ni mwenyekiti, nimeoa yeye ni mwenyekiti
hadi nimezaa mtoto wa pili bado yeye ni mwenyekiti.
“Juzi
nilisikitika sana kuna mmoja alikuwa anahoji mshahara wa Rais, yeye
anachangia chama Sh milioni tatu kila mwezi… sasa hizo fedha zinakwenda
wapi?” alihoji Mlinga ambaye alitumia muda wake wote kuvishambulia
vyama vya upinzani, huku akizomewa na wabunge wa upinzani wakimwambia
“teja huyooo”.
0 comments:
Post a Comment