Friday, 1 April 2016

#MICHEZO>>>BARCELONA VS REAL MADRID: RONALDO NA MESSI WANAVYOLINGANA REKODI ZA EL CLASICO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mapumziko ya lili mbalimbali kupisha mechi za kimataifa yamemalizika, sasa wachezaji wanarejea kwenye vilabu vyao kuendelea na majukumu yao. Mwishoni mwa juma hili zitapigwa mechi kibao kutoka ligi za mataifa mbalimbali, lakini akili, macho na masikio ya dunia nzima ni juu ya mchezo wa Barcelona dhidi ya Real Madri ‘El Clasico’ mchezo wa ligi ya Hispani maarufu kama La Liga.

Barcelona wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa mbele ya Madrid kwa pinti 10 wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, mchezo huo utagubikwa na hisia juu ya kifo cha gwiji wa Barcelona Johan Cruyff aliyefariki juma lililopita na Barcelona wamepanga kutoa heshima zao kwa nyota huyo kwenye mchezo huo dhidi ya Madrid.

Siku hizi game ya El Clasico si vita kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona pekee bali na fursa kwa watu kuwalinganisha Cristinano Ronaldo na Lionel Messi ndani ya uwanja kutokana na upinzani wa ubora wa wachezaji hao nyota wa timu mbili tofauti.

Bila shaka hawa ndiyo wachezaji nyota kuwahikutokea katika vilabu hivi kuwa na upinzani mkubwa kwa wakati mmoja wakichezea vilabu vyao. Ni fursa nzuri ya kuwashuhudia Messi na Ronaldo wakicheza katika timu zenye upinzani mkubwa angalau mara mbili au zadi ndani ya msimu mmoja.

Ukweli ni kwamba, wawili hao wamepokezana tuzo ya Ballon d’Or katika kipindi cha miaka nane mfululizo.
Kuelekea mchezo wa El Clasico, ukilinganisha rekodi ya wachezaji hao kufunga magoli tangu Ronaldo alipojiunga na Madrid inafanana kwa kiasi kikubwa sana.

Ronaldo na Messi wanamagoli sawa wakiwa wacheza idadi sawa ya mechi, huku Messi akimzidi Ronaldo kwenye upande wa assists.
El Clasico tangu msimu wa 2009-10…
MESSI
24 idadi ya mechi alizocheza
15 idadi ya magoli aliyofunga
10 idadi ya assists alizotoa

CRISTIANO
24 idadi ya mechi alizocheza
15 idadi ya magoli aliyofunga
2 idadi ya assists alizotoa

Gazeti moja la Madrid linalofahamika kwa AS limelinganisha rekodi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi juu ya mchezo wa El Clasico, angalia ukurasa ma mbele wa gazeti hilo hapa chini.
AS linaripoti kwamba, hakuna mtu atakayebisha kwamba Ronaldo ni mchezaji wa mechi kubwa kwa mujibu wa takwimu walizozitoa.

Lakini kati ya michezo 24 ya El Clasico waliyokutana, Messi amefanikiwa kuisaidia Barcelona kushinda michezo 12, Ronaldo amefanya hivyo mara 6, huku michezo mingine 6 timu hizo zikitoka sare.

Ukichambua idadi ya magoli yao kwenye mchezo wa El Clasico, Ronaldo amefunga magoli 9 kwenye uwanja wa Nou Camp wakati Messi ametupia mara 10 akiwa Bernabeu. Hiyo inamaanisha wachezaji hao ni hatari kwenye mchezo huo bila kujali wapo kwenye uwanja gani.

0 comments:

Post a Comment