Wednesday, 5 April 2017

Download wimbo mpya wa Rayvanny & Bahati unaoitwa "Nikumbushe".





Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Majibu ya Spika wa Bunge yawakela baadhi ya wabunge Bungeni.Fahamu zaidi hapa.






Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

SUTI WATAKAZOVAA SERENGETI BOYS WAKIWA SAFARINI HIZI HAPA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

VIJANA WA SERENGETI BOYS WATAVAA SUTI HIZI WATAKAPOKUWA SAFARINI AU KWENYE HAFLA SEHEMU MBALIMBALI.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Baada ya Zitto Kumpongeza JPM kwa Kumteua Kitila..Mange Kimambi Amshushia 'Kichambo' Hiki Kizito.ahamu zaidi hapa.

Aisee Zitto unazingua …. Yani umeongea kama msemaji wa Ikulu sio opposition!! Seriously naomba ukajisikilize Tena kwenye Hii clip Yani umesound kama publicist wa Magufuli…. So sad yani ….Ndo maana hukutia mguuu clouds?? Nyie ndo tunawategea mkamwajibishe Rais kwa utumishi mbovu Alafu unakuja kumlamba lamba na kumsifia Hapa? .. Aisee upinzani uko South Africa tu kwa kina Malema huku kwetu bado sana!!! #LipumbaJR
.
.
Magufuli alichokifanya Hapa ni kuwatenganisha upinzani… Na wewe umemruhusu afanye hicho kitu…… Yani in short umemsaidia Magufuli kudhoofisha upinzani. Kweli Zitto unasema Rais anaondoka kwenye kutenganisha watu, hivi ni kwamba huoni nchi ilivyotenganika kwa Sasa sababu ya Bashite? Very disappointed Na Huyu mtu! Yani I always thought Chadema ndo walimkosea huyu kaka Ila dah huyu jamaa mbaya kushinda Lipumba! Yani Zitto sio mtu!!!!
.
.
.
Na hamuwezi kuelewa why naongea Hivi, Jamani mimi kuna mtu wa CCM aliniapia Miungu yooooote just a few months ago wakati namposti posti Zitto kama opposer wa Magu..akaniambia wewe achana Na Zitto kabisaaa humjui na wala you don’t know how the system works. Hapo Zitto anapiga kelele anatafuta pakumshikia Magu akipapata utamuona atakavyobadilika kama sio yeye… anatafuta pa kumshikia Magu kama alivyomshikaga JK mpaka wakamake a deal akaacha kuichokonoa serikali ya JK.Same thing Na Magu hapo anampa Magu jamba jamba mpaka Magu aingie line Alafu atatulia ataacha kuichonoa serikali kwa issue nzito Yani atabaki kama vile anagusia gusia tuu Ila sio ile kumu-Attack full kama mwanzoni…. Leo kanichekaaaa mnoooooo ananiambia haya mama much know umeona eeeeh??? Wewe bado mtoto mdogo huijui system sisi ndo tunaijua system, Doh, limenishuka shuuuu! Maana nilivyokuwa namtetea Zitto utasema nna undugu nae!!! .


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

VIDEO: ‘Hatukubaliani na Matokeo na Tutakwenda Mahakamani’ -Freeman Mbowe.

April 5, 2017 Bunge limepiga kura za kuwapitisha wawakilishi wa bunge la Afrika Mashariki ambapo wagombea saba pekee ndio waliopitishwa kwa kupigiwa kura za ndio huku sita kati yao wakitokea Chama cha mapinduzi (CCM) na mmoja Chama cha wananchi CUF huku wagombea wawili wa CHADEMA wakikosa sifa baada ya kupigiwa kura nyingi za HAPANA.

Nje ya ukumbi wa Bunge Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe ameongea na waandishi wa habari na kusema kuwa hawakubaliani na matokeo na watakwenda Mahakamani.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

A - Z ya Binti Aliyejitupa Bahari Juzi Wakati Akirudishwa Kwao Zanzibar.Fahamu zaidi hapa.

KISA cha binti mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa kutokana na miaka yake) kujitupa baharini akiwa katika boti ya Kilimanjaro V akitoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar juzi, kinaanzia kwenye mawasiliano yake na mvulana mmoja, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, imefahamika.

Msichana huyo alikuwa akiwasiliana na mvulana huyo ambaye walifahamiana kupitia Facebook, kwa kutumia simu ya mkononi.

Nipashe ilifika Kikwajuni, nyumbani kwa msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu (shule inahifadhiwa) na kuikuta familia yake ikiwa na majonzi, huku wakiwa hawaamini kilichotokea na binti huyo akiwa bado hai.

Akizungumza kwa huzuni, mama mdogo wa msichana huyo, Asha Saleh Mandhi, alisema palitokea mzozo baina yake na binti huyo baada ya kumkuta na simu ya mkononi wakati wazazi wake hawajamnunulia.

Alisema Jumatano iliyopita majira ya jioni akiwa nyumbani hapo na baada ya kupata taarifa kuwa mtoto wake wa kumlea anamiliki simu, alimwita na kumtaka aeleze amepewa na nani la sivyo atampeleka polisi akajieleze.

Alisema siku ya pili yake asubuhi, msichana huyo alitoroka nyumbani na ndipo alipotoa taarifa kituo cha polisi Madema kuwa amepotelewa na mtoto.

“Mimi ndiye ninayemlea huyu mtoto. Kwa kweli sijui amefikwa na mtihani gani kwa sababu hatujampa simu, lakini nashangaa tumemkuta na simu na hakutaka kumtaja aliyempa," Asha alisema.

"Kitendo cha kumuuliza ndicho kilichomfanya kukimbia na kwenda kusikojulikana.”

Mama mdogo huyo alisema baada ya kuwa ametoroka, aliichukua simu hiyo na kuangalia mawasiliano yake na ndipo alipofanikiwa kupata jina la kijana mmoja wa kiume ambaye alikuwa anawasiliana naye mara kwa mara. Hakumtaja.

Alisema baada ya kumpata kijana huyo kwa njia ya simu, aliulizwa anamfahamu vipi binti yao na kujibu kuwa wamejuana kupitia Fecbook, lakini hawajawahi kuonana kwa sababu yeye anaishi Dar es Salaam na binti anaishi Zanzibar.

Alisema alimpa taarifa kijana huyo kuwa binti yao ametoroka na haijulikani alikokwenda, hivyo kumwomba kusaidiana kuhakikisha wanampata akiwa salama.

“Kwa kweli huyo kijana alikubali kutoa ushirikiano na akawa anawasiliana na binti yetu na kumueleza kuwa yuko Dar es Salaam na amehifadhiwa na dereva teksi baada ya kukosa msaada wa eneo analotaka kwenda ambako ni kwa bibi yake anayeishi Mburahati, Dar es Salaam,” alisema.

Alisema aliwasiliana na dereva huyo ambaye alimueleza kuwa amesharipoti katika serikali ya mtaa katika eneo analoishi kuwa amemwokota binti huyo bandarini, Dar es Salaam baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kupata msaada.

Mama mdogo huyo alisema mama mzazi wa binti huyo anaishi Muscat, Oman na kwamba amemlea tangu akiwa mdogo.

Alisema walipata mshtuko baada ya kupata taarifa kuwa binti yao amejitupa baharini wakati akitokea Dar es Salaam baada ya kusakwa kwa siku kadhaa na hatimaye kupatikana.

MFANYAKAZI WA NDANI
Mmoja wa mashuhuda na mfanyakazi wa ndani katika nyumba anayoishi manusura huyo alisema wakati akiwa katika boti wakitokea Dar es Salaam juzi, walipata taarifa kuwa kuna mtu amejitupa baada ya kufika Chumbe, lakini hakujua kuwa aliyejitupa anamfamu.

“Baada ya kupata taarifa kuwa kuna mtu kajitupa baharini, tukaanza kupiga kelele na nilimwona akielea baharini, lakini nilijua ni mtoto wa kizungu bila kufahamu kuwa nilikuwa namfahamu,” alisema Hiyari Miraji Othman.

Alisema alikuja kufahamu kuwa anamfahamu manusura baada ya saa nne na kwamba hakutegemea angeweza kufanya kitendo hicho.

Alimwelezea msichana huyo kuwa ni mpole na mwenye nidhamu kwa kuwa amekuwa akimuona hivyo nyumbani kwao Kikwajuni kwa muda mrefu.

“Hapa kwao nakuja kila siku kwa sababu ndipo penye kibarua changu," alisema.


"Hapa huwa tunapika vyakula kwa ajili ya biashara na huwa namwona tabia zake ni mtoto mzuri anayejielewa.”

Credit - Nipashe


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Matokeo ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki......Wabunge Wote wa CHADEMA Wapingwa.Fahamu zaidi hapa.

Jana Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipiga kura kuchagua wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kwa kipindi cha miaka mitano.

Baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu uchaguzi huo, ulifanyika na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza orodha ya washindi waliochaguliwa kuiwakilisha nchi.

Tanzania inatakiwa kutoa wabunge 9 kwenda EALA, lakini matokeo ya jana yalitangaza washindi saba tu baada ya wagombea wawili kupigiwa kura nyingi za hapana, na hivyo kuonekana kuwa wabunge hawakuwataka.

Kati ya wabunge 7 waliotangazwa, 6 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja na wa Chama cha Wananchi (CUF).

Wagombea wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipingwa kwa kupigiwa kura nyingi za hapana.
  1.      Fancy Nkuhi (CCM)
  2.     Happiness Legiko (CCM)
  3.     Maryam Ussi Yahya (CCM)
  4.     Dkt Abdullah Makame (CCM)
  5.     Dkt Ngwaru Maghembe (CCM)
  6.     Alhaj Adam Kimbisa (CCM)
  7.     Habib Mnyaa (CUF)
Baada ya matokeo hayo kutangazwa, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge alisema kuwa, hawayakubali matokeo hayo na kuwa watakwenda mahakamani.

Mbowe pia amemtuhumu Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika katika mchakato wa kuwakataa wagombea wa CHADEMA na kusema kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa na kasoro.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Polisi Dar watumia silaha kuwatawanya wafanyabiashara Mwenge.Fahamu zaidi hapa.

Jeshi la Polisi limetumia silaha za moto kuwatawanya wafanyabiashara katika eneo la Mwenge, wilayani Kinondoni leo.

Taharuki iliwakumba wakazi wa eneo hilo mara baada ya polisi hao kuanza kuwatanya wafanyabiashara hao waliofunga barabara wakishinikiza magari yaruhusiwe kupaki katika eneo hilo.

Inaelezwa kuwa polisi wamezuia watu  kupaki magari katika eneo hilo  hali iliyosababisha wafanyabiashara hao kutofungua biashara zao leo.

Mmoja wa wafanyabiashara na shuhuda wa tukio hilo, Musa Godwin alisema polisi walifika sokoni hapo saa12 asubuhi na kutawanya wafanyabiashara waliofunga barabara kuzuia polisi magari yasiegeshwe eneo hilo.

"Walifika hapa sokoni saa 12 asubuhi na baadhi ya watu walifunga njia ikasababisha polisi wapige risasi hewani, hadi sasa wanazunguka hapa kuzuia magari ambao ni wanunuaji wetu," alisema Godwin.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Tuesday, 4 April 2017

Kimenukaa..Spika Ndugai Afunguka Mazito Baada ya Wabunge Kumshangilia Kupita Kiasi Rais Kikwete Wakati wa Kikao cha Bunge Leo.Fahamu zaidi hapa.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameshangazwa na jinsi wabunge walivyomshangilia Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kuelezea kuwa hakuna mgeni aliyewahi kupata shangwe kama hizo.
Rais Mstaafu huyo ameshangiliwa kwa muda mrefu mara baada ya kuingia bungeni leo asubuhi alipoenda kumshuhudia mke wake, Mama Salma akiapishwa tangu ateuliwe kuwa mbunge.
“Waheshimiwa wabunge, binafsi mimi ni kipindi cha nne humu bungeni sijawahi kuona mgeni amepokelewa kwa kiwango hiki,” alisema Spiga Ndugai huku akicheka kwa furaha.
Ikumbukwe kuwa Bunge limeanza leo mjini Dodoma.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Hataree..Huu Ndio Ujumbe Alioandika Kikwete Baada ya Wabunge Kumshangilia Sana Bungeni Leo.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya kupokelewa kwa shangwe katika ukumbi wa bunge leo hii, Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema ni zamu yake kwa sasa kumuunga mkono mkewe Mama Salma Kikwete.
Kikwete aliyekuwa ameambatana na familia yake, ameshuhudia mkewe akila kiapo cha ubunge katika kikao cha kwanza cha bunge lililoanza leo mjini Dodoma.
Salma Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa WAMA, alionekana kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono mumewe wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kulitumikia taifa.
“Leo asubuhi nmeshuhudia kiapo cha mke wangu, mheshimiwa Salma Rashd Kikwete kuwa mbunge wa kuteuliwa bungeni Dodoma. Ni zamu yangu kumuunga mkono,”alinukuliwa Kikwete katika akaunti yake ya twiter.
Kikwete aliingia ndani ya bunge hilo huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa bunge hilo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Harmonize Hawezi Nipiga Chini – Jack Wolper Afunguka.Fahamu zaidi hapa.

Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka kwa kudai kuwa mpenzi wake wa sasa Harmonaze hana uwezo wa kumuacha kimapenzi pamoja na tetesi ambazo zimekuwa zikisikika kwamba mwanamuziki huyo kuwa ana warembo wengine anaotoka nao kimapenzi.


Wawili hao kwa sasa wako karibu zaidi baada ya wiki chache zilizopita kudaiwa wameachana.

Akiongea na mtandao wa Central Filamu wiki hii, Wolper amedai yeye na Harmonize wako vizuri na hawadhani kama wenaweza kutengena hivi karibuni.


“Wengi wanaongea sana kuhusu mpenzi wangu kama anatoka na wanawake wengi pengine inaweza kuwa ndio sababu ya kuniacha mimi hicho hakiwezekana wanaongea kama kuna wasichana wanajipendekeza watachezewa tu,” alisema Wolper.

Muigizaji huyo amedai Harmonaze hana uwezo wa kumwacha kwani yeye ni muhimu kwake.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Ukweli Mchungu..Haya Ndiyo Madhara ya Kutisha ya Kufanya Ngono Kinyume na Maumbile.Fahamu zaidi hapa.

Ngono kinyume na maumbile au wengine husema Ngono kwa nyia ya haja kubwa, ni hali ya kingono ambayo muhusika huingiza uume katika njia ya haja kubwa kwa lengo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo ili kujirishiza hisia zake.
Watu ambao wanajishughulisha na kushiriki katika ngono ya nia hii ya kinyume na maumbile wapo katika hatari kubwa ya kiafya, kwa sababu njia ya haja kubwa inazungukwa na mishipa/neva nyingi sana zipo eneo hilo ambalo kazi zake si maalumu kwa tengo la ngono kwa kuingiziwa kitu ambacho hakistahiri eneo hilo.
Ambapo kwa utafiti uliofanyika Nchini Tanzania uliohusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miakan 15 na kuendelea na iliyohusisha kada tofauti katika jamii kama wanafuzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa, wauguzi, makahaba na kina mama wa majumbani katika maeneo tofauti. Watu waliojitokeza ni 903 wakiwemo pia wanaume walihusika katika tafiti hiyo.
Utafiti huo ulisema wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wamewahi kufanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambao ni sawa na asilimia 27 huku asilimia 73 ya waliohojiwa walidai kufahamu njia hiyo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, katika Utafiti huo ulifanywa na Irene Mremi kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Nchini Tanzania.
Inakadiriwa kuwa asilimia 90% ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao (mashoga) huwa wanajihusisha na ngono kinyume na maumbile.
JE, NGONO KINYUME NA MAUMBILE NI SALAMA?
HAPANA, Ngono kinyume na maumbile si salama kwa sababu ina madhara mengi kiafya kama yafuatavyo;
MOJA, Njia ya haja kubwa haina vilainishi/lubrication asilia kama jinsi Uke ulivyo.
Hivyo wakati wa tendo la ngono husasani wakati wa uingizaji wa uume huwa inasababisha kuchubuka kwa tisu/ngozi laini ndani ya njia ya haja kubwa hiyo, na hivyo kupelekea michubuko ambayo bacteria, virusi na hata vimelea vingine kuweza kupenyea wakati wa majeraha hayo ya michubuko na hivyo kuingia katika mfumo wa damu kupitia majeraha hayo.Hii inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa pamoja na VVU.
Tafiti zinaonyesha ya kuwa Ngono kwa Njia ya haja kubwa ipo katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa zaidi ya asilimia 30% kuliko watu wanaotumia njia ngono kwa njia ya Uke.
Vile vile mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kupata virusi vya human papillomavirus (HPV ) ambavyo huweza kumpelekea mtu anayejihusisha na ngono kinyume na maumbile kupata muwasho katika eneo hilo la haja kubwa na hata kupelekea kupata kansa.
PILI, Tishu ndani ya njia ya haja kubwa, haijakingwa na kulindwa kwa ngozi ngumu kama ilivyo sehemu za nje za mwili. Tishu zote za nje ya miili yetu zina ngozi ambayo ni seli zilizokufa ambazo hutusaidia kutukinga dhidi ya maabukizi ya vimelea na vile vile hutulinda na vitu tofauti katika mazingira.
Hivyo ndani ya njia ya haja kubwa hakujakingwa na ulizi huo wa asili wa seli hizo ili kuweza kuhimili, hivyo kuifanya iwe katika hatari kubwa ya kusuguliwa na hivyo kuchanika ambayo hupekea kusababisha maambukizi kuwa rahisi kutokea.
Pia ngozi ndani ya njia ya haja kubwa iko tofauti na ile ya ukeni ambapo ngozi ya ukeni huweza kuhimili ile misuguano pasipo kuweza kusababisha michumbuko kwa sababu ya vilainishi asili vinavyoatikana ndian ya uke na gozi husika.
TATU, Njia ya haya kubwa ni Maalumu kupitisha Kinyesi tu.
Kwa jinsi ambavyo njia hii imeundwa ama kutengenezwa ni maalumu kwa kuhimili na kupitisha kinyeshi tu na si vinginevyo.
Njia ya haja kubwa imezungukwa na kama misuli mfano wa ringi ama kwa kitaalamu huitwa (Anal sphincter) ambayo kazi yake ni kukaza eneo hilo kabla na baada ya kujisaidia tu.
Kipindi ambapo misuli hiyo (anal sphincter)imekazwa ama kubwa kwa kuingiziwa kitu kingine kigumu huweza kusababisha maumivu makali kwa muhusika.
Panapoendelea kuwa na mrudio wa mara kwa mara wa ufanyaji wa Ngono kwa njia hii ya haja kubwa ama kinyume na maumbile hufanya misuli hiyo ya njia ya haja kubwa kuwa dhaifu ama kulegea na isiwe na uwezo tena wakukaza kama kazi yake inavyotakiwa kufanya. Na hivyo kuwa vigumu kuweza kuzuia kinyesi kuweza kupita mpaka utapokuwa tayari kuweza kukitoa hivyo kusababisha utokaji ovyo wa kinyesi.
NNE, Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi.
Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi sana tofauti na Ukeni kulivyo hata kama wapenzi hawana maambukizi yeyote ya zinaa au ugonjwa wowote bacteria huwa wapo tu eneo hilo na hawa ni bacteria wa kawaida (Normal flora).
Mtu anapokuwa naingiza uume ndani ya njia ya haja kuwa anakuwa anaingiza vimelea vingine vya bacteria katika eneo hilo na wanapokutana na wale bacteria wengine waliopo katika eneo hilo husababisha madhara.
Pia pale unapohamisha uume toka katika njia ya haja kubwa na kupeleka katika Njia ya Uke badi bacteria hao utawapeleka katika eneo Uke ambapo Njia ya haja kubwa inakuwa na bacteria wengi na hivyo kupelekea maambukizi ukeni na pia maambukizi katika njia mkojo.
Ngono kwa njia ya haja kubwa inaweza kusababisha madhara mengine kwa afya ya watu wanaojihusisha na Njia hii ya ngono na wanaweza kupata madhaara kama haya yafuatayo,
Pale mdomo unapogusana na njia ya haja kubwa au kugusa uume uliotoka kwenye njia ya haja kuwa kwa mdomo kunaweza kupelekea kupata kwa wote mtu na mpenzi wake kuwa katika hatari ya kupataa magonjwa ya HEPATITIS C, HERPES/ malengelenge, kupata virusi vya human papillomavirus (HPV) na maambukizo mengine.
Hata hivyo, majeraha makubwa wakati wa ngono kwa njia ya haja kubwa mara nyingine ingawa sio kila mara hali hii kutokea inaweza kupelekea Damu kuvuja kwa ndani (hemorrhoids) baada ya tendo hilo kufanyika ambalo inaweza kusababisha au kupasuka ama kuchanika kwa misuli/nyama ndani ya njia ya haya kubwa kwa sababu ya msuguano mkali na muda mwingine hupelekea kuweza kutoboka kwa utumbo mpana(colon) hii huweza kwa ni tukio la hatari zaidi ambalo huhitaji msaada wa kitabibu haraka kwa matibabu na hata kufanyiwa upasuaji zaidi na hata kupoteza maisha kunaweza kutokea.
TANO, pia kwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao kushindwa kuhimili kukaza kwakati wa kusukuma mtoto na hivyo inaweza kupelekea utokaji wa kinyesi wakati wa kusukuma mtoto. jambo ambalo huleta tabu kwa wahudumu wa afya kwa kutumia muda mwigi kuwahudumia.
Njia pekee ya kuepuka kabisa hatari hizo za ngono kinyume na maumbile ni kuacha kabisa ngono kwa njia hiyo ya haja kubwa.
shiriki katika ngono kwa njia ya kawaida na ikibidi kwa kutumia kondomu ili kujilinda dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Kuepuka kuingiza uume ndani ya uke na kisha mdomoni ikiwa uume ulikuwa umeingizwa katika njia ya haja kubwa.
Ikiwa umepata michubuko na kutoka damu baada ya ngono ama vidonda karibia na njia ya haja kubwa na hata katika maeneo ya uke basi onana na daktari wako haraka iwezekanavyo ili upatiwe tiba hii iakusaidi kuzuia maambukizi ya vimelea katika eneo la jeraha.
MADHARA ANAYOWEZA KUYAPATA MWANAUME ANAYEPENDA KUJIHUSISHA NA MCHEZO HUU WA NGONO NI KAMA IFUATAVYO;
KWANZA, Kunauwezekano wa Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa kwa sababu ya vimelea kuingia na kuziba ama kuingia kwa kinyesi katika njia ya haja ndogo hivyo kukuweka katika wakati mgumu utapohitaji kujisaidia haja ndogo.
PILI, unaweza kupata magonjwa ya saratani(kansa) ya tezi tezi Prostate gland.
TATU, Maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa sababu kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata maabukizi tofauti na kwenye njia ya Uke hii ni kutokana na kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata michubuko kiurahisi.
NNE, Kuathirika kisaikolojia hivyo mhusika kuandamwa na msongo wa mawazo kila wakati kujutia tendo hili baya.
Nina imanai ndugu msomaji wa makala hii umeweza kuona madhara mabaya sana ya tabia hii mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako ama kuingiliwa kwa namna hiyo na kuona raha lakini umeziona hasara zake, amabazo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.
Jiepushe kuiga mambo bila kujua hasara zake, pia usimtie mwenzako majaribu kwa kumlazimisha kufanya kitendo hiki na wanaume kwa kigezo cha kuachwa kwa lengo la kuwaingilia kinyume na maumbile kwa kuwatishia kuwaacha kama watakataa.
Kipi bora kuharibiwa ama kuachwa? Jibu unalo mhusika!!
Kumbuka baada ya kuharibiwa thamani yako inashuka mbele ya jamii. Kasha kupelekea kuingia katika msongo wa mawazo na mateso ya ugonjwa ama magonjwa utakayoyapata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.
UKWELI MCHEZO HUU UMEWAATHIRI SANA WANAWAKE NA WANAUME AMBAO WENGI WANAUJUTIA.
JIEPUSHE NA NGONO KINYUME NA MAUMBILE!!!!!


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Ukwepaji Kodi: TRA wawashusha Serengeti Boys njiani walipokuwa wakielekea kwa Makamu wa Rais.Fahamu zaidi hapa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania Wamewashusha Njiani Timu ya vijana chini ya miaka 17 TRA wakilitaka Basi lililokua limewabeba vijana hao ili kulipiga mnada waweze kulipa deni la kodi.

Ni hatua nzuri kama unashindwa kulipa madeni maana yake umefilisika na kama umefilisika Mali zako zitauzwa na Cha kwanza Kulipwa huwa Kodi kama unadaiwa na Wadai wengine

Hii ni Hatua nzuri na fundisho kwa Taasisi zingine zinazokwepa kulipa kodi na Alarm hii inaonesha kuwa Nchi hii si yawapiga dili tena.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Hatimaye The Undertaker Asataaf Kucheza Mieleka,Aaacha Gumzo Dunia Nzima.Fahamu zaidi hapa.

Marekani.Mashabiki wa mchezo wa mieleka WWE walitokwa na machozi mwishoni mwa wiki wakati mcheza mieleka mashuhuri The Undertaker alipotangaza kustaafu kucheza mchezo huo baada ya miaka 25.
 
Katika mchezo wake wa mwisho Undertaker alipigwa na Roman Reigns na kuondoka ulingoni akiwa na rekodi ya kushindi michezo 23 na kupoteza miwili  Wrestlemania.
 
Wakati akitoka ulingoni Undertaker alifanya kitu ambacho hajawahi kufunga hadharani kwa kwenda kumkumbatia mkewe Michelle McCool baada ya mechi dhidi ya Roman Reigns
 
Akithibisha kustaafu kwake mchezo huo Undertaker aliacha katikati ya ukumbi koti lake, kofia na glovisi zake na kuamsha shangwe kwa mashabiki wake.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

EFM yakanusha kurusha habari ya Prof. Kitila Mkumbo kukataa uteuzi wa Rais Magufuli.Fahamu zaidi hapa.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

Kauli ya ACT Wazalendo kuhusu Rais Magufuli kumteua Mwanachama wao , Prof. Kitila Mkumbo Kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.Fahamu zaidi hapa.

 Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. 
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na uzalendo wa kutumikia nchi yetu.

Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya Chama ikiwemo Kamati Kuu. 
Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu kama mshauri wa chama. 
Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Taifa utokanao na kila mwananchi, ndio msingi wa kaulimbiu yetu ya ‘Taifa Kwanza, Leo na Kesho’, hivyo basi tunamtakia kila la kheri ndugu Kitila katika utumishi wake kwa Taifa letu katika nafasi yake hii mpya. 
Wizara Hii ni kubwa na muhimu Sana kwa nchi yetu. Maji ni tatizo moja kubwa ambalo wananchi wetu wanakumbana nalo na Kama Taifa hatujaweza kulimaliza. 
Tunamtakia kila la kheri ndugu Mkumbo katika kuongeza nguvu kumaliza kero ya maji na kuhakikisha tunaimarisha Kilimo cha Umwagiliaji nchi nzima. Tunamsihi aanze na ajenda ya Mfuko wa Maji Vijijini na kuanzishwa Kwa Wakala wa Maji Vijijini utakaosimamia upatikanaji wa Maji Kwa wananchi wetu.

Kwa hatua hii, tunaona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu Kwa kufanya kazi na watu wote bila kuwabagua Kwa itikadi zao za vyama.
 Watanzania ni wamoja na kauli za kuwagawa zinaumiza zaidi Taifa kuliko kuliweka pamoja. Tunaamini kuwa Rais Ana nia njema katika uteuzi huu na sisi tumempa baraka zote Mwanachama wetu mwanzilishi wa Chama kwenda kwenye nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma. Tunaamini hatamwangusha Rais na muhimu zaidi hatawaangusha Watanzania.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo
Aprili 4, 2017
Dodoma
 


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MAYWEATHER AMWAGA SH MILIONI 84 KUNUNUA GARI LA ZAWADI KWA MWANAYE, AMPA FEDHA AGAWE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Bondia mstaafu, Floyd Mayweather ameendeleza nyodo ya fedha baada ya kumwaga kitita cha sh milioni 84 ambazo ni pauni 31,000 kununua gari la zawadi.

Mayweather maarufu kama Money, amenunua gari aina ya  Mercedes C-Class Coupe kwa ajili ya mwanaye Zion ambaye ametimiza miaka 16.

Pamoja na gari hilo la kifahari, wasanii kadhaa maarufu walitumbuiza katika pati hiyo ya siku ya kuzaliwa ya Zion huku yeye akiwa anamwaga fedha kama ilivyozoeleka kwa baba yake.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

EWURA Yatangaza bei Mpya Za Mafuta...Petroli Yashuka, Diseli Yapanda.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza mabadiliko ya bei za mafuta nchini zitakazoanza kutumika kuanzia kesho, huku mafuta ya petroli yakionekana kushuka.

Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na ya taa zimebadilika ikilinganishwa na beo za Machi Mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya ofisi za EWURA, Meneja Mawasiliano ma Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema, bei ya reja reja ya petroli imepungua kwa Shilingi tatu kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 0.13, pianbei ya jumla imepungua kwa Shilingi 5.65 kwa lita sawa na asilimia 0.29.

Aidha Kaguo amesema bei ya rejareja ya Dizeli imepanda kwa Shilingi saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 wakati bei ya jumla ikiwa imepanda kwa Shilingi 3.68 kwa lita sawa asilimia 0.21.

"Hii shilingi tatu inaweza kuonekana ni ndogo lakini ina impact () kubwa sana kwa jamii, kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei, pia gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita," amesema Kaguo.
==>Bei zota ziko hapo chini.....Tazama jedwali hili



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

SAFARI YA SERENGETI BOYS KWENDA MOROCCO KESHO MCHANAFAHAMU ZAIDI HAPA.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, inatarajiwa kusafiri kesho saa 10.45 jioni kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Morocco kupitia Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Timu hiyo yenye wachezaji 23 na viongozi wanane watakuwa Uwanja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere kuanzia saa 7.00 mchana kwani wanatakiwa kuanza kuingia uwanjani saa 7.45 kwani saa tatu baadaye ndipo ndege itakapopaa.

Wanahabari wanaweza kupata mahojiano ya mwisho kadhalika kupata picha za habari wakati huo wa mchana kabla hawajaingia ndani kwenye ukaguzi wa taratibu za (check in logistics).

Kabla ya kusafiri, timu hiyo ilikuwa kambini hapa nyumbani tangu Januari 29, mwaka huu na baada ya kambi ya mwezi mmoja na nusu, ilicheza mechi tatu za kirafiki za kimataifa.

Machi 30, 2017 ilicheza Burundi ‘Intamba Murugamba’ na kushinda mabao 3-0 kabla ya kurudiana tena Aprili 1, mwaka huu na kushinda mabao 2-0. Mechi zote mbili zilifanyika Uwanja wa Kaitaba, ulioko Bukoba mkoani Kagera.

Mechi ya mwisho hapa nyumbani ilifanyika Aprili 3, mwaka huu dhidi Ghana ‘Black Starlets’ na kutoka sare ya 2-2 katika mchezo ulifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Serengeti Boys ilitumia mchezo kama ishara ya kuwaaga mamilioni ya Watanzania kabla ya kusafiri kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.

Serengeti Boys itakuwa Rabat, Morocco kufanya kambi ya takribani mwezi mmoja kuanzia Aprili 5, mwaka huu. Ikiwa huko angalau itacheza mechi za kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji morocco na timu nyingine ya jirani ama Tunisia au Misri.

Kambi hiyo ya Morocco itamalizika Mei mosi, mwaka hu ambako timu itasafiri hadi Cameroon. Ikiwa Cameroon, timu itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji yaani Mei 3 na 6, mwaka huu kabla ya kusafiri Mei 7, mwaka huu kwenda Gabon ambako Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.

Vipimo vya mechi dhidi ya Ghana kadhalika hapo baadaye Cameroon, vitakuwa mwafaka kwenye kufanya tathmini ya uwezo wa Serengeti Boys kwani wapinzani hao wamekuwa na rekodi nzuri kwenye soka la vijana na kwa kipindi hiki zimepangwa kundi A pamoja na wenyeweji Gabon na Guinea.


Kila la kheri Serengeti Boys katika mapambano ya kuwania ubingwa wa Afrika kadhalika kucheza fainali za Kombe la Dunia hapo Novemba, mwaka huu zitakazofanyika India. Serengeti Boys inaweza na Mtanzania tunakuomba kuichangia timu hii kwa namna ya 223344 kupitia mitandao yote ya simu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MBARAKA YUSUPH ABEID ALIYEIUA SIMBA, MCHEZAJI BORA WA VPL MACHI 2017.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi kwa msimu wa 2016/2017.

Mbaraka aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo kuisadia timu yake kupata matokeo mazuri.

Katika mwezi huo ilichezwa raundi moja tu na Mbaraka ambaye alicheza kwa dakika zote 90 aliisaidia timu yake kukusanya pointi zote tatu zilizoifanya timu yake kubaki katika nafasi ya nne (4) katika msimamo wa ligi kwa mwezi huo.

Katika mchezo huo mmoja, Mshambuliaji huyo alifunga goli moja, na alionyesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la kadi.


Kwa kushinda tuzo hiyo, Mbaraka atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania PLC.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

JPM awateua Kitila Mkumbo na Semakafu.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 04 Aprili, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Prof. Kitila Alexander Mkumbo anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.

Kabla ya Uteuzi huu Prof. Kitila Alexander Mkumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Leonard Akwilapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarishi amehamishwa na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).

Bi. Maimuna Tarishi anachukua nafasi iliyoachwa na Mussa Uledi ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambako anajaza nafasi iliyoachwa na Dkt. Leonard Akwilapo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Ave Maria Semakafu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Wateule hao wataapishwa kesho tarehe 05 Aprili, 2017 saa 3:00 Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa