Tuesday 4 April 2017

Hataree..Huu Ndio Ujumbe Alioandika Kikwete Baada ya Wabunge Kumshangilia Sana Bungeni Leo.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya kupokelewa kwa shangwe katika ukumbi wa bunge leo hii, Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema ni zamu yake kwa sasa kumuunga mkono mkewe Mama Salma Kikwete.
Kikwete aliyekuwa ameambatana na familia yake, ameshuhudia mkewe akila kiapo cha ubunge katika kikao cha kwanza cha bunge lililoanza leo mjini Dodoma.
Salma Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa WAMA, alionekana kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono mumewe wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kulitumikia taifa.
“Leo asubuhi nmeshuhudia kiapo cha mke wangu, mheshimiwa Salma Rashd Kikwete kuwa mbunge wa kuteuliwa bungeni Dodoma. Ni zamu yangu kumuunga mkono,”alinukuliwa Kikwete katika akaunti yake ya twiter.
Kikwete aliingia ndani ya bunge hilo huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa bunge hilo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment