Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya ziara
ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam mapema leo na kubaini
upotevu wa makontena 349.
Waziri
Mkuu amebaini upotevu wa makontena hayo ambayo yana thamani ya zaidi ya
shilling bilioni 80, na kuagiza kufutwa kazi mara moja kwa maafisa
waliohusika na upotevu huo.
Majaliwa amewasimamisha kazi Kamishna wa Kodi, Tiagi Masamaki pamona na Habibu Mpozya wa kitengo cha huduma kwa wateja.
Uamuzi
huo wa Waziri Mkuu umekuja baada ya kubaini kuwa katika kumbukumbu za
Mamlaka ya Bandari kuna taarifa ya makontena 349 yenye thamani ya
shilingi bilioni 80 lakini taarifa hizo hazipo kwenye kumbukumbu ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Waziri Mkuu ameelekeza Polisi kuwakamata maafisa wote waliohusika na sakata hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
0 comments:
Post a Comment