Sunday, 5 February 2017

Nape aingilia kati sakata la wasanii wa ‘unga’..Aongea Mazito ..Msikilize hapa.Fahamju zaidi hapa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Waziri Nape Nnauye akiwa na Wema Sepetu
Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku nne tangu mkuu huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya wakiwemo wasanii wa bongo fleva na filamu.
Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda, Babuu wa Kitaa n.k

Wema Sepetu (Kushoto) alipokuwa akiwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa agizo la Paul Makonda

Nape baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu suala hilo amesema kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.
Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.

Waziri Nape Nnauye
Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.
Msikilize hapa alipokuwa akizungumza na wanahabari, leo mjini Dodoma.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kauli ya Vanessa Mdee Baada ya Kutajwa na RC Makonda Kwenye Listi ya Wahusika wa Madawa ya Kulevya.Fahamu zaidi hapa.

Iliwashangaza wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. 
Ni shutuma nzito, na hata kabla uthibitisho rasmi haujatoka, madhara ya kutajwa majina yao yameanza kuonekana katika maisha yao.

Wito huo umemkutia Vee Money akiwa nchini Afrika Kusini anakoshoot tamthilia ya MTV Shuga, na bila shaka atalazimika kukatisha kwa muda na kurudi Tanzania kwenda kituo cha polisi central, anakotakiwa Jumatatu ya kesho.

Pamoja na hivyo, Vee ameonesha kuvuta pumzi ndefu na kuacha maisha yaendelee kama yalivyo. Kupitia Instagram, Vee amepost picha hizo juu na katika ile aliyokaa ameandika: The show must go on … bomb ass dress from @asos #FILA.

Kwenye hiyo black and white ameandika: The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.”

Kwenye picha hizo amezima comments ili kuepuka maneno ya kejeli kutoka kwa baadhi ya watu ambao tayari wamefanya hivyo kwenye picha zingine. Vee anaungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Wema Sepetu, Mr Blue, TID na wengine kwenye orodha hiyo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

#Breaking news>>>Mzambia, Mtanzania Wakamatwa na Madawa ya Kulevya India Yenye Thamani ya Bilioni 9.Fahamu zaidi hapa.

NEW DELHI, INDIA: WANAWAKE wawili, Mzambia Thelma Mkandawire (38) na Mtanzania Pamela David Kiritta (41) wamekamatwa kilo nne  za madawa ya kulevya (cocaine) yenye thamani ya Rs milioni 300 sawa TZS bilioni 9.7 katika hoteli moja karibu na uwanja wa ndege wa New Delhi nchini India.
 
Askari  wanaohusika na kupiga vita madawa hayo nchini humo (NCB), waliwatia mbaroni baada ya kudokezwa na hivyo kuanza kumfuatilia Mkandawire aliyetua nchini humo kutokea Sao Paulo (Brazil) kupitia Addis Ababa (Ethiopia) ambapo walimvamia akiwa hotelini eneo la Mahipalpur akiwa na Kirrita aliyedaiwa kwenda kuupokea mzigo huo.
 
Mkurugenzi wa NCB wa Kanda ya Delhi, Madho Singh,  alisema madawa hayo yalipatikana katika mizigo ya Thelma na hivyo wanawake wote wawili wamekamatwa kuhusiana na madawa hayo ambayo thamani yake katika soko ni kubwa.
Habari nyingine zilisema kwamba Thelma aliwahi kukamatwa nchini Pakistan mwaka 2015 akiwa na madawa ya kulevya lakini aliweza kuachiliwa kwa madai ya kutoa hongo.  Pia habari zimesema  Kiritta alikuwa akikaa katika nyumba moja eneo la Vasant Kunj la Delhi Kusini tangu aingie nchini India mwanzoni mwa Januari mwaka huu.
Pamela ambaye hiyo ilikuwa ni safari yake ya tisa kwenda India, alikuwa aupokee mzigo ambapo walivamiwa na askari na kupekuliwa begi lao walikokuwa nalo  na kukutwa na madawa hayo waliyokuwa wameyaweka kitaalam kiasi kwamba mashine za uchunguzi zilishindwa kuyagundua kutokana na kufungwa kitaalam.
Inasemekana madawa hayo yangefungwa katika paketi ndogondogo na kusambazwa kwa watumiaji nchini India.
Alipoulizwa, Kiritta alikiri kuingia nchini India mara tisa tangu 2006 na amewahi kwenda katika nchi nyingine za Ecuador na Kenya kwa shughuli kama hizo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Friday, 3 February 2017

Universal Music Group (UMG) watangaza rasmi kumsainisha Diamond.Fahamu zaidi hapa.

Hatimaye record label kubwa duniani, Universal Music Group (UMG), imemtangaza rasmi kumsainisha Diamond Platnumz.

Anakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kusainishwa kwenye label hiyo.

Wimbo wake, Marry You akiwa na Ne-Yo ni wa kwanza kutoka chini ya mwamvuli wa Universal Music.

“He’s a star, he is talented and full of energy and creatively he’s on par with any international artist I’ve worked with,” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa label hiyo Afrika, Sipho Dlamini.

“He’s focused and determined to succeed. He’s passionate about his country, his people , his language and his culture and I love that. He is a first class performer on stage, his new material is authentic, fresh and African, yet it will touch people across the globe. Artists like him are the reason we do what we do.”

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kwa wanaume Tu..Jua Mbinu 10 za Kufanya ili Kumfikisha Mpenzi Wako Kileleni Haraka na Akaridhika,Huitaji Madawa Tena Ukizijua Mbinu Hizi..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Karibuni katika somo jingine ndugu wapenzi wa Udaku Special, kumekuwa na maombi toka kwa watu mbalimbali hasa wanaume wakihoji  juu ya kuweza kumfikisha mwanamke kielelni.
 kama huwezi kumfikisha mwanamke kileleni basi unausika katika hili somo!!!!...Wengi wakitaka kujua ni namna gani ya kumfikisha mwanamke kileleni kwa kuzani hawana nguvu za kuhimiri kufanya tendo kwa muda mrefu bila kufikiri kuwa kumuandaa mwanamke kabla ya tendo kunaweza kukusaidia katika kumridhisha.
Wanaume wengi huwa hawana maandalizi mazuri kwa wanawake wao kabla ya tendo la ndoa yanayoweza kuwasaidia kama kichochezi cha kuwafikisha kileleni mapema.
Basi njia hizi zinaweza kuwa msaada mkubwa endapo zitatumika ipasavyo na hata yule ambaye ulikuwa umridhishi baada ya somo hili utaweza kumlidhisha ipasavyo kwa kumfanyia yafuatayo.
1.Mpe maneno matamu okimtomasa kwa ulimi sikio lake kimahaba zaidi
2. Pitisha ulimi wako shingoni kifuani, tumboni, mapajani ni ikibidi zama chumvini walau kwa dakika kumi hivi
3. Tumia ulim wako ipasavyo kutomasa kitovu chake
4. Mnyonye lita kadhaa za mate na huku ukitumia ulimi wako ipasavyo kuuchanganya ulimi wake
5. Papasa matiti yake huku ukifinya finya chuchu zake na peleka mdomo wako huku ukinyonya kama mtoto
6. Zungusha viganja vyako karibu kila kona ya mwili wake bila kusahau kubinya binya sehemu za mbavu hips na makalio yake
7. Tekenya ki**mi chake kwa vidole vyako au kwa ulimi ikiwezekana
8. Mpe koni ya asili ajilambie kwa raha zake
9. Muweke mkao mzuri wa kupokea zawadi yake
10. Ingiza taratibu mti shimoni
Hata kama huna uwezo wa kumfikisha kileleni hiyo dozi itakusaidia vilivyo.
Naamini kama utayafanyia kazi ipasavyo tatizo la kumridhisha mwanamke litapungua..
ZINGATIA yafuatayo
Maandalizi kwanza:
Tumia muda wa kutosha mwanzoni, wanawake wanapenda kuingiliwa taratibu bila pupa. Mbusu, mfanyie masaji na mchezee kwa muda, huku ukim non'goneza maneno machafu masikioni, na tumia mda kumpapasa sehemu nyeti. Anahitaji kuloana hata kabla hujamvua nguo.
Mtafutie Style anayoipenda:
Najua wengi mnapenda ile ya kumweka juu huku ukimshika matiti yake na makalio. Itunze hiyo utaitumia badae, mwanzoni jaribu kutafuta style ambayo ina mchanganya na kumfurahisha yeye kwanza, kama vipi muulize kwanza.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Cameroon Yatinga Fainali AFCON..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Cameroon imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) baada ya kuwafunga Ghana mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili uliofanyika usiku huu mjini Frenceville nchini Gabon.
Michael Ngadeu-Ngadjui alianza kuipatia Cameroon bao la kuongoza dakika ya 72 ambapo kabla ya sekunde chache refa kupuliza kipenga cha mwisho Christian Bassogog aliipa timu hiyo goli la pili na la ushindi.
Magoli hayo mawili yanawapa Cameroon nafasi ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.
Cameroon itakutana na Misri ambayo ilitinga hatua ya fainali jana baada ya kuwafunga Burkina Faso goli 4-3 kwa mikwaju ya penalti.
Fainali hiyo itachezwa Jumapili ijayo ambapo itatanguliwa na mechi ya kusaka mshimdi wa tatu siku ya Jumamosi kati ya Ghana na Burkina Faso.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

P funk - Harmorapa ni Level Nyingine Bana..!!!.Fahamu zaidi hapa.

Producer mkongwe na mwenye heshima yake P Funk Majani ameibuka na kumzungumzia huku akimsifia msanii anayeibukia kwa kasi katika bongo fleva, Harmorapa na kusema kuwa rapa huyo ni "level nyingine".
Tangu Msanii Harmorapa ameingia kwenye muziki kwa kuanza kujifafanisha na msanii Harmonize, kila wakati rapa huyo amekuwa akiingia kwenye 'headline' mbalimbali na kuzungumziwa na wasanii wengi wakubwa nchini, wengine wakifurahishwa na matendo yake huku wengine wakimdhihaki na kuona kuwa hastaili kuwa mwanamuziki.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kitwanga Aibuka Bungeni....Atishia Kuongoza Wananchi Kung'oa Mitambo ya Maji Ziwa Victoria.Fahamu zaidi hapa.

Mbunge  wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga, amesema yuko tayari kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kwenda kuing’oa ama kuizima mitambo ya kusukuma maji Ziwa Victoria kupeleka mkoani Shinyanga ikiwa maji hayatafika jimboni kwake.

Kitwanga alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la nyongeza.

Mbunge huyo alisema wananchi wa jimbo lake katika Vijiji vya Ihelela Kashwasa, walishapewa ahadi tangu mwaka 2008 kuwa wangeunganishiwa maji kutoka katika mtambo wa kusukuma maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Shinyanga, lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

“Ahadi hii ilitolewa na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete, lakini kila siku ni ahadi bila utekelezaji. Kweli nitawasindikiza wananchi wangu kuzima mitambo ili maji yasipelekwe Shinyanga, nasema kweli nitafanya hivyo,” alisisitiza Kitwanga.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isaack Kamwelwe, alikiri kuwa Rais wa awamu ya nne alitoa ahadi hiyo mwaka 2008 kwamba wananchi wa maeneo ya Ihelela wataunganishiwa maji kutoka bomba la Ziwa Victoria.

Hata hivyo, Kamwelwe alimuomba mbunge huyo asihamasishe watu kuzima mitambo hiyo wakati wowote badala yake wavute subira.

Katika swali la msingi la Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako (CCM), alitaka kujua Mto Malagarasi una ujazo gani wa maji na kama yanatosheleza mahitaji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Kamwelwe alisema serikali imepanga kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia Mto Malagarasi ikiwamo mradi wa maji kwa ajili ya miji ya Urambo, Kaliua pamoja na kilimo cha mwagiliaji na uzalishaji umeme wa megawati 44.5.

“Wakati wa masika, mto huo unakuwa na maji yanayotiririka kwa mita za ujazo 55 kwa sekunde na wakati wa kiangazi unakuwa na mita za ujazo 40 kwa sekunde," alisema.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mwiguli Nchemba Amkataza Makonda Kutembea na Ving'ora vya Polisi.Fahamu zaidi hapa.

WAKUU wa Mikoa na Wilaya ni ruksa kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali za utendaji, zikiwamo za ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Ufafanuzi huo ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliyetaka kujua kama ni itifaki za kiserikali kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora.
Mbowe alishangaa na kuhoji kuwa ni itifaki gani kwa viongozi hao, akatoa mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutembea na kikosi cha polisi chenye watu tisa, pikipiki za polisi za kuongoza msafara na gari lenye king’ora.
Waziri Mwigulu alisema, viongozi hao hawaruhusiwi kutembea na misafara yenye magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda ofisini, labda kama viongozi wa mkoa na polisi wapo ofisi moja, lakini hawakatazwi kwenda navyo wanapoenda eneo la kazi maalumu.
“Viongozi hao wanapokuwa na majukumu ya kwenda kutoa maelekezo au kufanya shughuli zinazohusiana na majukumu ya ulinzi wa maeneo yao, wanaruhiswa kuwa na magari hayo,” alisema.
Chanzo
               Udakuspecially

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

New Video: Diamond Platnumz ft Ne-Yo – Marry You.

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, video ya Diamond Platnumz ya wimbo wake, Marry You aliomshirikisha Ne-Yo imetoka. Kwa mara ya kwanza video hii imewekwa kwenye channel ya Vevo ya staa huyo.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Picha: Wema Sepetu na wenzake watua Central Polisi Dar......Walitakiwa Wajisalimishe Leo Kwa Kujihusisha na Madawa ya Kulevya.

Kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwataka baadhi ya mastaa wanaoshukiwa kujihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuwasili kituo cha polisi cha kati siku ya leo baadhi ya mastaa wametii agizo hilo na kuwasili.

Wema Sepetu ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Da es salaam Paul Makonda kwamba anatumia Madawa ya kulevya, amewasili kituoni hapo  huku akiwa amevalia vazi la  hijab.

Wasanii wengine waliofika kituoni hapo ni pamoja na TID, Nyandu Tozzy pamoja na mtangazaji wa Clouds TV Babu wa Kitaa.
TID akiwa kituoni hapo

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 2 February 2017

#Breaking News>>>>Necta Watangaa Matokeo ya Kidato cha Nne Mwaka 2016,Tazama Matokeo Hapa..!!!.

Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne (CSEE) na QT kwa mwaka 2016. Jumla ya watahiniwa 277,283 ambao ni sawa na asilimia 70.09 ya watahiniwa waliofanya mitihani kidato cha nne 2016 wamefaulu.

Wasichana waliofaulu ni 135,859 ambao ni swa na asilimia 67.06 wakati wavulana waliofaulu ni 142,424 sawa na asilimia 73.36.

Kwa mwaka 2015, watahiniwa waliofaulu walikuwa 272,947 sawa na asilimia 67.53. Ukilinganisha na matokeo ya mwaka huu, ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.56. Idadi hii ni ya watainiwa wote, yaani watahiniwa wa shule na watahiniwa wa kujitegemea.

Bonyeza hapa kuweza kuona matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 –>CSEE 2016

Bonyeza hapa kuweza kuona matokeo ya QT mwaka 2016  –>(QT) 2016

Wanafunzi 10 Bora Kitaifa



  1.      Alfred Shauri (Feza Boys)
  2.     Cynthia Nehemiah Mchechu (St. Francis Girls)
  3.     Erick Mamuya (Marian Boys)
  4.     Jigna Chavda (St. Mary Goreth)
  5.     Naomi Tundui (Maria Girls)
  6.     Victoria Chang’a (St. Francis Girls)
  7.     Brian Johnson (Marian Boys)
  8.     Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)
  9.     Ally Hassan Koti (ALCP Kilasara)
  10.     Emmanuel M. Kajege (Marian Boys)


Wasichana 10 Bora Kitaifa


  1.     Cynthia Mchechu (St. Francis Girls)
  2.     Jigna Chavda (Mary Goreti)
  3.     Naomi Tundui (Maria Girls)
  4.     Victoria Chang’a (St. Francis Girls)
  5.     Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)
  6.     Christa Edward (St. Francis Girls)
  7.     Nelda John (Marian Girls)
  8.     Mariamu Shabani (Kifungilo Girls)
  9.     Beatrice Mwella (St. Mary’s Mazinde Juu)
  10.     Rachel Kisasa (Canossa)


Wavulana 10 Bora Kitaifa


  1.     Alfred Shauri (Feza Boys)
  2.     Erick Mamuya (Marian Boys)
  3.     Brian Johnson (Marian Boys)
  4.     Ally Koti (ALCP Kilasara)
  5.     Emmanuel Kajege (Marian Boys)
  6.     John Ng’hwaya (Nyegezi Seminary)
  7.     Clever Yohana (Living Stone Boys)
  8.     Desderius Rugabandana (Morning Star)
  9.     Kennedy Boniface (Feza Boys)
  10.     Assad Msangi (Feza Boys)


Shule 10 Bora Kitaifa


  1.     Feza Boys
  2.     St. Francis Girls
  3.     Kaizirege Junior
  4.     Marian Girls
  5.     Marian Boys
  6.     St. Aloysius Girls
  7.     Shamsiye Boys
  8.     Anwarite Girls
  9.     Kifungilo Girls
  10.     Thomas More Machrina


Shule 10 za Mwisho Kitaifa


  1.     Kitonga
  2.     Nyeburu
  3.     Masaki
  4.     Mbopo
  5.     Mbondole
  6.     Somangila Day
  7.     Dahani
  8.     Ruponda
  9.     Makiba
  10.     Kidete


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

VIDEO..Hivi Ndivyo Mbowe na Naibu Spika Leo Walivyoozana Bungeni Kisa Swali la Lema Kufungwa Gerezani kwa Waziri Mkuu..!!.Fahamu zaidi hapa.

Mbowe aliuliza kuwa kutokana na viongozi wa chadema ikiwamo wabunge 2 Lema kunyimwa dhamana na Lijuakali kufungwa kwa sababu za kisiasa, wabunge 6 wa Chadema kufungwa, kiongozi wa Chadema Lindi nae kufungwa na viongozi wengine takribani 216 kufungwa au kuwa na kesi mahakamani ni utekelezaji wa kauli ya Magufuli kufuta upinzani kabala ya 2020?
Waziri mkuu anasema masuala ya mahakamani hawezi kuyazungumzia na nchi inaongozwa kwa katiba na sheria
Mbowe anasema ushahidi upo wa kauli za rais kuanagamiza upinzani kabla ya 2020 na hafuati katiba na sheria kama alivyodai ila waziri na wakithibitisha hilo waziri mkuu atakuwa tayari kujiuzulu, ndipo naibu spika akazuia maswali hayo na kukawepo kelele kutoka kwa wabunge wa upinzani



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kudadeki..Eti Ng'ombe 150 Watachinjwa siku ya Birthday ya Mugabe...!!!!!.Fahamu zaidi hapa.

Chama kinachotawala nchini Zimbawe Zanu-PF, kimeanza kuchangisha pesa kwa sherehe za siku ya kuzaliwa ya Rais Robert Mugabe ambaye anahitimiza miaka 93.
Waandalizi wa sherehe hizo wanasema kuwa wanataka kuchangisha ng’ombe 150 kwa chakula.
Gazeti la serikali la Herald limemnukuu mbunge Never Khanye, akisema kuwa hakuna mtu atalazimishwa kuchanga lakini wakulima wakubwa katika maeneo ya matabeleland ambapo shehere zitafanyika, ni lazima watoe ngombe mmoja kila mmoja, kutoa asante kiongozi huyo wa miaka mingi.
Wakulima wakubwa ni wale walipata mashamba makubwa kutoka kwa serikali kufuata hatua ya serikali ya kunyakua mashamba kutoka wa wazungu wakati wa programu iliyokumbwa na utata nchini Zimbabwe.
Chama cha Zanu-PF kinasema kuwa kinatarajia karibu watu 100,000 kuhudhuria sherehe hizo.
Shere hizo zitafanyika eneo la Matobos nje kidogo ya mji wa Bulawayo.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

VIDEO:Hii ni Kali Aisee..Baada ya Kuimba 'Wacha Waisome Namba'Khadija Kopa Naye Aanza Kuisoma Namba,Alia Hali Ngumu,...!!!.Fahamu Zaidi hapa.

Msanii wa taarab Bongo, Khadija Kopa ni kama naye sasa 'anaisoma namba' baada ya kutoa kilio chake juu ya kupungukiwa na mapato yatokanayo na muziki na kutaja sababu mojawapo kuwa ni uamuzi wa serikali kuzuia matamasha ya muziki baada ya saa 6 usiku.
Amesema hivi sasa yeye na wenzake wapo katika mpango wa kuongea na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ili aangalie upya sheria iliyowekwa ya kufunga sehemu za starehe saa sita usiku kwa kuwa inawaumiza wasanii wa taarabu.
Amesisitiza kuwa kwa sasa biashara ya bendi za taarabu imekuwa ngumu na wanakosa mashabiki kwa kuwa muda wa kutumbuiza umekuwa mchache hivyo wanajipanga kuomba kwa mkuu wa mkoa ili siku za Ijumaa na Jumamosi ziongezewe  muda hadi saa tisa usiku.
Khadija Kopa aliyekuwa akizungumza kupitia eNewz ya EATV, amesema sababu nyingine ni utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia majina ya wasanii wakubwa wa taarab kufanya show na kujiingizia kipato kisicho halali.
Hii ni ishara kuwa Khadija Kopa ambaye pia ni muimbaji wa wimbo wa 'Wataisoma namba' kupitia bendi ya TOT, naye sasa 'anaisoma namba'.
Mtazame hapa mbele ya kamera ya eNewz:-



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Mamelod Sundowns Yashangazwa na Azam Fc,Kocha Wao Haamini Kilichotokea Uwanjani Jana Usiku.Fahamu zaidi hapa.

Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini  wameshindwa kufurukuta mbele ya Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa Taifa usiku huu.
Mamelodi ambao wapo nchini kwa ziara ya maandalizi kwa ajili ya ligi kuu nchini Afrika Kusini na mchezo wa Super Cup dhidi ya TP Mazembe itakayochezwa mwezi huu, licha ya kutawala muda mwingi wa mchezo walishindwa kupenya ngome imara ya Azam iliyoongozwa na nahodha Himid Mao.
Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Sundowns, Pitso Mosimane alisema kuwa Azam FC walikuwa kipimo bora kwao kutokana na kiwango walichoonyesha.
“Nawapongeza vijana wangu kwa kucheza vizuri na nimeridhika na kiwango chetu ingawa sijafurahi kwa sababu hatukufunga bao. Pia niwapongeze Azam kwa kucheza vizuri na walionyesha kiwango bora uwanjani,” alisema Mosimane.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wabunge Wacharuka Bungeni Kuhusu Suala la Maslahi ya Zanzibar,Hoja za Lissu Zazidi Kuichachafya Serikali..!!!..Fahamu zaidi hapa.

SERIKALI imetoa ufafanuzi juu ya marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana na kubainisha kuwa masharti ya mikopo ya nje, yaliyowekwa dhidi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), yanatokana na masharti ya wadau wanaotoa mikopo hiyo.
Aidha, imebainisha kuwa kupitia marekebisho hayo ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana yanayopendekeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) kufaulisha mkopo kwa SMZ, yana nia njema na yamelenga kuwahakikishia wahisani hao kuwa masharti yao yanafuatwa.
Ufafanuzi huo wa serikali umekuja baada ya kuibuka mjadala mkali bungeni kutoka kwa baadhi ya wabunge, wanaotaka marekebisho ya sheria hiyo yabadilishwe kwa kuwa yanainyima uhuru Zanzibar kukopa yenyewe kadri ya uwezo wake.
Hoja hizo ziliibuka baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 4 wa Mwaka 2016 bungeni mjini Dodoma jana.
Akitoa ufafanuzi huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitaja baadhi ya wadau wanaoikopesha SMT ambao ni Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Saudi Fund, kuwa katika moja ya sehemu ya makubaliano ya primary loans wanahitaji kuona kuna utaratibu wa wanaonufaika kuwajibika katika malipo.
“Haya si masharti ya SMT ni masharti ya wanaotukopesha, mkiyafungia mtaweka vikwazo kwa hawa wanaotukopesha kwa masharti nafuu,” alisisitiza Dk Mpango.
Alisema lengo la muswada huo, ni kuweka kisheria sasa kwamba fedha zinazokopeshwa na SMT kwa SMZ zinawasilishwa kwa masharti yaliyopo na zinalipwa kama ilivyopangwa lakini pia kuhakikishia wahisani hao kuwa masharti waliyoweka ya ukopeshaji yanafuatwa.
Alisema madai kwamba SMZ imekuwa ikikandamizwa na kunyimwa fursa ya kujipatia mkopo si ya kweli, kwani hata katika sheria hiyo ya Mikopo, Misaada na Dhamana vipo vifungu vinavyotoa mamlaka ya serikali hiyo kupokea fedha bila kupitia mgongo wa SMT.
“Leo nimeangalia deni la nje kuanzia mwaka 1993 mpaka mwaka jana, fedha zilizokopwa na SMT kwa ajili ya SMZ zilifikia dola milioni 772.39 sawa na asilimia 2.59 ya deni lote la taifa letu,” alieleza Dk Mpango.
Masaju wakati akihitimisha mjadala huo, alimuunga mkono Dk Mpango kuhusu suala hilo la kufaulisha mkopo kwa SMZ na kubainisha hata pale itakapotokea tatizo lolote katika mikopo hiyo inayokopeshwa tena kwa Zanzibar atakayewajibika si Zanzibar bali ni Serikali ya Tanzania.
Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) aliwataka wale wote wanaopinga marekebisho ya sheria hiyo ya mikopo, misaada na dhamana, kuwasilisha hoja za nini kifanyike na si kubakia kulalamika hali ambayo hailisaidii Bunge wala serikali.
Alisema kwa upande wake kutokana na uzoefu wake, haoni tatizo lolote katika marekebisho ya sheria hiyo kutokana na ukweli kuwa yamefanyika kwa sababu ya matakwa ya wakopeshaji na wala hayana nia yoyote ovu kama inavyodhaniwa na baadhi ya wabunge.
“Muswada huu ni muswada mzuri, uzuri wa sheria yoyote ni pale unapoanza kuitumia ndio utaona. Kazi ya bunge ni kutunga sheria, tunapaswa tuwe watulivu na kujenga hoja ili kutengeneza sheria nzuri,” alisisitiza Chenge aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aliongeza kuwa, “Namheshimu sana Lissu (Waziri Kivuli wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu) amesema mengine mazuri, lakini kwa hili angesaidia sasa nini tufanye, kulalamika hakusaidii Bunge wala mtu”.
Alisema sheria hiyo imetungwa kulingana na matakwa ya Katiba kwani kwa mujibu wa katiba hiyo mikopo ya nje na dhamana inayotolewa na serikali sheria zake haziwezi kutungwa nje ya Katiba hiyo.
“Kupitia muswada huu inapendekezwa angalau ifanyike utaratibu utakaowezesha SMZ kupata mikopo ya nje kupitia mgongo wa SMT. Huu ni utaratibu wa watoa mikopo, haya yanayozungumzwa hapa hayaendani na wanachokitaka watoa mikopo hiyo,” alisema.
Katika muswada huo, ambao una sheria sita zilizofanyiwa marekebisho, kwenye marekebisho ya sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana Sura ya 134, inapendekeza masharti mapya ya mikopo kuhusu serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Marekebisho hayo yamependekeza serikali hizo kuingia katika utaratibu wa on-lending (serikali ya muungano ndiyo inayokopa na baadaye kuikopesha SMZ baada ya serikali hiyo kukidhi mahitaji na masharti ya kupewa mkopo).
Kwa mujibu wa Masaju, marekebisho ya sheria hiyo yanapendekeza kabla ya SMT haijakopa kwa niaba ya SMZ, lazima ijiridhishe kuwa mkopo huo unaweza kulipwa.
“Lengo la marekebisho haya ni kuweka utaratibu wa kisheria utakaowezesha serikali ya Tanzania kukidhi masharti ya baadhi ya wakopeshaji wanaohitaji masharti hayo na pia kuhakikisha mikopo inalipwa kwa mujibu wa makubaliano ya mkopo,” alisema.
Hata hivyo, wakati akiwasilisha mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu muswada huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Mchengerwa, alisema kamati hiyo inaishauri serikali katika suala hilo la ukopaji itoe uhuru mkubwa wa kukopa kwa Zanzibar kadri ya uwezo wake.
Naye Lissu wakati akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu muswada huo, alisema ni wakati sasa wa serikali ya Tanzania kuipatia uhuru Zanzibar ili nayo iwe na uwezo wa kukopa yenyewe kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar.
Pamoja na yao, baadhi ya wabunge wa CUF na CCM walirushiana maneno makali walipokuwa wakichangia muswada huo, hatua iliyompa wakati mgumu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Najma Murtaza Giga.
Mwenyekiti huyo alilazimika kuwatuliza wabunge hao na kuwaomba waheshimiane na kuvumiliana wakati mjadala huo ukiendelea, kwani wakati mmoja wao akiwasilisha hoja inayopinga upande mwingine, walikuwa wakirushiana maneno bila kuheshimu kiti.
Wakati akichangia mjadala huo, mbunge wa Wingwi, Juma Kombo Hamadi (CUF), aliitaka serikali kuangalia kwa makini marekebisho ya sheria hiyo kwani badala ya kutoa unafuu kwa upande wa Zanzibar, yanazidi kuinyima haki serikali hiyo ya SMZ.
Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM) alisema marekebisho ya sheria hiyo, hajalenga kukandamiza upande wowote, isipokuwa imeweka kinga na kuongeza masharti kwa wakopaji ili kudhibiti taasisi zinazokopa kiholela bila kuwa na uwezo wa kulipa.
Masaju alisema marekebisho hayo ya sheria ya mikopo ya elimu ya juu, yanapendekeza bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosomea kozi za Stashahada (Diploma) na sifa za kupata mkopo huo zitachapishwa kwenye gazeti la serikali.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Utata Mtupu ‘Dili’ Minofu ya Punda,Kasi Uchinjaji Yafika 100 kwa Siku,...!!!..Fahamu zaidi hapa.

UTATA umeibuka kuhusiana na biashara ya minofu ya punda nchini baada ya watetezi wa haki za wanyama kudai kuwa viumbe hao watatoweka nchini ndani ya miaka michache ijayo ikiwa kasi ya kuchinjwa kila uchao itaendelea kama ilivyo sasa.
Aidha, imeelezwa kuwa endapo jitihada hazitafanywa katika kusimamia biashara ya minofu ya wanyama hao, kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa umaskini katika kaya za maeneo yanayotumia wanyama hao kama chombo chao cha usafiri.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Ustawi wa Wanyama Tanzania (Taweso), Dk. Thomas Kahema, ndiye aliyeeleza kuhusu dalili za kutoweka kwa punda nchini wakati akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya biashara ya punda wilayani Mpwapwa, mkoa wa Dodoma, jana.
Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Joram Mghwira, ambaye anashughulikia wanyama, alikiri kuwapo kwa hatari ya kutoweka kwa punda na jambo hilo kuwaathiri wananchi wanaowatumia wanyama hao kama chombo cha kazi na usafiri, chanzo cha tishio hilo kikiwa ni pamoja na kuwapo kwa wizi na uchinjaji holela wa wanyama hao kwenye viwanda vilivyopo Dodoma na Shinyanga.
UTATA WENYEWE
Akifafanua juu ya kuwapo kwa hofu ya kutoweka kwa punda nchini, Dk. Kahema alisema kuwa hadi sasa, utafiti uliofanywa na shirika lake unaonyesha kuwa nchi nzima ina punda takribani 500,000 huku kasi ya uchinjwaji wa wanyama hao ikifikia wastani wa punda 100 kila uchao.
Alisema takwimu hizo ndizo zinazoongeza hofu ya kutoweka kwa punda na hivyo akazitaka mamlaka husika kuchukua hatua ya kusimamia sheria kwa umakini ili kuwaokoa viumbe hao.
Dk. Kahema alisema kushamiri kwa biashara hiyo kila siku, kutasababisha pia kupungua kwa nguvu kazi ya jamii zenye punda ambao huwasaidia katika shughuli zao zikiwamo za ubebaji wa mizigo na kazi nyingine mbalimbali.
Alisema mbali na biashara ya kitoweo, pia ngozi za punda zaidi ya 100 wanaochinjwa kila uchao huuzwa katika viwanda vya Wachina vilivyopo Dodoma na Shinyanga.
Aliongeza kuwa iwapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa sasa, taifa litakuwa halina mnyama huyo kutokana na ukweli kuwa biashara ya ngozi yake pia ingali ikishika kasi kubwa China na kwingineko barani Asia.
Alisema hatari zaidi ya kutoweka kwa punda nchini inaongezwa pia na ukweli kuwa hakuna uwiano mzuri kati ya idadi ya wale wanaochinjwa kila uchao na kuzaliana kwao.
Kuhusiana na athari za kiuchumi, Dk. Kahema alisema wastani wa bei ya punda mmoja kwa sasa ni Sh. 200,000, lakini utafiti unaonyesha kuwa thamani yake kwa ujumla kutokana na mchango wake kwa kaya zenye wanyama hao ni takribani Sh. milioni 5 kwa mwaka.
“Kwa sasa punda mmoja anauzwa Sh. 200,000 wakati kwa mwaka mnyama huyo hufanya kazi ya zaidi ya Sh. milioni 5 kwa mkulima iwapo atatumika kusaidia shughuli za kulima, kuchota maji, kubeba mizigo na kazi nyingine za kila siku,” alisema Dk. Kahema.
Akizungumzia utata kuhusiana na hatima ya punda nchini, Dk. Mgwira wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, alisema pamoja na serikali kuwapa vibali wawekezaji kufungua viwanda vya nyama za punda, lakini sheria zinawataka wawekezaji hao kuwa na mikakati ya inayoonyesha jinsi watakavyoongeza kuzaliana kwa wanyama hao nchini.
Ofisa mmojawapo wa Kiwanda cha Nyama ya Punda cha Huwa Cheng Company Limited kilichopo mjini Dodoma, Mohamed Hamis, alisema baada ya kufungiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kutozwa faini kutokana na kasoro za kimazingira, sasa kiwanda hicho kimefunguliwa na kinaendelea na uzalishaji.
“Hivi sasa kwa siku tunaingiza punda 40 kulingana na kibali tulichopewa… lakini uwezo wetu ni kuchukua punda 600,”alisema Hamis, na kuongeza kuwa jana serikali iliwapatia kibali kingine cha kuingiza punda 80 kwa siku kutokana na wingi wa punda mnadani.
Kuhusu mkakati wa kuufanya uzalishaji uwe endelevu ili punda wasipotee, Hamisi alisema kuna shamba la punda mkoani Singida na hadi sasa wapo punda zaidi ya 200 wanaofugwa kukidhi sharti hilo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa punda katika Manispaa ya Dodoma, Mussa Charles, alisema wamekuwa wakiuza punda mmoja kwa Sh. 190,000.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kudadeki..Obama Amuibukia Trump,Amshambulia Kwa Kauli Hizi Juu ya Agizo Lake la Kuwazuia Waislamu Wasiingie Marekani.Fahamu zaidi hapa.

RAIS mstaafu Barack Obama ameibuka na kuzungumzia siasa ikiwa ni mara ya kwanza tangu astaafu urais – akiunga mkono maandamano yanayosambaa nchini kote kupinga agizo la Rais Donald Trump kuhusu uhamiaji.
“Rais Obama amesikitishwa na kiwango cha matukio yanayotokea hivi sasa kwenye jamii mbalimbali nchini,” kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake ya rais mstaafu.
“Wananchi kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kukusanyika, kuandaa na kufanya sauti zao zisikike na maofisa waliochaguliwa, ndicho hasa tunachotarajia kukiona pale maadili ya Marekani yanapokuwa matatizoni,” alisema Obama.
Hata hivyo, Rais huyo mstaafu hakuingia ndani zaidi kuhusu matamko ya Trump – yakiwamo ya kuzuia ruhusa ya wakimbizi kuingia nchini na kusimamisha uhamiaji wa watu kutoka nchi saba duniani zikiwamo Iraq na Syria.
Badala yake, Obama ambaye ana haki ya kuingilia kati pale mambo ya kisiasa na hasa ‘masuala nyeti’ yanapokuwa hatarini, aliomba “kulinganishwa kwa uamuzi wa sera zake za nje na za Trump.”
“Kwa kuzingatia mlinganisho na uamuzi wa sera za nje za Rais Obama, kama tulivyosikia kabla, kimsingi rais hakubaliani na suala la ubaguzi dhidi ya watu kwa sababu ya imani yao au dini,” kwa mujibu wa taarifa.
Katika mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari, Obama alisema anaweza kuingilia “nyakati fulani wakati anapokuwa anadhani kwamba maadili yetu ya msingi yamo hatarini.
Obama kwa kiasi kikubwa alishambulia moja kwa moja kauli ya Rais Trump: kwamba “Sera yangu ni sawa na alichokifanya Rais Obama mwaka 2011 alipopiga marufuku viza kwa wakimbizi kutoka Iraq kwa miezi sita.”
Gazeti la Washington Post lilielezea kauli hiyo kama madai yasiyo na kichwa wala miguu, “kwa sababu utawala wa Obama haukupata kuzuia Wairaqi kuingia nchini. Utawala huo ulibana uingiaji wa Wairaqi nchini mwaka 2011 wakati ilitangaza majina yaliyokuwa kwenye kanzidata ya nchi, baada ya Mwiraqi ambaye alikuiwa na hifadhi nchini, kubainika kuwa alipata kutega mabomu barabarani nchini mwake”.
Hata hivyo, msaidizi wa Obama hakujibu swali la alikokuwa Rais huyo mstaafu wakati akitoa taarifa yake hiyo.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wakuu Wa Shule za Dar Ambazo Zimeshika Mkia Matokeo Kidato cha Nne Watumbuliwa.Fahamu zaidi hapa.

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne  kwama 2016 yametoka na miongoni mwa Shule 10 zenye Wanafunzi waliofeli zaidi Tanzania, 6 zinatoka Dar es salaam na hiyo imemfanya Mkuu wa wilaya ya kigamboni Hashim Mgandilwa kufanya uchunguzi kwenye hizo shule.

Baada ya uchunguzi wake Mkuu huyu wa wilaya ameagiza kushushwa vyeo kwa Wakuu wa shule mbili za za Sekondari ambazo ni Kidete na Somangila Day na ametoa sababu mbili za kuchukua uamuzi huo.

Amesema sababu ya kwanza ni kufelisha na pili kuna mmoja amepata ukuu wa shule katika namna ambayo ina ukakasi na inaonekana kwa namna moja ama nyingine kuna Watu walimtengenezea kukipata hicho cheo

"Hiyo ilileta mvutano shuleni na baadhi ya Walimu walimuunga mkono na wengine hawakumuunga mkono hivyo ikasababisha Walimu takribani 7 kuihama shule hiyo kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu." Amesema  DC Mgandilwa

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Ridhiwani Kikwete Afafanua Kwanini ilikuwa ni Aibu Kwa TFF na Waziri, Diamond Kukabidhiwa Bendera Kwenda Gabon.Fahamu zaidi hapa.

Ridhiwani Kikwete aliingia kwenye headlines mwanzoni mwa mwezi uliopita pale alipoandika post Instagram akisikitishwa na kitendo cha Diamond kukabidhiwa bendera na Waziri wa michezo, Nape Nnauye kwenda kutumbuiza kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika, nchini Gabon.



Mbunge huyo wa Chalinze, amedai kuwa, post yake haikumlenga Diamond, bali aliwapa ujumbe shirikisho la soka Tanzania, TFF na Waziri Nape.


“Kilichonifanya niandike ile meseji ni baada ya kuona kwamba mashindano yanayoenda kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa miguu, lakini to our surprise, badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira wa miguu, tunawapa waburudishaji kwa maana ya wanamuziki kama Diamond,”
Ridhiwani alisema kwenye mahojiano na The Beauty TV.

“Matarajio yetu sisi ni kumuona kapteni wa taifa ndiye anayepokea bendera na sio wanamuziki,” ameongeza. “Pia watu wa TFF, kwamba nao wanashangilia yale anayoyafanya waziri?” Hivi vitu lazima tuwe serious.”

“Diamond yeye nampongeza sana, kwa hatua aliyofika, anafanya kazi nzuri, na ndio maana watu wamemuona, wamempa nafasi ya kwenda kutumbuiza ambayo sisi kama watanzania we feel proud. Lakini the bottom line ni kwamba, nini agenda kubwa inayomfanya Diamond aende Gabon? Ni mpira wa miguu, Diamond si mchezaji wa mpira wa miguu, hata kama labda anashabikia mpira wa miguu, lakini yeye ni mshabiki tu, wanaoenda kushiriki pale ni wachezaji.”

Ridhiwani amekiri kuwa kitendo hicho kilimsikitisha na ndio maana hakupenda kukaa kimya.

“Si kwamba sikupenda kwasababu amepewa Diamond, hapana, sikupenda kwa sababu, matarajio ya mimi mpenzi wa mpira ni kumuona kapteni wangu wa timu ya taifa anapokea bendera kwa niaba ya watanzania wote, anakwenda kutuwakilisha kule, hata kama tutashindwa, hata kama tutafanikiwa lakini anayetakiwa kwenda kule ni kapteni wa timu ya mpira wa miguu kwenda kutuwakilisha kama taifa na si vingine.”


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Agizo la Rais Magufuli latekelezwa, pikipiki 16 zatolewa matari kwa kupita barabara za mwendokasi.Fahamu zaidi hapa.

Agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli la kulitaka jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kung’oa matairi vyombo vyote vya moto vitakavyopita katika barabara za mabasi yaendayo haraka limeanza kutekelezwa kwa vitendo ambapo pikipiki kumi na sita zimeng’olewa matairi na wahusika wakitarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 2 Febuari mwaka huu.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema kuwa pikipiki hizo 16 zilizotolewa matairi ni sehemu tu ya nyingi zilizokamatwa huku akisema kuwa mkakati huo ni endelevu ambapo wote watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Dkt Magufuli alitoa maagizo kwa askari kukamata magari na pikipiki zinazotumia barabara za mabasi yaendayo haraka na kisha kuzitoa matairi na madereva hao wafikishwe mahakamani. Rais Magufuli alisema madereva hao wakiuliza matairi yao yalipo, wajibiwe kuwa askari hawajaajiriwa kulinda matairi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Wednesday, 1 February 2017

ULIMWENGU ATOA PASI YA BAO, TIMU YAKE YATOA SARE HISPANIA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu jana ametoa pasi ya bao timu yake, AFC Eskilstuna ikipata sare ya 1-1 na Elfsborg zote za Ligi Kuu ya Sweden katika mchezo wa kirafiki nchini Hispania.


Katika mchezo huo uliofanyika mjini Barcelona, Ulimwengu aliyejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa Januari, alimsetia mshambuliaji wa Nigeria, Chidi Dauda Omeje kufunga bao hilo la AFC Eskilstuna.


Akizungimza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwa simu kutoka Hispania, Ulimwengu alisema kwamba anamshukuru Mungu ameanza vizuri katika timu yake mpya.

Thomas Ulimwengu jana ametoa pasi ya bao timu yake, AFC Eskilstuna ikipata sare ya 1-1 na Elfsborg “Leo (jana) tumecheza mechi ya kirafiki tumetoa sare ya 1-1 na mimi ndiye nimetoa pasi ya bao letu,”alisema mchezaji huyo aliyekaribia kusajiliwa Yanga mwaka 2012 akitokea Moro United, lakini akachagua kwenda AFC Eskilstuna, ambayo baadaye ilimuuza TP Mazembe.


Kwa wiki nzima sasa, Ulimwengu yuko Hispania na klabu yake hiyo mpya, AFC Eskilstuna kwa maandalizi ya Ligi Kuu ya Sweden. 


Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya AFC Eskilstuna ya Sweden, alikocheza hadi 2011 TP Mazembe alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.


Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana.


Ulimwengu anajivunia kushinda mataji makubwa akiwa na Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

FARID MUSSA AKINUKISHA HISPANIA TENERIFE IKITOA SARE NA ZAMBIA U20.FAHAMU HAPA

 WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Malik Mussa jana amecheza dakika zote 90 timu ya vijana ya Tenerife ikilazimishwa sare ya 0-0 na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia katika mchezo wa kirafiki.

Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwa simu, Farid alisema kwamba walikutana na timu nzuri ya Zambia katika mchezo mzuri wa kirafiki.

“Jamaa nilizungimza naop baada ya mechi nikawaambia mimi ninatoka Tanzania, wakafurahi sana na wakaema nitafika mbali nisivunjike moyo, mimi ni mchezaji mzuri,”alisema Farid.

U20 ya Zambia ipo Hispania kwa kambi ya siku 10 kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrikaya Vijana na watacheza pia na U-20 za Las Palmas, Real Madrid na Barcelona.


Zambia ndiyo wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika la U20 na wataanza kampeni yao ya kuwania taji hilo nyumbani kwa kumenyana na Guinea Februari 26 mwaka 2017 Uwanja wa Heroes.


Farid alijiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary Desemba mwaka jana kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.


Azam FC ilimtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa.


Farid alitua Hispania kwa mara ya kwanza Aprili 21, mwaka jana baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.


Na ilimchukua wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo Desemba, 2016.


Na baada ya kutua Tenerife amepangiwa kuanza kuchezea kikosi cha U23 ili kupata uzoefu kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza kinachocheza Ligi Daraja la Kwanza nchini humo, maarufu kama Segunda.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa