Mbunge
wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga, amesema yuko tayari kuwahamasisha
wananchi wa jimbo lake kwenda kuing’oa ama kuizima mitambo ya kusukuma
maji Ziwa Victoria kupeleka mkoani Shinyanga ikiwa maji hayatafika
jimboni kwake.
Kitwanga alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la nyongeza.
Mbunge
huyo alisema wananchi wa jimbo lake katika Vijiji vya Ihelela Kashwasa,
walishapewa ahadi tangu mwaka 2008 kuwa wangeunganishiwa maji kutoka
katika mtambo wa kusukuma maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Shinyanga,
lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.
“Ahadi
hii ilitolewa na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete, lakini
kila siku ni ahadi bila utekelezaji. Kweli nitawasindikiza wananchi
wangu kuzima mitambo ili maji yasipelekwe Shinyanga, nasema kweli
nitafanya hivyo,” alisisitiza Kitwanga.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isaack Kamwelwe,
alikiri kuwa Rais wa awamu ya nne alitoa ahadi hiyo mwaka 2008 kwamba
wananchi wa maeneo ya Ihelela wataunganishiwa maji kutoka bomba la Ziwa
Victoria.
Hata hivyo, Kamwelwe alimuomba mbunge huyo asihamasishe watu kuzima mitambo hiyo wakati wowote badala yake wavute subira.
Katika
swali la msingi la Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako (CCM),
alitaka kujua Mto Malagarasi una ujazo gani wa maji na kama
yanatosheleza mahitaji.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri Kamwelwe alisema serikali imepanga kutekeleza
miradi mbalimbali kwa kutumia Mto Malagarasi ikiwamo mradi wa maji kwa
ajili ya miji ya Urambo, Kaliua pamoja na kilimo cha mwagiliaji na
uzalishaji umeme wa megawati 44.5.
“Wakati
wa masika, mto huo unakuwa na maji yanayotiririka kwa mita za ujazo 55
kwa sekunde na wakati wa kiangazi unakuwa na mita za ujazo 40 kwa
sekunde," alisema.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment