Tuesday 4 April 2017

Kimenukaa..Spika Ndugai Afunguka Mazito Baada ya Wabunge Kumshangilia Kupita Kiasi Rais Kikwete Wakati wa Kikao cha Bunge Leo.Fahamu zaidi hapa.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameshangazwa na jinsi wabunge walivyomshangilia Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kuelezea kuwa hakuna mgeni aliyewahi kupata shangwe kama hizo.
Rais Mstaafu huyo ameshangiliwa kwa muda mrefu mara baada ya kuingia bungeni leo asubuhi alipoenda kumshuhudia mke wake, Mama Salma akiapishwa tangu ateuliwe kuwa mbunge.
“Waheshimiwa wabunge, binafsi mimi ni kipindi cha nne humu bungeni sijawahi kuona mgeni amepokelewa kwa kiwango hiki,” alisema Spiga Ndugai huku akicheka kwa furaha.
Ikumbukwe kuwa Bunge limeanza leo mjini Dodoma.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment