MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu jana ametoa pasi ya bao timu yake, AFC Eskilstuna ikipata sare ya 1-1 na Elfsborg zote za Ligi Kuu ya Sweden katika mchezo wa kirafiki nchini Hispania.
Katika mchezo huo uliofanyika mjini Barcelona,
Ulimwengu aliyejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa Januari, alimsetia
mshambuliaji wa Nigeria, Chidi Dauda Omeje kufunga bao hilo la AFC
Eskilstuna.
Akizungimza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwa simu
kutoka Hispania, Ulimwengu alisema kwamba anamshukuru Mungu ameanza
vizuri katika timu yake mpya.
Thomas Ulimwengu jana ametoa pasi
ya bao timu yake, AFC Eskilstuna ikipata sare ya 1-1 na Elfsborg “Leo
(jana) tumecheza mechi ya kirafiki tumetoa sare ya 1-1 na mimi ndiye
nimetoa pasi ya bao letu,”alisema mchezaji huyo aliyekaribia kusajiliwa
Yanga mwaka 2012 akitokea Moro United, lakini akachagua kwenda AFC
Eskilstuna, ambayo baadaye ilimuuza TP Mazembe.
Kwa wiki nzima sasa, Ulimwengu yuko Hispania na klabu yake hiyo mpya, AFC Eskilstuna kwa maandalizi ya Ligi Kuu ya Sweden.
Ulimwengu
amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa
inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United akitokea TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Ulimwengu aliyezaliwa Juni
14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka
2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu
ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda
akademi ya AFC Eskilstuna ya Sweden, alikocheza hadi 2011 TP Mazembe
alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.
Alicheza U-20 ya Mazembe
kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na
moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba
wake Oktoba mwaka jana.
Ulimwengu anajivunia kushinda mataji makubwa
akiwa na Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na
pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment