Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>Sababu 5 zinazoweza kumpeleka Messi Manchester City.Fahamu zaidi hapa.
Moja ya story ambayo inazungumziwa sana kipindi hiki ni tetesi za
kwamba Messi anaweza kujiunga na kocha wake wa zamani kwenyue club ya
Manchester City msimu ujao.
Hizi hapa ni sababu 5 ambazo zimechambuliwa kuonyesha uwezekano wa Messi kujiunga na Manchester City.
1)Guardiola connection
Pep anaweza kuwa kivutio kikubwa kwa Messi kwa sababu wamepata mafanikio
makubwa wakiwa pamoja ndani ya Barcelona. Muda wote Pep amekua shabiki
mkubwa wa Messi na anamuamini kiasi cha kumuacha afanye kile
anachofikiria uwanjani bila maelekezo yake akiamini hawezi kumuangusha.
Kila mchezaji angependa kuwa na kocha kama huyu.
2)Changamoto mpya
Messi ameshinda karibia kila taji ambalo anatakiwa kushinda akiwa na
Barcelona. Kuanzia binafsi hadi ya ki-team, sasa kwa mtu ambaye
anatafuta mafanikio mengine anaweza kuamua kwenda zake kutafuta
changamoto mpya. Mfano kushinda taji la ligi ya England.
3)Muda muafaka Barca kumuuza Messi
Sasa hivi ana miaka 28 na ana thamani kubwa, baada ya miaka miachache
ijayo lazima thamani yake itapungua na hawataweza kupata pesa nyingi
kama wakimuuza sasa hivi. Wanatakiwa kumuuza na ku-focus kwa vipaji
vyenye umri mdogo kama Neymar.
4)Kufata Pesa
Messi anaweza kuongeza mshahara wake kwa kiasi kikubwa sana kama
akihamia Etihad. Wamiliki wa Man City watamuangalia Messi kama faida
uwanjani na nje ya uwanja, hivyo basi mzigo watakaompa sio wa kitoto
kama kawaida ya warabu kwenye pesa hawana noma.
5)Marafiki
Sergio Aguero na Messi ni marafiki wa karibu sana. Wamecheza pamoja
wakiwa under 20 World Cup mwaka 2005 na pia wakashinda Gold Medal kwenye
Olympic pamoja. Messi ni baba wa ubatizo wa mtoto wa Aguero kuonyesha
kwamba hawa jamaa wapo karibu hadi kifamilia.
Related Posts:
Miaka Mitano Baada ya Kufariki,Huu Hapa Ukweli Juu ya Kifo cha Patrick Mafisango kwa Saa 24 Kabla na Baada ya Ajali..!!!..Fahamu zaidi hapa.
USIKU wa Jumanne ya Aprili 15, 2012 vijana wawili wachezaji wa soka
wanabishana kuhusu kuondoka mahali walipokuwa ili wakapumzishe miili
yao baada ya pirika za kutwa nzima. Hao ni viungo wa soka, Ramadhan
Chombo ‘Redond… Read More
MZIGO WA MAN CITY, TOTTENHAM SPURS WAISHA KWA SARE YA MABAO 2-2.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Manchester
City (4-2-3-1): Bravo; Zabaleta, Otamendi, Kolarov, Clichy (Stones 84);
Toure, Silva (Delph 90); De Bruyne, Sane, Sterling (Jesus 82), Aguero
Unused subs: Caballero, Kompany, Fernando, Nolito
Goals: Sane 49,… Read More
SAMATTA ATUMBUKIA NYAVUNI GENK IKIICHAPA EUPEN BAO 1-0 LIGI KUU UBELGIJI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Mbwana Samatta ameifungia KRC Genk bao pekee wakati ikiitwanga Eupen katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Genk imeshinda 1-0 baada ya Samatta kufunga bao hilo katika dakika ya 82 akiunganisha basi safi ya Ruslan Malinovysky.
… Read More
Uganda imeyaaga rasmi mashindano ya AFCON 2017.Fahamu zaidi hapa.
Mabingwa wa kihistoria wa kombe la mataifa ya Afrika timu ya Misri,
wameitupa Uganda nje ya michuano hiyo inayoendelea nchini Gabon baada ya
kutandika bao 1-0 kwenye uwanja wa Port Gentil.
Baada ya kukaza kwa dakik… Read More
Beki wa Simba Method Mwanjali Awa Mchezaji Bora wa Mwezi wa 12..!!!..Fahamu zaidi hapa.
Sentahafu wa Simba, Method Mwanjale amechaguliwa kuwa mchezaji bora Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.
Beki
huyo wa kati, aliwashinda kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna
Niyonzima na beki Yaku… Read More
0 comments:
Post a Comment