Mstahiki Meya wa Maspaa ya Ubungo Bonface Jacob ameeleza kuwa Jiji la Dar es Salaam limeshindwa kusonga mbele kwa maendeleo kutokana na hujuma
Ametaja wa Mradi wa Maendeleo wa jiji la Dar es Salaam(DAR ES SALAAM METROPOLITAN DEVELOPMENT PROJECT DMDP) Chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
Benki ya Dunia ilikubali kugharamia mradi huu kwa kiasi cha USD 300 millioni (zaidi ya Sh600 bilioni za Kitanzania) kwa halmashauri zote za Jiji la Dar es salaam.
Mradi ulilenga maeneo mahususi yafuatayo;
1. Barabara za mitaani (feeder roads) jumla ya barabara 11 kwa Halmashauri ya Kinondoni wakati huo.
Makumbusho 1.3 Km, MMK 1.2 Km, Nzasa 1.2 Km, Tanesco Mikocheni 1.5 Km, Viwandani 1.75 Km kwa zisizo hitaji fidia
Na zinazohitaji fidia ni
Makanya 5.1 Km, Tandale-Mwananyamala 0.8 Km, Simu 2000 1.3 Km (Ubungo), Kilimani 1.3 km (Ubungo), Korogwe-Kirungule 3.0 Km (Ubungo), Kilongawima 1.8 Km, Sinza Kijiweni-Makanya-Morocco 5.1 Km (Ubungo).
2. Usimamizi wa Takataka Ngumu (Solid Waste Management)
3. Uboreshaji wa Miundombinu kwenye maeneo yasiyo pangwa (Infrastructure upgrading on unplanned statements).
Makusudio yalikuwa kupagusa Mwananyamala, Mburahati na Tandale.
4. Uimarishaji wa Taasisi (Institutional strengthening) uliolenga uimarishaji wa uwezo wa Halmashauri na ukusanyaji mapato.
5. Mifereji ya maji ya mvua (Storm Water Drainage) ujenzi wa Mto Ng'ombe wenye urefu wa 8.2 Km kuanzia Ubungo (UDSM) hadi Hananasif
6. Uwekezaji wa pamoja katika sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) kwa eneo la Kiwanja Na. 2005/2/2 kitalu c Sinza (simu 2000).
MIRADI ILIYOKWAMA UBUNGO
1. Barabara ya simu 2000 (Sinza) kiasi cha Sh1.85 bilioni, fedha za Benki ya Dunia.
2. Barabara ya Kilimani (Manzese) Sh1.76 bilioni.
3. Barabara ya Korogwe-Kirungule (kimara) Sh4.39 bilioni.
4. Ujenzi wa Mto Ng'ombe kuanzia Daraja la UDSM(Ubungo) mpaka Suna-Hananasifu 8.3 Km Sh20.1 bilioni.
5. Barabara ya Sinza Kijiweni-Makanya-Morocco 5.1 Km Sh6.54 bilioni.
Sababu za miradi kukwama
Kwa kuwa Benki ya Dunia ilikubali kulipa kiasi chote cha fedha, USD 300 million (zaidi ya Sh600 bilioni), masharti ya Benki ya Dunia juu ya Mradi yalikuwa kama ifuatavyo;
1. Miradi yote ya moundombinu kama kuna utanuzi wananchi walipwe fidia kabla ya kuvunjiwa nyumba zao wakati wa mradi.
2. Halamshauri ndizo zitafute fedha za kugharamia fidia kwa watu wake.
Hivyo kwa Miradi ya awamu ya kwanza pekee Manispaa za ubungo na Kinondoni kabla ya kugawanywa zilipaswa kupewa kiasi cha Sh51 bilioni. Hata hivyo, kwa mashati kwamba zilitakiwa kuwa Sh14 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia watu ambao wangepisha upanuzi wa miundombinu.
Hivyo Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni 2016/217, liliidhinisha mpango wa kukopa fedha kiasi cha Sh14 bilioni kutoka Benki ya CRDB, kwa ajili ya kupata fedha za kuwalipa wananchi wanaodai fidia kwa kuwa miradi ya Benki ya Dunia haiendelei kama kuna manung'uniko ya wananchi kuvunjiwa bila kulipwa fidia.
MIPANGO HUJUMA KUBWA SANA
Baada ya baraza la madiwani kukubali azimio hilo la mkopo wa CRDB Sh14 ili kufanikisha kupata msaada huo wa Benki ya Dunia.
Vilevile Benki ya Dunia walitoa idhini ya kuendelea kwa miradi ya Sh25 bilioni, iliyohusu miradi isiyohitaji fidia.
Na utaratibu wa kupata fedha hizo za mkopo benki kwa ajili ya fidia, unataka SERIKALI KUU kutoa Government Guarantee ambayo inasainiwa na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Fedha ili kuiruhusu Benki kuikopesha Manispaa.
Sasa basi, kwa vile Halamshauri ya Kinondoni ilikuwa chini ya wapinzani, SERIKALI KUU iligoma kusaini government guarantee wakati Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyopo chini ya CCM, walikubaliwa haraka sana kukopa fedha kama hizo katika benki hiyohiyo ya CRDB.
Sasa ni zaidi ya miaka miwili, mabillioni tuliyokuwa tusaidiwe na Benki ya Dunia, yamekaa tu, na hakuna anayejali.
BENKI YA DUNIA WAMEANZA KUKATA TAMAA-NA HAWAPEWI USHIRIKIANO
Benki ya Dunia wameanza kukata tamaa juu ya mradi wa DMD kupitia barua yao ya Mei 02 2017. Mkurugenzi wa Benki ya Dunia ya tawi la Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird, aliandika kuitaka Serikali Kuu na Wadau kukaa kikao cha pamoja kujua sababu za kuchelewa kwa miradi hiyo au kama Serikali bado ina uhitaji wa miradi hiyo.
Barua hiyo nakala iliwasilishwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango-Bw DOTO JAMES. Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI-MUSA IYOMBE
Barua ya pili ikaandikwa kuja kwetu viongozi wote wa Halamshauri za Dar es Salaam, na Serikali Kuu Mei 22, 2017 kuanzia Ngazi ya wizara-mkoa-mpaka wilaya, iliyoandikwa na Eric Dickson, Mkuu wa Maendeleo ya Miji na Udhibiti wa Majanga.
Katika barua hiyo, Eric Dickson, alitaka kiitishwe kikao cha pamoja Juni Mosi, 2017, Alhamisi, ambacho kwa masikitiko viongozi wote waligoma kutokea kikaoni hali iliyosababisha wafadhili kuondoka ukumbini(Millenium tower) bila suluhu.
Hawajui ya fedha hizo,tarehe 19 june nilifika ofisi za benki ya Dunia kuongea na wadadhili,wamekata tamaa kabisa na hawajui sababu ya kususiwa na kugomewa kupata ushirikiano.
Haya ndiyo mambo ambayo yanasikitisha. Fedha ni za Benki ya Dunia. Kinachotakiwa ni Serikali Kuu kuridhia Manispaa ikopeshwe ili kufanikisha miradi hiyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment