WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Malik Mussa jana amecheza dakika zote 90 timu ya vijana ya Tenerife ikilazimishwa sare ya 0-0 na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia katika mchezo wa kirafiki.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwa simu, Farid alisema kwamba walikutana na timu nzuri ya Zambia katika mchezo mzuri wa kirafiki.
“Jamaa nilizungimza naop baada ya mechi nikawaambia mimi ninatoka Tanzania, wakafurahi sana na wakaema nitafika mbali nisivunjike moyo, mimi ni mchezaji mzuri,”alisema Farid.
U20 ya Zambia ipo Hispania kwa kambi ya siku 10 kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrikaya Vijana na watacheza pia na U-20 za Las Palmas, Real Madrid na Barcelona.
Zambia
ndiyo wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika la U20 na wataanza kampeni
yao ya kuwania taji hilo nyumbani kwa kumenyana na Guinea Februari 26
mwaka 2017 Uwanja wa Heroes.
Farid alijiunga na klabu hiyo ya Santa
Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary Desemba mwaka jana kwa
mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
Azam
FC ilimtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum
baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana
alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa.
Farid
alitua Hispania kwa mara ya kwanza Aprili 21, mwaka jana baada ya
kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya
Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya
mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
Na ilimchukua
wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na
kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo
Desemba, 2016.
Na baada ya kutua Tenerife amepangiwa kuanza kuchezea
kikosi cha U23 ili kupata uzoefu kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza
kinachocheza Ligi Daraja la Kwanza nchini humo, maarufu kama Segunda.
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment