Kufuatia
agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa
wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua
na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na
mbili wanaohusika na wizi huo.
Akiongea
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa,
uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa
kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili ambao wamehusika na wizi
huo.
“Kati
ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika
watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.
Wanaoshikiliwa
kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru
TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na Bi.
Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa
wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha
Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa
Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.
Aidha
Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali
za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu
yake.
0 comments:
Post a Comment